Sunday 17 May 2015

EPL: STEVEN GERRARD AAGWA NA MASHABIKI WA THE KOP


Captain wa Liverpool na Legend kwenye timu ya Liverpool Steven Gerrard ameagwa rasmi kwenye uwanja wa Anfield...Gerrard akiingia uwanjani na watoto wake watatu alishangiliwa sana na mashabiki wa the Kop na kupewa gwaride la heshima na timu zote mbili...


Steve Gerrard ni mchezaji aliyekulia kwenye club miaka 25...Gerrard alisema kweli "You'll never walk alone" akihojiwa na waandishi wa habari huku akishukuru hasa mashabiki wa Kop na uongozi wote wa club ya Liverpool huku akishangiliwa sana na mashabiki wakilitaja jina lake...


Gerrard aliingia Liverpool akiwa na miaka 9 na alifanikiwa kufunga mabao 185 kati ya mechi 709 alizocheza...Gerrard anaondoka Liverpool kwenda kucheza Marekani kwenye timu ya L.A Galaxy...


Gerrard amekuwa Captain toka 2003 nafasi aliyoishikilia kwa miaka 12...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment