Friday 31 July 2015

ARSENAL: THEO WALCOTT ASAINI MKATABA MPYA NA GUNNERS


Theo Walcott ameamua kubakia Arsenal baada ya kusaini mkataba abao utamweka Emirates kwa miaka 4...Walcott atapata pound za Uingereza 140,000 kwa wiki...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 30 July 2015

KAGAME CUP 2015: YANGA YATOLEWA NA AZAM FC


Azam FC imefanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la Kagame baada ya kuwatoa wakongwe Yanga kwa matuta...Yanga waliaga mashindano baada ya kukubali mabao ya matuta 5-4 kutokana na kutoka 0-0 kipindi cha kawaida...Azam walifunga mabao yao yote lakini Aishi Manula aliokoa penalty ya 3 ya Haji Mwinyi...Bofya hapa upate habari zaidi.

EUROPA LEAGUE: RATIBA YA LEO (GMT)

  • Kairat AlmatyvAberdeen15:45
  • West HamvAstra Giurgiu19:45
  • SouthamptonvVitesse20:05
  • IF ElfsborgvOdd17:00
  • AIKvAtromitos Athens18:00
  • Apollon LimassolvFK Qabala18:00
  • CASHPOINT SCR AltachvVitória Guimarães18:00
  • FK KrasnodarvSlovan Bratislava18:00
  • PAOK SalonikavSpartak Trnava18:00
  • SK Puntigamer Sturm GrazvRubin Kazan18:00
  • Slovan LiberecvHapoel Ironi Kiryat Shmona18:00
  • AZ AlkmaarvIstanbul Basaksehir18:30

FIFA: PLATINI ATAKA KUONGOZA FIFA WENZAKE HAWATAKI



Michel Platini ametangaza anataka kuwania kiti cha juu kabisa cha Shirikisho la Soka Duniani Fifa lakini wenzake amabo pia wana wania hawataki....Platini alitangaza Jumatano kwama anataka kuwania nafasi ya juu kabisa ya Fifa tarehe 26 mwezi wa 2 mwakani...Prince Ali bin al-Hussein na Musa Bility wamesema Platini sio chaguo zuri kwa Fifa kwa sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 28 July 2015

MANCHESTER UNITED: KIPA SERGIO ROMERO NDANI YA OLD TRAFFORD


 Manchester United wanazidi kuimarisha timu baada ya kumyakua Sergio Romero kipa kutoka Argentina...Kocha Louis van Gaal amesema walihitaji kipa mzuri kutokana na uwezekano wakampoteza David De Gea ambaye Real Madrid wanamtaka sana...Romero atachukua nafasi ya Victor Valdez ambae ameambiwa na kocha anaweza kusepa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 27 July 2015

KAGAME CUP 2015: YANGA YASHINDA NA SASA KUKUTANA NA AZAM FC


Yanga imefanikiwa kushinda mechi yake dhidi ya Al Khartoum ya Sudan bao 1-0...Khamis Tambwe ndiye aliyepachika bao pekee ingawa Yanga walikosa mabao ya wazi na wangeweza kuongoza kwa mengi lakini sasa wana uhakika wa kucheza robo fainali na Azam FC...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 26 July 2015

MANCHESTER UNITED: DI MARIA AINGIA MITINI


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema hajui kwanini Di Maria hakuingia kwenye ndege wakati wa ziara ya Man U kabla msimu haujaanza...Pia amesema Marcos Rojo hakuingia lakini Rojo anamatatizo na Passport yake...Gazeti moja la Ufaransa linaloitwa L'Equipe limesema Manchester United na Paris St-Germain wamekubaliana dau la pounds milioni 46.5 kwa Di Maria lakini bado mazungumzo yanaendelea...Manchester wametoka kuwachapa Barccelona 3-1 kweye mechi ya kirafiki...Bofya hapa upate habari zaidi za Man U.

KAGAME CUP 2015: AZAM YAIRARUA ADAMA CITY


Azam FC iko kileleni baada ya kuirarua Adama City ya Ethiopia mabao 5-0 kwenye michuano ya CECAFA inayoendelea jijini Dar es Salaam...Wafungaji mabao walikuwa Ivorian striker Kipre Tchetche ambae alipachika mabao 2, Farid Mussa, Mudadhir Yahya na Aggrey Morris...Azam walikuwa walikuwa na ball control safi toka mwanzo wa mechi na walistahili ushindi na sasa wanaongoza Group C wakiwa na oints 9...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 25 July 2015

KAGAME CUP: YANGA YAIZAMISHA KMKM 2-0

 
Donald Ngoma akimtoka beki Khamis Ali Khamis (Source:Michuzi Blog)

Dar es Salaam Young Africans jana wamefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano mikali ya Kagame Cup kwa kuichapa KMKM ya Zanzibar mabao 2-0 ndani ya uwanja wa Taifa...Timu zote zilicheza mpira safi lakini Yanga ndio waliokosa mabao mengi sana ya wazi kipindi cha 2 lakini nao KMKM kipindi cha kwanza walikuwa wanasumbua sana Yanga...


Busungu mnamo dakika ya 56 alipachika bao safi baada ya kupokea pasi kutoka kwa mchezaji mpya hatari Donald Ngoma kutoka Zimbabwe...Yanga pamoja na kushinda wako nafasi ya 3 wakiwa na points 6 ndani ya Group A...Bofya hapa upate habri zaidi.

Thursday 23 July 2015

CONCACAF GOLD CUP: FUJO ZATOKEA MECHI YA PANAMA NA MEXICO


Fujo kubwa ilitokea kwenye mechi ya Gold Cup chini ya Concacaf ambayo ilikuwa aibu sana kwa waandaaji...Panama walichapwa na Mexico na watacheza na Jamaica ambao waliwachapa kwa mshangao Wamarekani...


Mechi ya Mexico na Panama ilikuwa nzuri sana na ya kasi sana sema vikumbo na fouls zilikuwa vingi sana...


Fainali itafanyika Jumapili ndani ya Lincoln Financial Center jiji la Philadelphia...Bofya hapa upate habari zaidi.


Wednesday 22 July 2015

F1: LEWIS HAMILTON ATAMKUMBUKA BIANCHI KWENYE SALA MUDA WOTE


Lewis Hamilton amesema atamkumbuka marehemu Jules Bianchi kwenye sala muda wote wa maisha yake ya udereva...Alisema hayo kwenye msiba wa Bianch ambao ulihudhuriwa na watu wengi sana akiwemo Nico Roseberg, Sebastian Vettel, Jason Button, Fillipe Massa na wengine wengi...



Hamilton alisema kumuaga Bianchi haikuwa jambo rahisi kwa wote kuja kumuaga dereva mwenzao...Bofya hapa upate habari zaidi.

KAGAME CUP: AZAM YAINGIA ROBO FAINALI


Azam FC imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano mikali ya CECAFA Kagame Cup kwa kuichapa timu ya Sudan ya Kusini, Malakia, 2-0 ndani ya uwanja wa Taifa...Mabao yalipatikana vipindi vyote viwili na mabao yalitoka kwa John Bocco na Kipre Tchetche...Hapo awali Azam waliwachapa KCC 1-0 Jumapili na sasa wameigia robo fainali wakiwa na game 1 ya ziada...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 21 July 2015

OPEN CHAMPIONSHIP: ZACH JOHNSON BINGWA ST. ANDREWS


Mmarekani Zach Johnson ameshinda play-off ya watu watatu na kuchukua ubingwa wa British Open...Johnson ameshinda major yake ya 2 mwaka 2007 alishinda Masters...Johnson alipambana na Louis Oosthuizen wa Afrika ya Kusini na Marc Leishman wa Australia kwenye mashimo manne ya ziada...Bofya hapa upate habari zaidi.

PELE: MCHEZAJI MAARUFU SANA WA ZAMANI PELE ATOKA HOSPITALI


Pele ametoka hospitali baada ya kufanyiwa operation ya mgongo...Pele alikuwa anasumbuliwa na mshipa wa fahamu ambao ulibanwa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 20 July 2015

CHAMPIONS LEAGUE: RATIBA YA MECHI (GMT)

  • Dila GorivPartizan Belgrade 13:30
  • FC PyunikvMolde
    (agg 0 - 5)
    15:00
  • Milsami OrheivLudo Razgd
    (agg 1 - 0)
    16:00
  • HJK HelsinkivFK Ventspils
    (agg 3 - 1)
    17:00
  • Maccabi Tel AvivvHibernians FC
    (agg 1 - 2)
    18:30
  • Lincoln Red ImpsvFC Midtjylland
    (agg 0 - 1)
    19:00
  • VardarvApoel Nic
    (agg 0 - 0)
    19:00
  • ZalgirisvMalmö FF
    (agg 0 - 0)
    19:10
  • Crusaders FCvSkenderbeu Korce
    (agg 1 - 4)
    19:45
WED 22 JUL 2015 - CHAMPIONS LEAGUE
  • FC AstanavNK Maribor
    (agg 0 - 1)
    15:00
  • Fola EschvDinamo Zagreb
    (agg 1 - 1)
    19:00
  • Steaua BucharestvAS Trencín
    (agg 2 - 0)
    19:30

FIFA: PLATINI AOMBWA AGOMBEE NAFASI YA JUU KABISA YA FIFA


Rais wa UEFA toka 2007, Michel Platini, ameombwa na wadau wengi wakubwa wa soka agombee nafasi ya Urais wa Fifa...Platini amesema anasupport ya Confederation yake na Asia, Marekani ya Kaskazini, Visiwa vya Caribbean, Marekani ya Kusini na Marekani ya Kati...Sepp Blatter ambae anaondoka ataanzisha mjadala wa mabadiliko ya Fifa na atakutana na executive committee kuhusu tarehe ya uchaguzi wa Fifa lakini Confederatin nyingi wangependelea tarehe 6 Desemba iwe siku ya uchaguzi...Bofya hapa upate habari zaidi  

Saturday 18 July 2015

F1: JULES BIANCHI DIES AT SUZUKA



Formula One has lost a young driver,  lJules Bianchi, 9 months  since the horrific accident at Suzuka, Japan.


His car hit a heavy duty machine vehicle and went under it.

He went into a coma until he passed away.

He was the first driver to die on track after the F1 legendary driver Ayrton Senna.

Senna died after hitting a barrier at very high speed during the San Marino Grand Prix at Imola in 1994.

Bianchi's family has thanked all well wishes since the day of the accident until his passing.

Team Murrusia, now called Manor, said Bianchi lhas left a mark that should be emulated inside their team and will be remembered forever.

Friday 17 July 2015

EPL: LIVERPOOL MBIONI KUMCHUKUA BENTEKE


Liverpool sasa wanauhakika wa kufikia dau ambalo Aston Villa wameliweka la ponds milioni 32.5 la kumchukua Christian Benteke mwenye umri wa miaka 24...Liverpool wamepata pesa za kutosha sasa kutokana na mauzo ya Rheem Sterling ya milioni 49...Benteke alifunga mabao 12 katika mechi 12 kuisaidia Aston Villa kubaki kwenye Premiership mwishoni mwa msimu uliopita...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 16 July 2015

MANCHESTER UNITED: VALDES KUUZWA BAADA YA KUKATAA KUCHEZA


Kipa wa Manchester United Victor Valdez atauzwa kutokana na kukataa kuchea reserves...Habari hiyo ametoa kocha Luis Van Gaal na kusema Valdes hakubaliani na filosofia yake na kutokana na hilo hana nafasi kwenye timu...Valdes alitoa tweet yake akaandila '.....? #Respect...


Valdes aliachwa kwenye safari ya kwenda Marekani...Van Gaal amesema De Gea bado yopo yupo mpaka wapate bei kubwa ndio watamwachia...Bofya hapa upate habari zaidi.

NIGERIA: SUNDAY OLISEH KOCHA MPYA


Shirikisho la Mpira la Nigeria limemchukua Sunday Oliseh kuwa kocha wao mpya...Oliseh anachukua nafasi ya Stephen Keshi aliyefukuzwa hivi karibuni...Oliseh alichezea timu ya Taifa ya Nigeria mara 63 na alisaidia timu hiyo ya Super Eagles kuchukua ubingwa wa Africa mwaka 1994 pamoja na Olympic gold mwaka 1996...


Oliseh amechezea timu kubwa za Ulaya kama Burussia Dortmund, Ajax na Juventus kwa hiyo ataleta uzoefu wake usaidie Super Eagles lakini haita kuwa rahisi kwani kutokana na siasa chafu ndani ya Shirikisho la Soka la Nigeria limeyumbisha sana maendeleo ya timu hiyo ya Taifa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 13 July 2015

ARSENAL: TASWIRA YA SAFARI YA ARSENAL KWENDA SINGAPORE NDANI YA NDEGE YAO











MANCHESTER UNITED: MORGAN SCHNEIDERLIN AKAMILISHA USAJILI ANASUBIRI USHAURI WA DAKTARI


French international Morgan Schneiderlin yuko tayari kuichezea Manchester United baada ya makubaliano ya pounds milioni 24 kukamilika na anategemewa kukaa Old Trafford kwa miaka 4...Morgan alitokea Southampton na anacheza nafasi ya midfield na ameingia AON Training Complex tayari kwa kupata medical tests aweze kupitishwa rasmi kama mchezaji wa Manchester United...Bofya hapa upate habari zaidi.

MANCHESTER CITY: RAHEEM STERLING AKUBALI DAU LA MAN CITY


Raheem Sterling amekubali kuingia Manchester City kwa dau la pounds za Uingereza milioni 49...Manchester City watatoa pounds milioni 44 awali na milioni 5  badae...Sterling alizua mzozo mkubwa sana Liverpool kutokana na dau la kumbakiza lakini sasa maneno yameisha na atapokea zaidi ya pounds 180,000 kwa wiki kwa miaka 5...Sterling atakuwa mchezaji tajiri sana mwenye umri wa miaka 20 katika historia ya Premier League...Bofya hapa upate habari zaidi.

WIMBLEDON 2015: DJOKOVIC AMCHAPA FEDERER NA KUCHUKUA UBINGWA WIMBLEDON


Novak Djokovic bingwa wa mwaka jana Wimbedon amemchapa bingwa mara 7 Roger Federer katika mechi kali sana iliyofanyika jana...Djokovic alimchapa Federer 7-6 (7-1) 6-7 (10-12) 6-4 6-3 ndani ya masaa mawili na dakika 56...Djokovic sassa amewapita wakongwe wa tennis duniani kama Jimmy Connors, Andre Agassi na Ivan Lendl katika list ya washindi wa vikombe vikubwa 'majors'...Djokovic alisema haikuwa rahisi kucheza na Federer mtu ambae watu wengi wamekua kwa kufuata kutokana na umahiri wake wa tennis...

Kocha wa Djokovic Boris Becker akiwa na mke wa
Djokovic Jelena
Kocha wa Djokovic mkongwe wa tennis Boris Becker alifurahi sana kutokana na ushindi huu mkubwa katika ulimwengu wa tennis duniani...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 9 July 2015

FIFA: CHUCK BLAZER AFUNGIWA MAISHA


Katibu Mkuu wa zamani wa Concacaf na executive committee member Chuck Blazer afungiwa maisha kushiriki biashra yoyote inayohusu soka...Habari zilizoingia hivi punde tu zinasema kutokana na vitendo vyake vya rushwa na kushtakiwa kupokea na kutoa rushwa wakati Afrika ya Kusini ilipozawadiwa kuwa mwenyeji wa World Cup...Blazer alianza kushirikiana na prosecutors wa Marekani muda mrefu ili kufichua uovu wa rushwa ya muda mrefu ndani ya Fifa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday 8 July 2015

BOXING: WBO WACHUKUA MKANDA WAO KUTOKA KWA MAYWEATHER


World Boxing Organisation wachukua mkanda wao wa welterweight ambao Mayweather alishinda kwenye pambano lake na Manny Paquiao...Sababu ya kuchukua mkanda ni kutokana na Mayweather kushindwa kulipa kiwango cha kuendesha pambano ambacho ni dola 200,000...


Mayweather amepewa mpaka tarehe 20 kukata rufaa...Kuanzia sasa Timothy Bradley ndio atatambulika kama mtu aliyeshikilia huo mkanda...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday 7 July 2015

SWIMMING: WATATU KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA YA FINA


Watanzania wa 3 wataenda Urusi kushiriki mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya FINA World Championship...Mashindano hayo yatafanyika kuanzia July 24 mpaka August 9 na yatafanyika Kazan, Urusi...Katibu Mkuu msaidizi wa chama cha kuogelea cha taifa (TSA) Marcelino Galinoma amessema wataowakilisha Tanzania ni Magdalena Moshi, Hilal Hilal na Amaar Ghadiyali...Watakuwa chni ya kocha Samson Makere...Bofya hapa upate habari zaidi.

WOMEN'S WORLD CUP: MAREKANI YACHAPA 5 NA KUCHUKUA KOMBE


Timu ya wanawake ya Marekani wanenyakua ubingwa wa dunia...Tumu ya USA imechukua kombe kwa mara ya 3 sasa kwa kumchapa Japan 5-2...

Nyota wa mchezo alikuwa Carli Lloyd ambaye alitumia daakiak 13 kupata 'hat-trick' na kati ya bao lake moja alipiga mkwaju kutoka katikati ya uwanja na kutingisha nyavu....


Rais wa Caf Issa Hayatou akikabidhi kombe kwa captain wa zamani Christie Rampone na veteran stiker Abby Wambach...Bofya hapa upate habari zaidi.