Slam Dunk kama inavyofahamika ni wakati mchezaji wa basketball anapofunga anaruka na kushika rim kwa mikono yote miwili au mkono mmoja...Dunk's zimetokea mbali sana hasa wakati American Basketball Association ilipofanya mashindano ya kwanza 1976...
Wakati huo masupastaa wa mchezo huo ndio walikuwa wanashiriki lakini sikuhizi madogo ndio wanatiliwa mkazo washiriki mashindano haya...1984 mashindano ya Slam Dunk chini ya udhamini ya Sprite yalianzishwa kwenye NBA All-Stars na mpaka leo yanaendelea vizuri kusisimua mashabiki wa mchezo wa Basketball...
Bingwa wa mwaka jana ni Terrence Ross ambaye dunk moja kali la mkono mmoja lilimtoa bingwa wa zamani Jeremy Evans...Tusibiri All-Star ya mwaka huu tujue nani atakuwa bingwa...
OKC iliionyesha Miami Heat kwamba wako fiti na sio timu ya madogo wakuchezewa...OKC walikuwa chini 22-4 mwanzo wa game na kumaliza na uchindi wa 112-95...Sasa Kevin Durant amefikia rekodi ya Tracy Mcgrady ya kufunga zaidi ya point 30 kwenye games 12 mfululizo...Bofya upate habari zaidi...
Manchester City jana iliikimbiza Tottenham na kuibuka na mabao 5-1...Aguero akifungua mlango mnamo dakika ya 15... Aguero kati ya mechi 8 kila mechi amefunga bao...Yaya Toure naye alipata bao kwa njia ya penalty wakati beki Danny Rose alipotolewa kwa kadi nyekundu na wachezaji kumlalamikia refa sana...Dzeko nae alipata goli na Jovetic ambaye aliingia baada ya Aguero alipata bao lakini aliumia Hamstring na anaweza kukosa mechi yake dhidi ya Chelsea jumatatu... Bofya hapa upate habari zaidi
Bingwa wa dunia Sebastian Vettel amepata wakati mgumu wakati yeye na timu yake ya RedBull wakijaribu gari lao vipya kwenye pre-testing huko Jerez Spain...Vettel aliweza kumaliza mizunguko 11 (11 laps) tu kwa siku mbili...Gari yake inamatatizo hasa kwenye system ya energy-recovery...Ameweza kumaliza kwa mwendo mdogo kuliko wote..Mabadiliko makubwa kwenye sheria mpya ya F1 itasumbua kidogo lakini ndio mambo mapya hayo...Pata habari zaidi hapa...
Habari ambazo sio nzuri zimekuja kutoka Monaco kwamba Radamel “El Tigre” Falcao hatoweza kucheza World Cup kwasababu juraha alipopata wakati akicheza mpira...Falcao amechana ACL na itachukua zaidi ya miezi mitano kupona vizui...World Cup bado miezi mitano tu...
Colombia ndio wamepata pigo kubwa sana kwani Falcao ni mchezaji wa kutegemewa sana huko kwao...Falcao amesema bado anataka kucheza World Cup na atajitahidi apone haraka...Max Sports inamtakia matibabu mema na ya haraka...Bofya hapa upate habari zaidi...
Jana usiku Liverpool iliichabanga Everton katika derby ambayo dakika 35 tu Everton ilikuwa imechapwa mabao 3 na kushangaa tu...Steve Gerrard akifunga goli la kichwa na Daniel Sturrige akipata mabao mawili baada ya dakika tatu tu na badae Suarez akamalizia la nne dakika ya 50...Machungu ya Everton yalizidi baada ya Romelu Lukaku kutolewa akiwa na maumivu makali baada ya kuumizwa na Gareth Barry...Liverpool wanasherekea ushindi mkubwa wa derby toka 1982...Bofya hapa upate habari za derby.....
Scott Stallings kutoka Marekani ameshinda mashindano ya Farmers Insurance Open katika viwanja vya Torrey ines huko California Marekani...Scott alipata 'birdie' katika shimo la 18 ambalo ndio la mwisho na kuchukua kombe kwa stroke moja...Watu watano wameshika nafasi ya pili ambao ni Pat Perez kutoka Marekani, KJ Choi kutoka South Korea, Graham DeLaet kutoka Canada, Jason Day na Marc Leishman kutoka Australia...
Formula One pre-season testing inaanza wiki hii huko Jerez Spain...Itakuwa siku nne za kutest magari yao ambayo pia wamebadilika kutokana na rules mpya za F1 kuhusu design ya gari...Timu zote zitatumia magari yao mapya mpaka sasa Ferrari, Force India, McLaren, Sauber na Lutus wameonyesha magayi yao mapya Toro Rosso wataonyesha gari lao jumatatu na Mabingwa Redbull na Mercedes wataonyesha gari lao jumanne...
Msimu huu utakuwa mgumu kidogo kwasababu wameruhuru tena Turbo kutumika...Turbo haijatumiwa toka 1988 pia kutakuwa na Hybrid technology (energy recovery)...Ingia hapa upate habari za F1...
Kevin Durant aliwaokoa Oklahoma City mwishoni kwa kufunga wakati zimebakia sekunde 1 nukta 5 kwenye clock wakiwafunga Atlanta Hawks 111-109...Durant alimaliza game ana pointi 41...half time ilivyofika OKC walikuwa chini pointi 14...Durant sasa kati ya mechi 11 anafunga zaidi ya pointi 30 kwa game hii haijatokea toka March na April 2003 wakati Tracy McGady alipoweza kucheza mechi 14 na zote kupata pointi zaidi ya 30...Kevin Durant akishangilia bao hapo juu (pichani) akiwa na mtanzania Hasheem Thabit anayechezea OKC...Bofya hapa upate habari zaidi...
Bingwa wa michuano ya Australian Open kutoka Uswiss Stanislas Wawrinka mwenye umri wa miaka 28 amekiri kuwa hakutegemea kushinda fainali dhidi ya bingwa wa dunia Rafael Nadal...Mafurahi kuwa namba tatu duniani na kumfunga bingwa wa dunia na anakuwa mchezaji wa kwanza kumfunga mmoja wa 'the big four' toka Del Potro 2009...
Nigeria imeingia nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika huko Afrika ya kusini...Zimbabwe pia imeingia nusu fainali...Nigeria ilitoka 3 bila kabla ya half time na Ejike Uzoenyi alisawazisha dakika ya 90 na baada ya hapo Aliyu Ibrahim alipachika bao la ushindi zikiwa zimebakia dakika 9 za nyongeza... Zim nao ilikuwa ngumu sana lakini waliichapa Mali 2-1...
Dar es Salaam Young Africans wameanza vizuri mzunguko wa pili wa ligi kwa kuwacgapa wauza mitumba Ashanti 2-1 uwanja wa taifa...Yanga ilipata wakati mgumu kigodo lakini ilichomoa na kushinda mwishoni...Yanga bado inaongoza ligi na pointi 31 ikifuatiwa na Azam point 30...Pia timu zingine kubwa ziliweza kufanya vizuri kama Azam iliichapa Mtibwa bao 1 kwa 0 na Mbeya City pia iliibuka na ushindi dhidi ya Kagera Sugar bao 1 kwa 0...
Mabingwa watetezi Dar es Salaam Young Africans (Yanga) leo inaingia uwanjani na wauza mitumba au kwa jina lingine Ashanti...Yanga walitoka safarini Uturuki ambapo iliweka kambi kwa wiki 2 na kujifua ili wawe fiti kwa round nyingine ya ligi...Max Sports inawatakia timu zote mbili heri na pia mashabiki wote nendeni mkashangilie timu hizo...
Arsenal jana usiku iliigonga Coventry City mabao 4 kwa 0 na kuingia round ya 5...Lukas Podolski alichapa 2 ambalo bao moja alipewa pande na Mesut Ozil...Giroud alichapa goli mnamo dakika ya 84 kwa shuti la mbali kidogo na badake kidogo Santi Carzola alichapa bao kama hilo la Giroud...Covenrty City kipindi cha pili hawakuwa vilaza walikimbiza mpira na kugonga mwamba lakini bado Arsenal walikuwa juu ya kiwango...
Kilicho furahisha washabiki wa Arsenal jana usiku ni kuingizwa kwa dogo mmoja machachari sana ambaye anacheza midfield Gedion Zelalm...Huyu dogo anamiaka 16 na yuko timu ya vijana ya Ujerumani na pia anatokea Ethiopia...Bofya hapa upate habari na stats za game hii...
Rafael Nadal ameingia fainali ya michuano mikubwa ya tennis ya Australian Open huko Melbourne Australia...Rafa ameonyesha kwamba yeye ni mkali kwa kumchapa Roger Federer set zote mfululizo 7-6 (4), 6-3, 6-3...Sasa atakutana na namba 8 duniani Stan Warwinka...Federer amechapwa na Rafa mara 23 kati ya 33 kati ya mikutano yao...Rafa ndio anatarajiwa kuutwa ubingwa wa Australian Open...Tusubiri kama itawezekana...
McLaren timu ya mashindano ya magari ya F1 imekuwa timu ya kwanza kuzindua gari lao jipya la msimu ambao utaanza muda si mrefu...Gari hilo limepewa jina la MP4-29...
Habari hizi ni njema lakini zilizidiwa na habari kwamba McLaren wamemuiba mtaalam kutoka timu ya Lotus...McLaren hawajafanya vizuri kwa muda sasa mpaka boss wao Martin Whitmarsh ilibidi aachie ngazi...Soma zaidi hapa kuhusu timu ya Mclaren...
Rafael Nadal leo atapambana na Roger Federer kwenye nusu fainali ya michuano mikali ya tennis huko Australia...Roger amechapwa sana na Nadal na sasa ananafasi ya kurudisha kichapo... bofya hapa ufuatilie live feeds za mechi hiyo...
Ahmed 'Mido' Hossam ametajwa kuwa ni kocha mpya wa timu kubwa ya Zamakel huko Egypt...Mido alikuwa mchezaji wa Tottenham na pia stiker wa timu ya Egypt...Inasemekana sasa ni kocha mdogo kuliko wote katika historia ya ulimwengu wa soka Egypt...Watu wanasema eti wewe ni mdogo lakini yeyey anasema yuko tayari kwa jukumu hilo...Zamalek ni timu kubwa sana Egypt na Afrika wamewahi kuchukua kombe mara 11 huko Egypt na mara 5 African Chapions...Bofya upate habari zaidi za striker Mido...
Mohamed Salah, miaka 21, kutoka mabingwa wa uswiss Basel ataelekea Chelsea muda si mrefu...Salah anatokea Egypt na nafasi yake uwanjani ni midfielder bado haja pewa uangalizi wa daktari ili apewe go ahead...Chelsea wanamchukua kwa pond za Uingereza milioni 11...Bofya hapa upate habari zaidi...
Chelsea wamekubali kumwachia Mata.. dau lake ni pound za Uingereza milioni 32 rekodi kwa Manchester United...Mara ya mwisho Man wamelipa bei kubwa ilikuwa wakari wamemchukua Berbatov kwa pond za uingereza milioni 30.75...Mata inasemekana alikuwa ana issue na kocha Jose na alikuwa hapangwi sana na anaingia kama sub mechi nyingi...Labda Mata atawasaidia Man wakati huu wakiwa wanapata shida ya kushinda mara kwa mara...
Striker mkali sana kutoka Colombia Radamel Falcao aliumia vibaya sana kwenye mechi ya kombe la Ufaransa akichezea timu ya Monaco...Mnamo dakika ya 40 jamaa wa timu pinzani, Soner Ertek, alimvaa Falcao na kumuumiza goti la kushoto...Bado haijajulikana kwa kiwangogani ameumia Falcao na pia iko hofu anaweza asicheze World Cup huko Brazil mwaka huu...Falcao alinunuliwa kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha milioni 60 euros...
British namba 1 Andy Murry jana aliaga mashindano ya Australian Open kwa kuchapwa set nne 6-3 6-4 6-7 (8-6) 6-3 na Roger Federer...Andy hakuwa na uwezo jana ingawa ameshamchapa sana Federer michuano ya nyuma lakini jana alishindwa vibaya sana...Andy alishindwa ku 'break' set mbili za mwanzo pia alipata wakati mgumu kutokana na 'serve' ya Federer kuwa kali sana...Bofya hapa upate habari zaidi...
Michuano ya tennis inaendelea kusisimua mashabiki huko Melbourne Australia na sasa Andy Murry atakutana na Roger Federer kwenye robo fainali leo...Roger Federer ambaye alichapa vibaya sana Jo-Wilfred Tsonga kwa straight sets na kuonesha dunia kwamba yuko fiti sana kama miaka ya nyuma na sasa kambi ya Andy Murry inabidi wajipange sana kwa game ya leo...
Andy na Roger wamekutana mara 20 na kati ya mikutano yao Andy ndio mshindi mara 11 kwa 9...Usikose kuangalia mchuano huu leo...Bofya hapa usome zaidi...
Timu ya Jamaica ya kuteleza kwenye barafu (Bobsleigh) imepata nafasi ya kuingia kwenye Winter Olympics huko Sochi Urusi....Jamaica kwa maraya ya kwanza waliweza kupata nafasi ya kushindana mwaka 1988 huko Calgary Canada mpaka badae ikatengenezwa filamu kuhusu hiyo timu ambayo ilitolewa na kampuni ya Disney na iliitwa 'Cool Runnings'....Mara ya mwisho kupata nafasi ilikuwa Olympics huko Salt Lake City Marekani mwaka 2002...Bofya upate habari zaidi..
David Moyez na timu yake ya Manchester United jana ilichabangwa mabao 3-1 na Chelsea ambapo mabao yote ya Chelsea yalitoka kwa Samuel Eto'o...Manchester United ilionekana inakiwango cha chini kabisa na Chelsea alikuwa hatari na makini kipindi chote...Goli la kwanza la Eto'o lilikuwa vuri sana...Mabeki wa Manchester United walionekana kujisahau nyuma na kutokuwa makini kukaba...Dogo mmoja tu wa Manchester United Adnan Januzaj ndio ameonesha ujuzi wa hali ya juu lakini peke yake hawezi kuibadilisha timu...Inabida Rooney na Van Persie warudi tu na wazee wote watolewe kabisa...Sasa United wamepoteza mechi 7 kati ya mechi 22...Mechi hiyo imeona kocha wa Chelsea Jose kupata magoli 100...Bofya upate habari zaidi...
Maria Sharapova ambaye ni namba tatu duniani ameaga mashindano ya tennis ya Australian Open huko Melbourne Australia...Sharapova alishapwa na Dominika Cibulkova (namba 20 duniani) kwenye round ya nne ya mashindano hayo 3-6 6-4 6-1 na kushangaza dunia...Sharapova aliwahi kushinda hayo mashindano mwaka 2008..Bofya hapa upate mambo...
Denver Broncos ikiongozwa na Payton Manning imeichapa New England Patriots 26-16 katika fainali za AFC...Manning sasa ananafasi ya kushinda tena ubingwa mara ya pili wakikutana na Seattle Seahawks kwenye fainali ya Super Bowl XLVIII...Seattle imeichapa 49ers...Payton Manning alikuwa anaumwa kwa muda na alifanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mishipa ya fahamu lakini sasa amejitahidi na kuingia fainali...
Simba Sports Club au wana wa Msimbazi jana walichapwa kihalali na Mtibwa Sugar bao moja kwa mtungi kwenye mechi ya kirafiki katika uwanja wa Taifa jana...
Mark Selby atakutana na Ronnie O'Sullivan kwenye fainali ya michuano ya masters au mabingwa wa mabingwa wa mchezo wa snooker...Mark Selby ambaye ni namba mbili duniani alimchapa Shaun Murphy 6-1nakuingia fainali...Pia Ronnie alimchapa kirahisi Stephen Maguire 6-2...Mechi yao ya fainali itachezwa leo jioni...Bofya upate habari za fainali ya snooker...
Manchester City imepita magoli 100 baada ya kumchapa Cardiff City mabao manne kwa mawili...mchezo ulikuwa mkali kwasababu Cardiff walivimbisha kifua na kufanya Man City kupata wakati mgumu kidogo...Bao la Dzeko ndio liliwafikisha kwenye magoli mia ambapo kati wa mechi 34 tu za mashindano wameweza kupata mabao mengi kiasi hicho...Haijawahi kutokea toka Premiership ianzishwe...Dzeko pia ni mchezaji wa kwanza kupewa goli kutokana na technolojia ya golini (Goal line technology) ambapo waamuzi wanaamua utata kama goli limeingia au la...Bofya hapa upate habari zaidi...
Arsenal bado yashikilia uskani baada ya kumchapa Fulham mabao mawili kwa mtungi....Mechi iliyomalizika muda si mrefu iliona mabao yakitoka kwa Santi Carzola dakika ya 57 na ya 62...Arsenal sasa imeshinda mechi tano mfululizo na kubakia kileleni kwa sasa...Bofya hapa upate mambo zaidi...
Simba au kwa jina jipya Mtani Jembe anaingia uwanjani na Mtibwa Sugar kwenye mechi ya kirafiki ili kujiweka sawa kabla ya ligi kuu...Kiingilio ni kuanzai buku 5 viti vya orange na blue, VIP C 7,000, VIP B 10,000 na VIP A 20,000...Simba inaingia kucheza ikiwa imetoka kwenye mashindano ya mapinduzi ambapo ilitoka mshindi wa pili...
Serena Williams kutoka marekani ameweka rekodi nyingine kwenye ulimwengu wa tennis kwa kuwa mwanamke ambaye ameshinda mechi nyingi duniani kwenye michano ya Australian Open...Sasa Serena ameshinda mechi 61 baada ya kumtwanga Daniela Hantuchova 6-3 6-3...Pamoja na joto kali ambalo liko huko Melbourne Australia Serena alichukua takriban saa moja na dakika ishirini kumchapa Daniela ambaye ni No. 31 duniani...Bofya hapa upate habari zaidi kutoka Melbourne Park...
Ron Dennis arejea tena McLaren kuiongoza timu hiyo kama C.E.O....Ron aliondoka McLaren mwaka 2009 na kumwachia Martin Whitmarsh lakini baada ya hiyo timu kutofanya vizuri na kukosa ushindi kwa miaka mitano sasa Ron amerejea kuweka mambo sawa...Ron alikaa McLaren miaka 27 lakini badae kulitokea scandal ya kudanganya ndio ikabidi aachie ngazi na kusaidia kutengeneza magari ya commercial sports na pia kubakia kama Chairman ambapo sasa pia ni Chairman na C.E.O...Mabadiliko haya yamekuja kabla ya pre-testing huko Jerez, Spain na mashindano ambayo yanaanza Melbourne, Australia Machi 16...
Man City jana iliendelea kukusanya magoli baada ya kuichapa Blackburn Rovers mabao 5 kwa mtungi kwenye mechi ya FA ambayo sasa inaiona Man City ikiingia roundi ya 4 sasa...Mabao yalitoka kwa Negredo ambaye alipachika mawili pia Dzeko nae alipachika mawili na Aguero alipachika moja...Sergio ndio amerudi baada ya kuumia...Bofya hapa kwa habari zaidi...
Michezo ya Tennis ilisimamishwa jana kutokana na jua kali sana huko Melbourne Australia...Joto lilkizidi sana na kufikia Celsius 42.2 na kulazimisha waandaaji wa michezo hiyo kusimamisha mechi zote kwenye courts ambazo ziko wazi mpaka joto lipungue...Mdada mmoja ambaye ni mchezaji mkali sana Alize Cornet alibaki analia baada ya kupumzika kati ya mechi yake dhidi ya Camila Giorgi...Mchezaji mwingine Frank Dancevic kutoka Canada alizimia juzi na kupatiwa huduma ya kwanza...
Stephane Peterhansel akichanja mbuga huko pwani ya Chile karibu anamfikia Nani Roma kwenye stage ya 11 ya mashindano hayo...Sasa wanapishana dakika mbili tu na baada ya siku moja tu alipunguza dakika 11 na sasa zimebakia kilometa 1,100 tu mashindano hayo yaishe...Bingwa wa 2010 Carlos Sainz aliaga hayo mashindano kwa kupata ajali..
Andy Murry (No. 4 Duniani) akicheza tennis kwenye joto kali alichukua dakika 87 tu kumchapa Go Soeda kutoka Japan 6-1 6-1 6-3...Murry sasa ameingia round ya pili ya michuano hiyo mikali huko Melbourne Ausralia...Mechi ijayo sasa atacheza na mfaransa Vincent Millot kwenye round ya pili...Murry ana kazi kwasababu lazima akutane na wakali wote wanne wa tennis na awachape ili aweze kushinda huko Melbourne...Pata habari zaidi hapa...
Cristiano Ronaldo jana usiku alishida tuzo ya FIFA ya Ballon d'Or mwanasoka bora duniani...Ronaldo alimshinda Lionel Messi na Frank Ribery na kuchukua heshima hiyo...Mara ya mwisho Ronaldo kushinda hiyo tuzo ilikuwa 2008 wakati Messi alishinda mara nne mfululizo kabla ya mwaka huu...Ronaldo aliwashukuru wachezaji wa timu yake na timu ya taifa...Mwaka jana Ronaldo alifunga mabao 66 kati ya mechi 56 akichezea club yake na timu ya taifa...
Ballon d'Or:
Cristiano Ronaldo
Women's world player:
Nadine Angerer
Male coach:
Jupp Heynckes
Female coach:
Silvia Neid
Ballon d'Or Prix d'Honneur:
Pele
Puskas goal award:
Zlatan Ibrahimovic (Sweden v England)
Roy Jones Jr. amesema Amir Khan ni boxer mzuri na akizichapa na Mayweather atamsumbua kwasababu anaweza kutoka kwenye situation nzito na kubox vizuri...Kama wakikutana May 3 Jones anaona Khana atafanya pambano liwe la kusisimua kutokana na style ya Khan ya kuzichapa na pia urefu utamsaidia...Lakini pia alisema Mayweather ni mzuri zaidi na ananguvu zaidi...
Tatizo moja Jones Jr anasahau ni kwamba Khan ni mbishi na ni kazi kumruddisha katika form yake ya kubox ya awali...Khan kafulia kiaina sasa na anabahati kupambana na bingwa...Welterweight contender Kell Brook kutoka Uingereza pia anasema Khana hana chance ya kushinda dhidi ya bingwa wa dunia Floyd Mayweather...Acha tu tusubiri pambano hilo...