Friday, 28 February 2014

DUBAI TENNIS CHAMPIONSHIP: FEDERER ATAKUTANA NA DJOKOVIC NUSU FAINALI


Roger Federer atakutana na namba 2 duniani Novac Djokovic kwenye nusu fainali ya michuano mikali ya Dubai Tennis Championship baada ya kumchapa Lukas Rosol kutoka Czech 6-2, 6-2...Watazichapa leo kwa hiyo usikose kuicheki hiyo mechi kali sana kutoka Dubai...

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND

Saturday, March 1, 2014
TimeHome AwayVenue
15:00 GMT Everton  v  West Ham United Goodison Park
15:00 GMT Fulham  v  Chelsea Craven Cottage
15:00 GMT Hull City  v  Newcastle United The KC Stadium
15:00 GMT Stoke City  v  Arsenal Britannia Stadium
Postp Sunderland P - P West Bromwich Albion Stadium of Light
17:30 GMT Southampton  v  Liverpool St. Mary's Stadium
Sunday, March 2, 2014
TimeHome AwayVenue
16:30 GMT Aston Villa  v  Norwich City Villa Park
16:30 GMT Swansea City  v  Crystal Palace Liberty Stadium
16:30 GMT Tottenham Hotspur  v  Cardiff City White Hart Lane

LA LIGA: RATIBA YA MECHI YA LEO NA WEEKEND

Friday, February 28, 2014
TimeHome AwayVenue
19:30 GMT Athletic Bilbao  v  Granada San Mames Barria
Sunday, March 2, 2014
TimeHome AwayVenue
11:00 GMT Villarreal  v  Real Betis El Madrigal
16:00 GMT Atletico Madrid  v  Real Madrid Vicente Calderon
18:00 GMT Sevilla FC  v  Real Sociedad Estadio Ramon Sanchez Pizjuan
20:00 GMT Barcelona  v  Almeria Camp Nou
20:00 GMT Rayo Vallecano  v  Valencia Campo de Vallecas

F1: TESTING INAANZA LEO BAHRAIN



F1 testing yaanza huko Bahrain...Hali ya hewa iko safi sana kwa timu za F1 kujaribisha magari yao...Red Bull inabidi wafanye kazi ya ziada kutokana na kutofanya vizuri katika majaribio ya mwanzo huko Spain...Tunatarajia kuwaona hawa madereva leo kwenye circuit ya Bahrain....

Red Bull - Daniel Ricciardo
Mercedes - Nico Rosberg
Ferrari - Kimi Raikkonen
Lotus - Pastor Maldonado
McLaren - Kevin Magnussen
Force India - Sergio Perez
Sauber - Adrian Sutil
Williams - Valtteri Bottas
Toro Rosso - Daniil Kvyat
Caterham - Kamui Kobayashi
Marussia - Max Chilton

Bofya hapa upate Live updated za testing... 

Wednesday, 26 February 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA MECHI ZA LEO

Wednesday, February 26, 2014
TimeHome AwayStageVenue
19:45 GMT Galatasaray  v  Chelsea Round of 16 Türk Telekom Arena
19:45 GMT Schalke 04  v  Real Madrid Round of 16 Veltins-Arena

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Tuesday, February 25, 2014
StatusHomeScoreAwayStageVenue
FT Zenit St Petersburg 2-4 Borussia Dortmund Round of 16 Petrovski Stadium (16,000)
FT Olympiakos 2-0 Manchester United Round of 16 Karaiskakis Stadium (32,000)

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MAN U WACHEZA OVYO NA KUCHAPWA BILA UBISHI NA OLYMPIAKOS


Manchester United jana usiku ilicheza mpira mbovu sana na kujikuta ikuchapwa na Olympiakos mabao 2 kwa 0...Timu 16 zimebaki na sasa itabidi wajitahidi mzunguko wa pili...Mnamo dakika ya 38 Alejandro Dominguez alipachika goli na baadae Joel Campbell ambaye yuko kwa loan kutoka Arsenal alichapa la pili dakika ya 54...Man U hawakuwa makini kabina na kupotteza mipira sana na pasi hafifu na juu ya hapo muda wote wa game wamapata shot 1 tu golini...Refa nae alikuwa sio mtu wa kutoa toa kadi ovyo alikuwa mtu wa kazi na alipeta faulo nyingi za pande zote kwa ufupi alitaka watu wacheze mpira na sio kulalamika kila wakati...Bofya hapa upate mengineyo yaliotokea jana...

Tuesday, 25 February 2014

Max Sports: UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA LEO

Max Sports: UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA LEO: Tuesday, February 25, 2014 Time Home   Away Stage Venue 17:00 GMT Zenit St Petersburg  v  Borussia Dortmund Round of 16 ...

CHAN: KENYA HAS BEEN SELECTED TO HOST CHAN


Kenya has been selected to host CHAN 2018 (African Nations Championship 2018).

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA LEO

Tuesday, February 25, 2014
TimeHome AwayStageVenue
17:00 GMT Zenit St Petersburg  v  Borussia Dortmund Round of 16 Petrovski Stadium
19:45 GMT Olympiakos  v  Manchester United Round of 16 Karaiskakis Stadium

LA LIGA: BARCA YALIPA MAMILIONI KWENYE KESI YA KODI



Barcelona wamelazimika kulipa mamilioni ya pesa kutokana na kesi ya kodi iliyokuwa inawakabili...Barcelona sasa wamelipa milioni 13.5 euros ambazo ni deni la kukwepa kodi...Hii imetokea wakati wakimchukua dogo kutoka Santos, Neymar, ambapo walilipa pounds 48.6 milioni...Ila Barca wamekataa kwamba walikwepa kodi lakini wanasema ni issue ya kimikataba zaidi na wameamua kulishughulikia kwa kulipa pesa hizo...Sasa Neymar amesababisha club ya Barca kutumia pounds milioni 106.8...Bofya hapa upate habari zaidi.....

Monday, 24 February 2014

SOCHI 2014: CANADA YAMCHAPA SWEDEN 3-0


Canada ilitetea medali zake jana baada ya kumchapa Sweden 3-0 huko Sochi Urusi...Sasa kati ya Olympic nne wameshinda Gold Olympic 3 na kuwa wakali wa dunia katika mchezo huo wa Ice Hockey...Ice Hockey ni mchezo wa Canada wa Taifa na wamebobea sana....

Wafungali walikuwa Jonathan Toews kipindi cha kwanza na pia Sidney Crosby ambaye ni Captain alipata goli kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo na pia Cris Kunitz alipachika bao...Michezo hiyo ya Sochi pia iliisha jana kwa show kubwa nzuri ya kufunga mashindano hayo...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: LIVERPOOL YASHINDA KATIKA GAME KALI DHIDI YA SWANSEA


Game ya Liverpool na Swansea ilikuwa kali na iliishia na magoli mengi na Liverpool kuibuka mshindi....Liverpool ilishinda magoli 4 kwa 3 baada ya Daniel Sturridge kupachika bao dakika ya 2 na badae kidogo Jordan Henderson kupachika bao la pili...

Swansea walijibu na shuti la yadi 20 kutoka kwa Jonjo Shelvey na pia Wilfred Bony dakika ya 27 alipachika bao na kuweka timu yako level na Liverpool...Sturridge alipachika goli lake la 2 na badae Swansea walipata penalty dakika ya 47 na Bony ndiye aliyefunga na kusawazisha na baada ya hapo dakika ya 74 Henderson alipachika goli la ushindi....

GOLF: JAYSON DAY ASHINDA WGC MATCH PLAY KWA MARA YA KWANZA


Jayson Day kutoka Australia aliweza kumshinda Victor Dubuisson kwenye mashindano makali ya WGC Match Play kwa mashimo matano ya nyongeza...Mchezo huo wa Golf ulifanyika Dove Mountain Arizona huko Marekani...Dubuisson alianza vizuri hayo mashindano na pia alianza kupata umaarufu baada ya kushinda Turkish Open ambapo alimshinda Tiger Woods na Justin Rose...

VPL: SIMBA YASALIM AMRI KWA JKT RUVU


Simba Sports Club wana wa Msimbazi jana walishindwa kunguruma dhidi ya JKT Ruvu kwa kuchapwa 3-2...Bao la kwanza lilitoka kwa Hussein Bunu baada ya pasi kali kutoka kwa  Mbaga...Simba waliamka kipindi cha pili na kuchuza vizuri kidogo lakini hawakuweza kushinda...Sasa matokeo haya yanaiweka Yanga nafasi nzuri ya kusogelea kombe mara ya pili...

Squad zao zilikuwa kama hapo chini...

Simba: Yaw Berko, William Lucian 'Gallas', Henry Joseph,  Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Awadh Juma, Said Ndemla, Amissi Tambwe, Amri Kiemba, Haruna Chanongo.

JKT Ruvu: Shaaban Dihile,  Damas Makwaya, Edward Charles, George Minja, Salum Mtaki, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Emmanuel Swita, Idd Mbaga, Hussein Bunu, Sosthenes Manyasi

Friday, 21 February 2014

NBA: LeBRON AUMIA KWENYE GAME



LeBron James wa Miami Heat aliumia na kutoka damu kwenye court kipindi cha nne wakati wakicheza na Oklahoma City...LeBron aligongana na Serge Ibaka na kujikuta akiangalia sakafu ya court wakati damu zikitoka...Hii ilitokea kipindi cha nne dakika 6 kabla game kuisha wakati LeBron James akienda kufunda goli akakutana na kipepsi (elbow) cha Ibaka na ndio damu zikaana kutoka nyingi kwenye pua...LeBron kabla ya tukio hilo alikuwa na points 33 na walishinda game 103-81...

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND

Saturday, February 22, 2014
TimeHome Away
12:45 GMT Chelsea  v  Everton
15:00 GMT Arsenal  v  Sunderland
15:00 GMT Cardiff City  v  Hull City
15:00 GMT Manchester City  v  Stoke City
15:00 GMT West Bromwich Albion  v  Fulham
15:00 GMT West Ham United  v  Southampton
17:30 GMT Crystal Palace  v  Manchester United
Sunday, February 23, 2014
TimeHome Away
13:30 GMT Liverpool  v  Swansea City
13:30 GMT Newcastle United  v  Aston Villa
16:00 GMT Norwich City  v  Tottenham Hotspur

Thursday, 20 February 2014

SOCCER: JUVE YAONGEZA KASI YA KUMSAKA VERRATTI


Juventus sasa imeongeza kasi ya kumnyakua Marco Verratti midfielder kutoka Paris Saint-Germain...Verratti pia anafukuziwa na Manchester United...PSG wametuma scouts kenda kumcheki na habari hizi zimetoka kwenye gazeti la L 'Equipe...Lakini huyu dogo kutoka Italia ametia saini extension ya mkataba ingawa alipata tabu kutulia Ufaransa...Dogo alitokea Serie B timu ya Pescara mwaka 2012 na alikuwa anatarajiwa kuwa the next 'Andrea Pirlo'...Ngoja tuone nani atamnyakua dogo kwenye transfer ya kati ya mwaka...Endelea kusoma Max Sports upate habari mpya mpya upesi...

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YAFUNGWA NA BAYERN


Arsenal jana usiku ilishindwa kuwafunga wajerumani Bayern Munich...Game iliisha 2-0 baada ya kuona mpira mzuri kutoka timu zote mbili lakini Arsenal ilizidiwa kutokana na kutolewa nje kwa kipa wa Arsenal, Szczesny, kwa challenge ambayo refa aliona ni hatari na kutoa kadi nyekundu lakini haikuwa hatari kihivyo...Mesut Ozil alikosa penalty na pia baada ya kadi nyekundu David Alaba wa Bayern alikosa penalty baadaa ya kugonga mwamba...

Goli lilipatikana dakika ya 54 baada ya shoti zuri kupigwa na Kroos na kufanya kipa wa ziada Fabianski...Goli lingine lilikuja dakika za mwishoni baada ya substitute Thomas Muller kufunga...Sanogo pia alianza na kusaidia sana Arsenal lakini alishindwa kupachika mpira wavuni...Bofya hapa upate habari zaidi...

Wednesday, 19 February 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCA WAIZIDI MAARIFA MAN CITY



Manchester City jana walichapwa na Barcelona kwenye mechi kali ambayo iliona Barca wakidominate na Man City wakikosa chances nzuri zakufunga...


Baada ya kutoka sare dakika 45 za mwanzo Martin Demichelis alipomkwatua Messi mara baaada ya mwanzo mwa kipindi cha pili na kupewa kadi nyekundu na ikabidi aende akaicheki game nyumbani kwake...

Messi akaamka akajipangusa alafu akapachika penalty ambapo Joe hart alikasirika kwanini ameshindwa kuzuia shuti la Messi...Dani Alves mwishoni akapachika la 2 na kufanya mlima uwe mkali kwa Man City...

Tuesday, 18 February 2014

F1: RED BULL WANATARAJIA KUFANYA VIZURI BAHRAIN


Timu ya Red Bull inatarajiwa kufanya vizuri katika majaribio ya F1 huko Bahrain kuanzia kesho...Red Bull hapo awali ilishemsha katika jaribio la gari lao jipya huko Jerez Spain na waliweza kumaliza lap 21 tu katika siku nne...Pia huko Bahrain Lotus itakuwa timu ya mwisho kuonyesha gari lao jipya na kulijaribu kwenye circuit ya Bahrain...Mwaka huu sheria zimeleta engine za 1.6 litre V6 Turbo na energy recovery systems kwahiyo timu zote zinamtihani wa kujifunza kutumia haya mabadiliko kwa muda mfupi...

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA MECHI ZA LEO NA KESHO

Tuesday, February 18, 2014
TimeHome AwayStageVenue
19:45 GMT Bayer Leverkusen  v  Paris Saint-Germain Round of 16 BayArena
19:45 GMT Manchester City  v  Barcelona Round of 16 Etihad Stadium
Wednesday, February 19, 2014
TimeHome AwayStageVenue
19:45 GMT AC Milan  v  Atletico Madrid Round of 16 Stadio Giuseppe Meazza
19:45 GMT Arsenal  v  Bayern Munich Round of 16 Emirates Stadium

Monday, 17 February 2014

NBA ALL-STARS: KYRIE IRVING MVP


MVP wa All-Star games mwaka huu ni Kyrie Irving kutoka Cleveland Cavaliers...Irving ameonesha dunia na mashabiki wa basketball kwamba akiwa katika kundi la wakali wa mchezo huo na yeye anaweza kuonekana mkali...

Irving alipata point 31 na assists 14 ambazo zilisaidia East kutoka point 18 chini na kushinfa West 163-155 katika game kali iliyojaa masupastaa kibao...

Ingawa Irving sio supa staa kivile na timu yake haifanyi vizuri lakini mashabiki walimchagua Irving katika timu ya East akijumuika na vichwa vikali sana kama LeBron James, Carmelo Anthony na Dwyane Wade...Bofya hapa upate kumjua zaidi MVP Irving.....

FA CUP: ARSENAL YAMTOA LIVERPOOL KWENYE MASHINDANO


Arsenal jana ilipata muda wakulipiza kisasi kutokana ka kuchapwa awali na Liverpool...Arsenal ilishinda 2-1 kwenye game kali ya round ya 5 ya FA Cup Emirates Stadium jana jioni...Oxlade-Chamberlain alipachika goli kwenye dakika ya 16 tu baada ya kupata loose ball...Pia alisababisha goli la pili mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kipiga cross ambayo ilimkuta Lukas podolski ambaye alichapa mkwaju kutoka yadi 15 na tutingisha nyavu...Livepool walipata goli lakufutia machozi baada ya Steve kupata bao la penalty...dogo wa Arsenal, Yaya Sanogo, ndiyo alikuwa gumzo jana baada ya Arsena Wenger kumuanzisha na kuacha mashabiki wakishangaa dogo akisumbua sana lango la Liverpool mapema sana...  Bofya upate habari zaidi hapa...

Sunday, 16 February 2014

FA CUP: MATOKEO YA MECHI ZA WEEKEND (FIFTH ROUND)

Sunday, February 16, 2014
StatusHomeScoreAwayStageVenue
FT Everton 3-1 Swansea City Round 5 Goodison Park (31,498)
FT Sheffield United 3-1 Nottingham Forest Round 5 Bramall Lane (25,118)
FT Arsenal 2-1 Liverpool Round 5 Emirates Stadium
Saturday, February 15, 2014
StatusHomeScoreAwayStageVenue
FT Sunderland 1-0 Southampton Round 5 Stadium of Light (16,777)
FT Cardiff City 1-2 Wigan Athletic Round 5 Cardiff City Stadium (17,123)
Postp Sheffield Wednesday P - P Charlton Athletic Round 5 Hillsborough
FT Manchester City 2-0 Chelsea Round 5 Etihad Stadium (47,013)

Friday, 14 February 2014

VPL: OKWI RUKSA KUICHEZEA YANGA


Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura, amesema Emanuel okwi kutoka Uganda sasa ruksa kusajiliwa na Yanga...Maagizo hayo yametoka kweye shirikisho la soka duniani FIFA kwamba Okwi sasa yuko huru kusajiliwa na Yanga...Okwi alitoka Sports Club Villa ya huko Uganda na kujiunga na Yanga lakini usajili wake ulizuiliwa...Okwi hakuelewana na timu kutoka Tunisia Etoile Du Sahel ndio akajishkiza S.C. Villa...

NBA: WADE ANAWEZA KUKOSA ALL-STAR GAMES


Mchezaji maarufu kutoka Miami Heat, Dwyane Wade, anaweza kukosa All-Star games ambazo zitaanza hivi karibuni. All-Star games michezo mbali mbali inayohusu basketball ambayo inajumuisha wachezaji wakali sana na pia wachezaji wapya wa mwaka wa kwanza (rookies)...Wade anatatizo kwenye mguu la 'aggravated nerves' ambalo linafanya mguu unakosa fahamu...Wade alikosa game dhidi ya Golden State Warriors kutokana na tatizo hilo...

Thursday, 13 February 2014

COPA DEL REY: BARCELONA REACH FINAL WITH REAL MADRID


Barcelona will play Real Madrid in the Copa Del Rey final on April 19 .

Messi helped Barcelona beat Real Socedad. He went through three defenders to score a superb goal.

Real Madrid won by 3-1.

SOCHI 2014: HISTORIA YATOKEA KWENYE MASHINDANO YA DOWNHILL


Kwa mara ya kwanza kutokea katika Olympics kwenye shindano la downhill kwa watu wawili kushida medali ya gold...Hii ilitokea kwenye mashindano ya kuteleza kwenye theluji (snow) ya downhill ambapo Tina Maze na Dominique Gisin walimaliza muda sawa na kushinda medali ya gold...Walipokabithiwa medali walipanda pamoja na kushikana mikono juu...

EPL: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Wednesday, February 12, 2014
StatusHomeScoreAwayVenue
FT Arsenal 0-0 Manchester United Emirates Stadium (60,021)
Postp Everton P - P Crystal Palace Goodison Park
Postp Manchester City P - P Sunderland Etihad Stadium
FT Newcastle United 0-4 Tottenham Hotspur St James' Park (48,264)
FT Stoke City 1-1 Swansea City Britannia Stadium (24,822)
FT Fulham 2-3 Liverpool Craven Cottage (25,375)

Wednesday, 12 February 2014

SQUASH: NICK MATTHEW AMCHAPA BINGWA WA DUNIA ASHAOUR NA KISHINDA SWEDISH OPEN


Nick Mattew amemchapa bingwa wa squash duniani Ramy Ashour katika game 5 kali sana na kuchukua ubingwa wa Swedish Open...Matthews kutoka Uingereza ameweza kupanda na kuwa namba 1 sasa kutokana na ushindi huu huko Linköping, Sweden....Matthews alitumia dakika 91 tu kumchapa Ashour 11-13, 11-6, 11-8, 6-11, 11-4...


Ushindi huu unakuja baada ya kuweka historia ya kumchapa Gregory Gaultier  kwenye pambano kali ambalo wote walikuwa ranking sawa...Ni mara ya kwanza mabingwa wenye ranking sawa kupambana...Bofya hapa upate habari zaidi za mabingwa wa Squash

EPL: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Tuesday, February 11, 2014
StatusHomeScoreAwayVenue
FT Cardiff City 0-0 Aston Villa Cardiff City Stadium (27,597)
FT Hull City 0-1 Southampton The Kingston Communications Stadium (23,670)
FT West Ham United 2-0 Norwich City Upton Park (35,153)
FT West Bromwich Albion 1-1 Chelsea The Hawthorns (24,327)

Tuesday, 11 February 2014

EPL: RATIBA YA MECHI ZA LEO NA KESHO

Tuesday, February 11, 2014
TimeHome AwayVenue
19:45 GMT Cardiff City  v  Aston Villa Cardiff City Stadium
19:45 GMT Hull City  v  Southampton The Kingston Communications Stadium
19:45 GMT West Ham United  v  Norwich City Upton Park
20:00 GMT West Bromwich Albion  v  Chelsea The Hawthorns
Wednesday, February 12, 2014
TimeHome AwayVenue
19:45 GMT Arsenal  v  Manchester United Emirates Stadium
19:45 GMT Everton  v  Crystal Palace Goodison Park
19:45 GMT Manchester City  v  Sunderland Etihad Stadium
19:45 GMT Newcastle United  v  Tottenham Hotspur St James' Park
19:45 GMT Stoke City  v  Swansea City Britannia Stadium
20:00 GMT Fulham  v  Liverpool Craven Cottage