Thursday 5 February 2015

AFCON 2015: IVORY COAST YAINGIA FAINALI


Ivory Coast imefanikiwa kuingia fainali ya michuano mikubwa sana Afrika ya Afcon kwa mara ya 3 sasa baada ya kuichapa timu ya DR Congo 3-1...Yaya Toure alianza kufungulia mabao baada ya kupachika bao la mbali la yadi 20 lakini baada ya muda mfupi Congo walisawazisha kupitia Dieumerci Mbokani dakika ya 24...


Wengine waliofunga ni Gervinho dakika ya 41 na Wilfred Kanon dakika ya 68...Ivory Coast walicheza mpira safi sana na Congo walikuwa wamezidiwa kidogo pia Gervinho alikuwa kinara wa kuwasumbua Congo na alikosa nasasi kibao a kupachika magoli...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment