Friday, 6 February 2015

AFCON 2015: FUJO ZA MASHABIKI ZATANDA NUSU FAINALI


Mechi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea huko Malabo ilisimamishwa kwa takriban dakika 30 kutokana na fujo kutoka kwa mashabiki wa Equatorial Guinea na kulazimu polisi waingilie kati kutuliza ghasia...

Ilikuwa patashika kwani mashabiki wa Ghana ilibidi wajichimbie kutokana na vitu na vyupa ambavyo walikuwa wanarushiwa...


Ghana ilimaliza mchezo na ushindi wa mabao 3-0 na bao la kwanza alipachika Jordan Ayew baada ya Kwesi Appiah kufanyiwa foul na kipa Felipe Ovono...Bao la 2 lilitokana na counter attack na Mubarak Wakaso hakufanya kosa...


Mwishoni mwa kipindi cha 2 fujo zilishaanza na Ghana ilibidi watolewe nje na kikosi chakuzuia fujo....Bao la 3 kutoka kwa Andre Ayew dakika ya 75 ndio mambo yakaharibika kabisa na mashabiki wa Ghana ilibidi wajifiche kwenye goli...


Tabia hizi za kipumbavu sana zinaharibu sifa ya mpira wa Afrika na zinaleta sura mbaya duniani na inabidi zikemewe sana...Tusubiri tamko la Caf kuhusu vurugu hizi...Ghana watacheza fainali na Ivory Coast...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment