Wednesday 27 May 2015

FIFA: MAKAMU MWENYEKITI WA FIFA NA WENGINE 5 WAKAMATWA


Jeffrey Webb Makamu Mwenyekiti wa Fifa na wengine 5 wamekamatwa na polisi kuhusiana na rushwa na kusafisha pesa haramu...Wamekamatwa wakiwa ndani ya  hoteli ya nyota 5 ya Baur au Lac mjini Zurich, Uswisi wakiwa wanajiandaa na uchaguzi mkuu wa Fifa Ijumaa ijayo...Polisi walivamia hiyo hoteli bila kumshtua mtu na kuwakamata hao maofisa na baada ya hapo wafanyakazi wa hoteli walianza kuchanganyikiwa wakiwa hawajui cha kufanya...

Jeff Webb.
Inasemekana polisi waliombwa na polisi wa Marekani kutokana na uchunguzi wa muda mrefu...Watuhumiwa wanasubiri wasafirishwe kwenda Marekani kujibu mashtaka hayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment