Tuesday 22 March 2016

NCAA TOURNAMENT 2016: MARCH MADNESS NOMA BALAA


Kwa wapenzi wa Basketball duniani March Madness ni kitu cha kuangalia...March Madness ni kipindi ambapo shule za vyuo Marekani vinachuana vikali mwezi March...Sasa kilichotokea mwaka huu ni mambo ambayo hayakutegemewa kabisa...Kwanza, tuanze na timu ya shule ya wasongo darasani ya Yale...



Yale wamewatoa wakali Baylor ambao ni namba 5 kwa ukali...Pili, Wichita State ambao karibu wasicheze wamewatoa wakali Arizona ambao ni namba 6 kwa ukali...Tatu, Arkansas-Little Rock ambao wamechukua kocha wa mwaka wa kwanza wamewatoa namba 5 Purdue...


Nne, namba 15 Middle Tennessee wamewatoa namba 2 Michigan State ambao ndio walikuwa wanatarajiwa kufika mbali sana dah...Imekuwa kali ya mwaka huu....Tano, Syracuse katimu ambao hata kasingekuwa ndani ya michuano ya NCAA wamewachapa vibaya Dayton na MTSU na kutinga 16 bora...


Sita, Iowa walichapa Temple ambao wazuri tu...Saba, Hawaii nao kwa mara ya kwanza wamechida game ya NCAA...Ngoja niishie hapo hebu pata habari zaidi kwa kubofya hapa.

No comments:

Post a Comment