Wednesday 4 February 2015

FA CUP: MANCHESTER UNITED NDANI YA ROUND YA 5


Manchester United imefanikiwa kuingia round ya 5 ya michuano ya FA Cup baada ya kuichapa Cambridge United 3-0.


United watakutana na Preston North End kwenye round ya 5 ya michuano hiyo muhimu katika ratiba soka la Uingereza.

Man United walikoswa dakika ya 1 baada ya mpira kugonga mwamba na badae Juan Mata ndie alifungulia magoli dakika ya 25 baada ya kupachika mpira kwa karibu na baae kidogo Marcos Rojo alipachika bao la kichwa dakika ya 32.


Kipindi cha 2 dakika ya 73 James Wilson alimalizia kwa bao kwenye 18.

Tarehe 26 February watasafiri kwenda kucheza na Preston huko Deepdale na hizi timu 2 hazijakutana toka 1972...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment