Tuesday 29 December 2015

HARLEM GLOBTROTTERS: LEGEND MEADOWLARK LEMON AFARIKI DUNIA



Kama wewe ni mdau wa basketball utakuwa umewahi kuwasikia Harlem Globetrotters...Harlem Globetrotters ni timu ya basketball ambayo ina kipaji cha juu sana na wanakitumia hicho kipaji kufurahisha wapenzi wa basketball na watoto duniani...


Katika timu huyo Meadowlark Lemon alikuwa mmoja kati ya wakali wa timu hiyo miaka mingi iliyopita...Lemon alitaka kucheza basketball ya burudani toka alipokuwa anamiaka 11 alipoona timu ya watu wenye asili ya Africa kwenye tv...

Globetrotters ilianzishwa mwaka 1920 na Lemon ni kati ya jezi 5 tu zilizostaafu...


Wadau wengi sana wameenda kwenye mitandao ya jamii kumkumbuka Lemon akiwemo Shaq na Isiah Thomas...Meadowllark Lemon alikuwa anamiaka 83 alipofariki...Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Meadowlark Lemon...Bofya hapa upate bahari zaidi. 

No comments:

Post a Comment