Saturday 18 July 2015

F1: JULES BIANCHI AFARIKI DUNIA


Formula One imepoteza dereva Jules Bianchi miezi 9 toka apate ajali mbaya sana Suzuka Japan...Bianchi alipata ajali mbaya alipogonga n kuingia chini ya gari zito la kutoa magari yaliyopata ajali Suzuka Japan na toka hapo aikuwa kwenye Coma muda wote mpaka mauti yalipomfikia...Amekuwa dereva wa kwanza kufariki ndani ya eneo la Grand Prix toka bingwa wa dunia Aryton Senna alipofariki kutokana na ajali mbaya ambayo aligonga kingo za pembeni akia na mwendo mkali sana huko San Marino Grand Prix huko Imola mwaka 1994...Familia ya Bianchi imeshukuru watu wote waliofariji familia hiyo toka siku ya ajali mpaka alipoaga dunia...Timu yake ya Marussia (Sasa inajulikana kama Manor) imesema Bianchi ameacha alama ya kuigwa ndani ya timu hiyo na atakumbukwa daima...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment