Thursday 16 July 2015

NIGERIA: SUNDAY OLISEH KOCHA MPYA


Shirikisho la Mpira la Nigeria limemchukua Sunday Oliseh kuwa kocha wao mpya...Oliseh anachukua nafasi ya Stephen Keshi aliyefukuzwa hivi karibuni...Oliseh alichezea timu ya Taifa ya Nigeria mara 63 na alisaidia timu hiyo ya Super Eagles kuchukua ubingwa wa Africa mwaka 1994 pamoja na Olympic gold mwaka 1996...


Oliseh amechezea timu kubwa za Ulaya kama Burussia Dortmund, Ajax na Juventus kwa hiyo ataleta uzoefu wake usaidie Super Eagles lakini haita kuwa rahisi kwani kutokana na siasa chafu ndani ya Shirikisho la Soka la Nigeria limeyumbisha sana maendeleo ya timu hiyo ya Taifa...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment