Monday 3 February 2014

NFL: SEAHAWKS MABINGWA SUPER BOWL XLVIII


Fainali ya NFL iliongelewa kwamba itakuwa fainali kali sana kwa kuwa timu moja ina defence bora sana na timu nyingine ina offence bora kuliko timu zote...Lakini haikuwa hivyo kilichotokea ni kwamba Seattle Seahawks waliwaburuza Denver Broncos mabao 43-8...Kitaa wanasema 'Noumer' au 'Soo'

Hii imeonyesha dunia timu yenye defence bora ndio inashinda...Denver walikimbizwa na mpaka ikawa aibu kwa timu kubwa kama hiyo kuchapwa na timu ambayo haijawahi kushinda Super Bowl...

Quarterback (QB) wao Payton Manning aliweza kurusha touchdown pass moja tu kwenye uwanja wa Metlife...Wakati QB wa Seattle Seahawks Russell Wilson ni mwaka wake wa pili kuichezea timu na ameweza kurusha pasi 25 na kati ya hizo 18 zilifika kwa yadi 206 pia na kurusha touchdown mbili...MVP wa mchezo ni Malcom Smith...Bofya hapa upate habari za Super Bowl...

No comments:

Post a Comment