Tuesday, 29 December 2015

HARLEM GLOBTROTTERS: LEGEND MEADOWLARK LEMON AFARIKI DUNIA



Kama wewe ni mdau wa basketball utakuwa umewahi kuwasikia Harlem Globetrotters...Harlem Globetrotters ni timu ya basketball ambayo ina kipaji cha juu sana na wanakitumia hicho kipaji kufurahisha wapenzi wa basketball na watoto duniani...


Katika timu huyo Meadowlark Lemon alikuwa mmoja kati ya wakali wa timu hiyo miaka mingi iliyopita...Lemon alitaka kucheza basketball ya burudani toka alipokuwa anamiaka 11 alipoona timu ya watu wenye asili ya Africa kwenye tv...

Globetrotters ilianzishwa mwaka 1920 na Lemon ni kati ya jezi 5 tu zilizostaafu...


Wadau wengi sana wameenda kwenye mitandao ya jamii kumkumbuka Lemon akiwemo Shaq na Isiah Thomas...Meadowllark Lemon alikuwa anamiaka 83 alipofariki...Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Meadowlark Lemon...Bofya hapa upate bahari zaidi. 

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal Dif  Points
 1 Arsenal 19 15 39
 2 Leicester 18 12 38
 3 Tottenham 19 18 35
 4 Man City 18 17 35
 5 Crystal Palace 19 7 31
 6 Man Utd 19 6 30
 7 West Ham 19 5 29
 8 Watford 19 4 29
 9 Stoke 19 1 29
 10 Liverpool 18 -1 27
 11 Everton 19 7 26
 12 Southampton 19 3 24
 13 West Brom 19 -6 23
 14 Chelsea 19 -6 20
 15 Norwich 19 -10 20
 16 Bournemouth 19 -12 20
 17 Swansea 19 -8 19
 18 Newcastle 19 -15 17
 19 Sunderland 18 -18 12
 20 Aston Villa 19 -19 8

EPl: VAN GAAL AGOMA KUACHIA NGAZI


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema hakuna haja ya kuachia ngazi baada ya kutoka sare ya 0-0 na Chelsea jana...Manchester washindwa kushinda mechi 8 katika mashindano yote na wako points 5 nyuma ya timu ya nafasi ya 4...


Mashabiki waliomchoka van Gaal wanamtaka Jose Mourinho ambae alitimuliwa hivi karibuni...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 28 December 2015

EPL: ARSENAL YAANZA KUONJA KIPIGO CHA BAADA YA X MAS



Arsenal huwa baada ya x-mas inaharibu hasa ikiwa iko kati ta timu za juu ua ligi...Hii imeonekana kwenye mechi dhidi ya Southampton baada ya kuchapwa 3-0 na ni mechi Arsenal ilitakiwa kuchukua points 3 za bure kabisa lakini kwa Southampton imekuwa ngumu hata mechi za awali Southampton walifanikiwa kushinda mechi 3 kati ya 4...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 22 December 2015

EPL: ARSENAL YAONYESHA MATUMAINI YA KUCHUKUA KOMBE



Arsenal baada ya kuwachapa Manchester City 2-1 sasa wanaona wako tayari kufukuzia kombe la premiership...Kocha wa Arsenal amesema ushindi huu unawapa Arsenal imani kushinda kombe...Arsenal sasa iko points 3 mbele ya Man City lakini iko chini ya Leicester kwa points 2...Bao la Toure mwishoni halikuzaa matunda kwani makosa yao yalifanya Arsenal kuwakimbiza muda mrefu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 21 December 2015

FIFA: BLATTER NA PLATINI WAFUNGIWA MIAKA 8


Kutokana na uchunguzi wa masuala ya rushwa ndani ya Fifa, kamati ya nidhamu imewafungia Sepp Blatter na Michel Platini miaka 8 kutojihusisha na kitu chochote kinacho husu mpira...Kwa mujibu wa uchunguzi Blatter na Platini wametumia vibaya ofisi za Fifa wakati Blatter alipompatia Platini ponds za Uingereza milioni 1.3...Blatter amesema atatetea jina late na atatetea Fifa na kuna watu wanamchafulia jina lake...Blatter ambae ni mswiss na Platini ambae ni mfaransa wamepigwa faini ya pounds 33,700 (Blatter) na pounds 54,000 (Platini)...Bofya hapa upate habari zaidi.

FRANK LAMPARD: LAMPARD AFUNGA NDOA NA MCHUCHU WAKE WA MUDA MREFU

Bwana harusi
Frank Lampard, star wa Chelsea wa zamani na sasa anachezea New York City FC, ameamua kuacha ukapela na kumweka ndani mchumba wake wa long time Christine Beakley...
 
Redknap na Mrs walikuwepo...

Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu maarufu wakiwemo wachezaji wa Arsenal na Chelsea...
 
Branislav na Mrs pia walishuhudia...

Harusi hiyo iliyofana ilifanyika Knightsbridge katikati ya jiji la London...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal D. Points
 1 Leicester 17 13 38
 2 Arsenal 16 16 33
 3 Man City 16 15 32
 4 Tottenham 17 14 29
 5 Man Utd 17 8 29
 6 Crystal Palace 17 7 29
 7 Watford 17 5 28
 8 West Ham 17 4 25
 9 Liverpool 17 -2 24
 10 Everton 17 7 23
 11 Stoke 17 -2 23
 12 Southampton 17 0 21
 13 West Brom 17 -6 20
 14 Bournemouth 17 -10 19
 15 Chelsea 17 -6 18
 16 Norwich 17 -9 17
 17 Newcastle 17 -13 17
 18 Swansea 17 -9 15
 19 Sunderland 17 -15 12
 20 Aston Villa 17 -17 7


EPL: MATOKEO YA MECHI ZA WEEKEND

Sun 20 Dec 2015
Sat 19 Dec 2015

EPL: WATFORD YAISHANGAZA LIVERPOOL



Watford FC timu ndogo jana iliwashangaza Liverpool na mashabiki wake baada ya dakika 3 tu mpira ulivyoanza Nathan Ake, mdachi ambae ni mchezaji wa Chelsea aliyechukuliwa kwa mkopo, akatingisha nyavu...Baada ya hapo nae Odion Igalo akatingisha nyavu dakika ya 15 akipiga mpira mshazari kwenye angle ngumu...Dakika ya 85 huyo huyo mnigeria alipokea mpira kutoka kwa Valon Brahimi na kutingisha wavu...Bofya hapa upate habari zaidi.

LA LIGA: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal D. Points
 1 Barcelona 15 21 35
 2 Atl Madrid 16 14 35
 3 Real Madrid 16 27 33
 4 Celta de Vigo 16 6 31
 5 Villarreal 16 6 30
 6 Deportivo de La Coruña 16 9 26
 7 Ath Bilbao 16 6 24
 8 Sevilla 16 2 23
 9 Valencia 16 7 22
 10 Eibar 16 0 21
 11 Real Betis 16 -6 20
 12 Espanyol 16 -10 20
 13 Málaga 16 -4 17
 14 Real Sociedad 16 -5 16
 15 Getafe 16 -8 16
 16 Sporting de Gijón 15 -8 15
 17 Granada CF 16 -10 14
 18 Rayo Vallecano 16 -19 14
 19 Las Palmas 16 -11 13
 20 Levante 16 -17 11

LA LIGA: REAL YAICHABANGA RAYO VALLECANO 10-2



Gareth Bale alijipatia mabao yake 4 walivyowagaragaza Rayo Vallecano 10-2...Dakika ya 12 Real walikuwa nyuma 2-1 lakini mambo yakabadikika kwenye dakika takriban ya 25 hivi Bale alivyosawazisha na baada ya hapo ilikuwa mvua ya maoli tu...Karim Benzema nae alijipatia hat-trick...Ni mara ya kwanza toka mwaka 1960 Real imemfunga mtu mabao 10...Mwaka huo Real walimchapa Elche 11-2...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 19 December 2015

CHELSEA: GUUS HIDDINK BOSS MPYA CHELSEA



Chelsea wamepata kocha mpya wa kubadilisha mambo ndani darajaji...Guus Hiddink mwenye umri wa miaka 69 ataipeleka timu mpaka mwisho wa msimu...Amesema anaipenda Chelsea na kwa kuwa Chelsea ni moja ya timu kubwa duniani haistahili kukaa hapo ilipo...Kwenye game ya leo atakaa juu kwenye viti vya watazamaji akiwa na mmiliki wa timu Roman Abramovich...Bofya hapa upate habari zaidi.

MICHAEL JORDAN: JORDAN ASEMA LARRY BIRD ALIONGOZA KUONGEA OVYO NDANI YA COURT


Michael Jordan ambae ni Basketball legend amesema ingawa nayeye alikuwa anamdomo mchafu lakini aliyoongoza kuwa na mdomo chafu wakiwa wanacheza ni Larry Bird mchezaji wa zamani wa Boston Celtics...Alisema haya alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha maswali na majibu ya 20th annual Michael Jordan Flight School ndani ya Santa Barbara, California...


Alisema forward huyo wa zamani wa Boston Celtics alikuwa anamdomo mchafu lakini sio kwa maneno mabaya...Bofya hapa uangalie Jordan anavyoosema.

PEP GUARDIOLA: RIO FERDINAND ANATAKA MANCHESTER KUMCHUKUA PEP HARAKA



Kocha bora duniani ataondoka Bayern Munich mwisho wa msimu na beki wa zamani wa Manchester United, Rio Gavin Ferdinand, ameseka inabidi Man U wamnyakue Pep Guardiola fasta kabla hajanyakuliwa na timu nyingine...Sasa presha iko juu ya Van Gaal kwani mashabiki bado hawajaisoma style yake na pia Manchester hawajashinda mechi kama 5 kwahiyo kazi anayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA MECHI YA ZA LEO (GMT)

CHAMPIONSHIP: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

Friday, 18 December 2015

NBA: LeBRON JAMES AMUUMIZA MKE WA JASON DAY



Katika hali ya kawaida ya kuokoa mpira usitoke nje ya court, LeBron James, alifanikiwa kuokoa mpira lakini shida ni kwamba alimwangukia mke wa Jason Day na kumuumiza...Jason Day ni Professional Golfer huko Marekani na alikuwa amekaa pembeni yake wakiangalia game wakiwa court side...


Mke wa Jason anaitwa Ellie Day aliwekwa kwenye machela na kukimbizwa hospitali haraka...Ilikuwa game kati ya Cleveland Cavaliers na Oklahoma Thunder...Kwa sasa Ellie Day anaendelea vizuri...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHELSEA: MAONGEZI NA GUUS HIDDINK YANAENDELEA


Kocha wa zamani ya Uholanzi, Guus Hiddink, yuko tayari kuingia Chelsea muda si mrefu...Hiddink yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa Chelsea na muda wowote wanaweeza kumtangaza kwenye vyombo vya habari...Hiddink amewahi kuwa boss wa Chelsea mwaka 2009 walivyo shinda FA Cup...Hiddink ana rekodi nzuri ya ukocha, kwa mfano, akiwa na PSV Eindhoven alishinda kombe la Dutch mara 6 na European Cup...Bofya hapa upate habari zaidi.

FIFA CLUB WORLD CUP: BARCA NDANI YA FAINALI



Hat-trick ya Luis Suarez imewaingiza Barcelona ndani ya fainali ya Fifa Club World Cup...Barca waliwachapa Guangzhou Evergrande 3-0 bina Neymar na Messi ndani...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 17 December 2015

BREAKING NEWS: JOSE MOURINHO ATIMULIWA


Habari moto moto zilizoingia hapa Max Sports ninasema Jose Mourinho ametimuliwa Chelsea...Chelsea wako hatiani kushuka daraja na mwenye timu Roman Abramovich kashindwa kuvumilia na kumtimua Jose Mourinho...The Special one mwanzo wa msimu aligombana na doctor wa Chelsea, Eva Carneiro, na hatimaye huyo doctor kuondoka baada ya hapo timu imefungwa mara 9 na sasa iko point 1 juu ya relegation stage...Bofya hapa upate habari hii moto kabisa

VODACOM PREMIER LEAGUE: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Pos Club P W D L GF GA GD PTS
1 Young Africans SC 11 8 3 0 23 5 18 27
2 Azam FC 10 8 2 0 22 7 15 26
3 Mtibwa Sugar FC 10 7 2 1 14 6 8 23
4 Simba SC 10 7 1 2 17 7 10 22
5 Stand United 11 6 1 4 11 6 5 19
6 Mwadui FC 11 5 3 3 13 10 3 18
7 Tanzania Prisons 11 5 2 4 11 14 -3 17
8 Toto African 11 4 4 3 10 13 -3 16
9 JKT Mgambo 11 3 3 5 6 9 -3 12
10 Majimaji FC 11 3 2 6 7 19 -12 11
11 Mbeya City Council FC 11 2 4 5 10 11 -1 10
12 Ndanda FC 10 1 6 3 7 9 -2 9
13 Coastal Union SC 11 1 5 5 3 9 -6 8
14 JKT Ruvu Stars 11 2 2 7 10 17 -7 8
15 Kagera Sugar FC 11 1 3 7 3 14 -11 6
16 African Sports 11 1 1 9 2 13 -11 4