Tuesday 1 December 2015

NBA: MKALI WA BASKETBALL KOBE BRYANT KUSTAAFU MWISHO WA MSIMU


Kobe Bryant ambae ni "legend" au mkali wa mpira wa kikapu ameamua kuachia ngazi na kupumzika mwisho wa msimu...Kobe Bryant amekaa LA Lakers toka aingie NBA miaka 20 iliyopita na ameisaidia Lakers kushinda ubingwa mara 5...Kobe amesema aliamua kustaafu muda na kwamba kichwa chake kiko poa na pia moyo wake uko poa ila mwili umekataa ndio maana anastaafu mwisho wa msimu...




Katika wachezaji ambao wamewahi kucheza NBA Kobe ni mmoja ambae amefanikiwa kwa hali ya juu sana na mashabiki watamkumbuka daima...Kobe amewahi kufunga points 81 na kwenye NBA ni wa pili katika historia ya mchezo huo pia amechaguliwa kwenye All-Star mara 17...Pamoja na yote ana points zaid iya 32,000 na rings 5...Kwa ufupi Kobe Bryant ni mchezaji bora wa kizazi kipya maana hakuna aliyeweza kumfikia kwa yote aliyeweza kufanya...Bofya hapa upate habari zaidi.

 

No comments:

Post a Comment