Tuesday 31 March 2015

COLOMBIA: RADAMEL FALCAO AFIKIA REKODI YA MAGOLI


Striker ambae ametoka Monaco na sasa yuko Manchester United kwa mkopo, Radamel Falcao, amefikia rekodi ya mabao katika timu ya taifa ya Colombia...Falcao amefikia rekodi ya Arnoldo Iguaran ya mabao 24...


Falcao mkataba wake wa pounds 265,000 kwa wiki unaisha mwisho wa msimu huu na Mnchester wakikubali kumshikilia inabidi watoe ounds milioni 43.5...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 30 March 2015

BOXING: KELL BROOK ABAKIA NA MKANDA WA IBF WELTERWEIGHT


Kell Brook amtwanga Jo Jo Dan ndani ya round ya 4 n kubakina na mkanda wa IBF Welterweight...Kell Brook alionekana yuko fit na anakiu ya ushindi ndani ya Motorpoint Arena huko Sheffield kabla ya taulo kurushwa ndani kusimamisha pambano hilo round ya 4...Brook alipanda taratibu kenye ngazi za boxing na sasa ni boxer mwenye ushindi wa mechi 34 na alijulikana duniani mwaka jana mwezi wa 8 aliposhinda pambano lake dhidi ya Shawn Porter huko Carson California...Brook sasa anamtaka Amir Khan katika bambano lake lijalo...Bofya hapa upate habari zaidi.

WORLD CROSS COUNTRY CHAMPIONSHIP: GEOFFREY KIPSANG BINGWA MASHINDANO YA 41 HUKO CHINA


Geoffrey Kipsang ameshinda mbio kali za Cross Country huko Guiyang China...Mkenya Bedan Karoki Muchiri aliibuka mshindi wa 2 na Muktr Edris alichukua nafasi ya 3...Kipsang ambae alitumia dakika 34 na sekunde 52 alisaidiwa kutokana na mkakati wa kusaidiana kitimu na wenzake...Bofya haa upate bahari zaidi.

MIAMI OPEN: VERDASCO AMTOA RAFA


Namba 2 duniani Rafael Nadal ametolewa kwenye mashindano ya Miami Open na mspanish mwenzake Fernando Verdasco....Nadal ambae hajawahi kuchukua kombe hilo huko Miami alichapwa 6-4 2-6 6-3 bila ubishi...Rafa alijaribu kurudi vizuri set ya 2 lakini alivunywa mara 3...Sehemu nyingine Any Murray nae alianikiwa kushinda mechi yake dhidi ya Santiago Giraldo 6-3 6-4...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 29 March 2015

CRICKET WORLD CUP: AUSTRALIA MABINGWA WA DUNIA


Australia imenyakua ubingwa wa dunia wa Cricket baada ya kuichapa New Zealand...Mambo yalimalizika New Zealand wakiwa na 183 na Australia 186-3...Kombe lilikabithiwa Captain wa timu ya Australia Michael Clarke mbele ya umati wa watu zaidi ya 93,000 kwa shangwe na makofi mengi sana na baada ya kupewa kombe alienda timu yake iliposimama na kunynyua kombe juu...


Man of the match alichukua James Faulkner...Hii ni mara ta 4 Australia wamechukua ndani ya miaka 5...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: FERRARI WASHINDA MALAYSIA GP


Dereva mpya wa Ferrari Sebastian Vettel ameshinda Malaysian Grand Prix...Ferrari kwa miaka mingi walikuwa wanasuasua na sasa wamepata dereva ambae anaweza kuchuana na timu ya Mercedes...Lewis Hamilton ameibuka mshindi wa 2 ingawa alianza wa kwanza kwenye Grid...Hamilton na timu yake ya Mercedes walipitwa kutokana na mkakati wa matairi waliyochagua...


Nico Rosberg aliibuka mshindi wa 3 mbele ya Kimi Raikkonen nae yuko team Ferrari...Msimu huu Mercedes watapata upinzani mkubwa kutoka kwa Ferrari...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 28 March 2015

TETESI: MAN U WAKO TAYARI KUTOA MILIONI 80 KUMNYAKUA RONALDO


Manchester United wako tayari kutoa dau la milioni 80 pounds kumnyakua Cristiano Ronaldo lakini bado mapema kujua mambo yatavyoenda...


Sehumu nyingine Jose Morinho yuko tayari kumchukua mchezaji wa Valencia na kiungo mshambuliaji wa Portugal Andre Gomes mwenye umri wa miaka 21 na mwenye dau la milioni 36 pounds...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday 27 March 2015

EPL: JOHN TERRY AONGEZA MKATABA DARAJANI


John Terry ataendelea kukaa darajani mpaka msimu 2015-2016...Jose Mourinho amesema mkataba mpya sio kwamba wanamshukuru Terry lakini Terry ni mchezaji mzuri na ni beki makini sana...Terry toka aingie darajani 1998 ameshinda vikombe 13 vikiwemo Champions Legue, Europa League, Premier League mara 3, FA Cup 5 n League Cup 3...Bofya hapa upate habari zaidi.

INTERNATIONAL FRIENDLIES: MATOKEO YA MECHI ZA JANA NA JUZI

THU 26 MAR 2015 - INTERNATIONAL FRIENDLIES
WED 25 MAR 2015 - INTERNATIONAL FRIENDLIES

INTERNATIONAL FRIENDLIES: BRAZIL BEATS FRANCE 3-1


Brazil came from behind to beat France 3-1.

Thursday 26 March 2015

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA YAZIDI KUSONGA MBELE


Simon Msuva apachika mabao 2 akisaidiwa na Danny Mrwanda bao la 3 mabao ambayo yamewasogeza Yanga pointi 4 mbele ya timu zingine...Yanga walishinda 3-1 dhidi ya Ruvu JKT jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam...


Yanga sasa wana points 40 katika mechi 19 wakifuatiwa na Azam points 36 na Simba points 32...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZIJAZO

SAT 4 APR 2015 - PREMIER LEAGUE
  • ArsenalvLiverpool12:45
  • EvertonvSouthampton15:00
  • LeicestervWest Ham15:00
  • Man UtdvAston Villa15:00
  • SwanseavHull15:00
  • West BromvQPR15:00
  • ChelseavStoke17:30

Wednesday 25 March 2015

BOXING: KELL BROOK ANATAKA KUZICHAPA NA MAYWEATHER AU PAC-MAN NA SIO KHAN


Kell Brook amesema hana mpango wa kuzichapa na Amir Khan na anasubiri kuzichapa na Mayweather au Manny Paquiao baada ya mechi yao ya May 2...Brook Jumamosi ijayo anategemea kutetea mkanda wa IBF welterweight...Bofya haa upate habari zaidi.

Tuesday 24 March 2015

MX2: ASSAF NATAN NA ALESTAIR BLICK WAONGOZA MASHINDANO YA PIKIPIKI UGANDA


MX2 ni mashindano ya 2 ya pikipiki kwenye barabara ambayo haina lami na inamabone na miinuko mingi kwa jina lingine ni Motor Cross huko Ugada....MX2 inayofanyika huko Uganda inaongozwa na Assaf Natan na Alestair Blick...Round nyingine ya Central African Challenge yatafanyika May 3 mwaka huu...Bofya hapa upaye habari zaidi.

EPL: MARTIN SKRTEL WA LIVERPOOL ASHTKIWA KWA KUMKANYAGA DAVID DE GEA


Martin Skrtel amshtakiwa na FA baada ya kumfanyia rafu mbaya ya kumkanyaga kip awa Manchester United David De Gea...Tukio hilo lilifanyika dakika za majeruhi kwenye mechi ambayo Manchester United walishinda 2-1 ndani ya Anfield...


Mechi hiyo hiyo iliona Steve Gerrard akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kucheza dakika 38 tu...Bofya hapa upate habari zaidi.


TFF: JAMAL MALINZI ATUMA SALAM ZA PONGEZI KWA TWIGA STARS


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ametuma salam za pongezi kwa timu ya Twiga Stars ambayo ni timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake baada ya kuwachapa timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (She-Polopolo) mabao 4-2...Malinzi amesema ushindi huo ni matokeo ya umakini wa maandlizi mazuri chini ya kocha Rogasian Kaijage pamoja na TFF...Timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam kati ya tarehe 10 na 12 na mshindi atafuzu kucheza All Africa Games huko Congo Brazzaville Septemba 3-18 mwaka huu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 23 March 2015

NSSF CUP: JAMBO LEO WAINGIA MITINI BAADA YA KICHAPO CHA 3-0

Jambo Leo wakiingia mitini game...
NSSF wamewachapa Jambo Leo 3-0 mpaka wakaondoka uwanjani eti kisa uwanja mbaya umejaa maji...Sijui hayo maji yalikuja baada ya bao la 3 maana mvua zinazoendelea kunyesha bado hazijaacha jijini Dar es Salaam...Baada ya mwamuzi kutoa dakika 15 akiwasubiri Jambo Leo warudi uwanjani na alivyoona hawarudi aliamua kuwapa NSSF ushindi...Bofya hapa upate habari zaidi.

EL CLASICO: BARCELONA YAILAZA REAL MADRID KWENYE GAME YENYE UPINZANI MKUBWA SANA


Barcelona kupitia Luis Suarez kipindi cha 2 wameifunga Real Madrid na kuendelea kuongoza la liga kwa points 4...


Barcelona walianza vizuri kipindi cha kwanza lakini Real walizinduka na kuanza kushambulia kwa kasi na hatari moja ilitokea wakati Ronaldo akipokea cross ya Karim Benzema lakini hakuwa na nafasi nzuri ya kumalizia na akagonga mwamba...


Suarez mnamo dakika ya 56 akitingisha nyavu na kuwaamsha mashabiki wa Barca kwa bao lake safi kabisa...Bofya haa upate habari zaidi.

BNP PARIBAS OPEN: DJOKOVIC AMCHAPA ROGER FEDERER NA KUCHUKUA UBINGWA INDIAN WELLS


Bingwa wa dunia Novak Djokovic amemchapa bingwa wa zamani Roger Federer 6-3 6-7 (5-7) 6-2 na kunyakua kombe la BNP Paribas Open huko Indian Wells California Marekani...Djokovic alijitahidi set ya kwanza lakini set ya 2 Federer alikomaa na kulazimisha tie-break...Djokovic sasa ameshinda vikombe 50 na ni mara ya 4 anashinda hapo Indian Wells...Bofya hapa upate habari zaidi.

BNP PARIBAS OPEN: SIMONA HALEP BINGWA


Simona Halep amenyakua ubingwa wa tennis katika mashindano ya BNP Paribas Open huko Indian Wells California Marekani...Halep alimchapa Jelena Jankovic katika mechi kali sana ambayo Jankovic alichukua seti ya kwanza na alionekana kucheza vizuri kuliko Halep lakini Halep aligeuza kibao na kumbreak mwenzake mara 4 kwenye set ya 2...Matokeo yalikuwa 2-6 7-5 6-4 ktika mechi hiyo kali ya fainali...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 22 March 2015

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Chelsea283564
No movement2Man City303461
No movement3Arsenal302760
No movement4Man Utd292456
No movement5Liverpool291354
No movement6Southampton302153
No movement7Tottenham30553
Moving up8Swansea30-443
Moving up9West Ham30342
Moving down10Stoke30-342
Moving up11Crystal Palace30-536
Moving down12Newcastle30-1535
No movement13West Brom30-1233
No movement14Everton29-531
No movement15Hull29-1128
No movement16Aston Villa30-2028
No movement17Sunderland30-2126
No movement18Burnley30-2325
No movement19QPR29-2222
No movement20Leicester29-2119