Thursday, 13 March 2014

TAIFA STARS: TAIFA STARS VS. SUDAN | 1972

Rais wa zamani wa Sudan Jaafar Muhamad an-Nimeiry akisalimiana na Omar Zimbwe (Africa Sports-Tanga)

Taifa Stars wakisalimiana na Rais (wa zamani) wa Sudan Jaafar Muhamad an-Nimeiry mwaka 1972 katika mechi ya kirafiki na Sudan siku ya sherehe ya Saba Saba...Walikutana kusherekea miaka 18 ya TANU (Tanganyika African National Union).


Timu yetu ilikuwa na hawa wafuatao:   

Kipa Mahadhi (African Sports, Tanga), Beki kulia Mweri Simba (Tanga), Beki kushoto Chuma (Nyota Mtwara), Namba nne Hassan Gobbos (Yanga), Beki tano Omar Zimbwe (African Sports, Tanga), Kiungo namba sita, Nahodha Abdulrahman Juma (Yanga), Wingi ya kulia Willy Mwaijibe (Simba), Kiungo namba nane Sunday Manara (Yanga), Namba tisa Kitwana Manara (Yanga), Namba 10, Kibaden (Simba) na Wingi ya kushoto Nassor Mashoto (Zanzibar).
 
Akiba: Kipa Elias Michael (Yanga), Kiungo Mohammed Msomali (Cosmopolitan), Winga Kassim Manga (Morogoro), Namba 10 Gibson Sembuli (Yanga) na wengine wachache. Kocha; Paul West Gwivaha.
 
Max Sports inaenzi mchango wao mkubwa katika soccer nchini...

No comments:

Post a Comment