Monday 17 March 2014

EPL: MANCHESTER UNITED HOI KWA LIVERPOOL



Manchester United jana walionekana kutojielewa kabisa katika game kali dhidi ya wapinzani wao wa siku nyingi Liverpool...Man U walionekana wazembe na wamechanganyikiwa na pamoja na kusaidiwa na refa hawakubebeka na wakala kichapo cha magoli 3-0...Gerrard alipachika mawili kupitia matuta na alikosa tuta moja...Suarez alipachika la 3 dakika ya 84...Vidic alipewa kadi nyekundu baada ya foul ndani ya box kwa Sturridge lakini baadae ilionekana Sturridge alipiga mbizi...Gerrard alishindwa kufunga penalty iliyotokana na hiyo foul...Refa pia badae alipeta foul aliyofanyiwa huyo Sturridge na kusema ameteleza...Fellaini alionekana kama sio mchezaji wa Man U na timu nzima ilionekana kama haijui inataka nini...Bofya hapa upate habari zaidi

No comments:

Post a Comment