Sunday 12 July 2015

WIMBLEDON 2015: SERENA BINGWA


Serena Williams ameshinda michuano mikubwa sana ya tennis duniani ya Wimbedon nchini Uingereza...


Serena ameshinda kwa mara ya 6 na pia ameshinda vikombe vikubwa 4 au kwa jina lingine 'Grand Slam' 4 na sasa wapembuzi wa tennis wanasema 'Serena Slam'.

Serena alimchapa Gabrine Munguruza 6-4 6-4 ndani ya Centre Court.

Mwishoni Munguruza ambaye ni namba 20 duniani alikoma na kujitahidi sana lakini alizidiwa na Serena.

Mechi ilichukua takriban saa 1 na dakika 23...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment