Wednesday 15 April 2015

HILLSBOROUGH DISASTER: LEO NI KUMBUKUMBU YA WALIOPOTEZA MAISHA HILLSBOROUGH


Tarehe 15 April 1989 watu 96 walipoteza maisha uwanja wa Hillsborough mji wa Sheffield kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la FA kati ya Liverpool na Nottingham Forest...


Siku hiyo watu wengi sana walikuja kuangalia mpira na mashabiki wa Liverpool walipewa eneo ambalo halikutosha na badae mkuu wa usalama wa uwanja akafungua mlango mwingine watu wakazidi kujaa na kuanza kukanyagana na watu 96 walipoteza maisha siku hiyo na watu 766 walijeruhiwa...


Mwaka 1990 ulifanyika uchunguzi chini ya usimamizi wa Lord Justice Taylor ambao ulibaini polisi hawakuwa makini na pia hiyo report ilisababisha viwanja vyote kutoa sehemu ya watu kusimama...


Ilikuwa siku ya hizuni sana Uingereza na duniani kwani ilikuwa moja ya ajali mbaya sana kutokea katika uwanja wa mpira...Max Sports na wadau tunaomba dua mola aendelee kuweka roho zao mahali pema peponi....Bofya hapa upate historia ya Hillsborough.


No comments:

Post a Comment