Saturday, 21 June 2014

WORLD CUP 2014: SAJO NA WADAU NDANI YA BRAZIL

Mdau Sajo Kibonde na Wasia Mushi wakiwa na bendera ya Tanzania wakituwakilisha vyema huko Brazil...Safi sana wadau...

Sajo Kibonde (kushoto) na Wasia Mushi (wa 4 kutoka kushto) wakiwa na wenyeji wao huko Brazil - Picha kwa hisani ya Materi a.k.a Bucha

WORLD CUP 2014: JOE MARO NA WENZAKE WATUWAKILISHA SAO PAULO

Mdau wa Max Sports Joseph Maro na wenzake wanatuwakilisha vyema huko Sao Paulo kwenye World Cup...Tunashukuru sana kwa kutuwakilisha...Brazuka!

Joe Maro (Kulia) na wadau wenzake

Sehemu zote ukipita utakutna na screen kubwa

MAZOEZI: GYM MPYA NA YA KISASA IMEFUNGULIWA UPANGA

Just Fitness ni Gym mpya na yenye vifaa vya kisasa imefunguliwa Upanga mtaa wa Mindu opposite Richmond Appartments...Karibuni wadau wote...Ukiwa unatoka kazini na hautaki kukaa kwenye foleni zetu za Dar basi unakaribshwa ufanye mazoezi...Walimu waliobobea katika mazoezi na pia waliobobeea katika mafunzo ya kuogelea pia wapo...Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako... Pata picha hapo chini za Just Fitness...










Karibuni wote...

WORLD CUP 2014: BENZEMA AIWASHIA MOTO USWISS

Hebu mcheki Benzima alivyo wawashia moto Switzerland hapo chini...Uswss walichapwa 5-2...



Friday, 20 June 2014

WORLD CUP 2014: ROY HODGSON AGOMA KUJIUZULU


Kocha wa England amegoma kujiuzulu baada ya kuchapwa na Uruguay 2-1...Sasa England ina hali tete sasa kwani nafasi ya kuingia kwenye mtoano imekuwa finyu sana...Hii haijawahi kutokea kwa England kuondoka mapema toka 1954...England sasa wanasubiri game ya Italy na Costa Rica...Italy wakishinda England itasonga mbele...Pata habari zaidi hapa...

YANGA: MAZISHI YA GEORGE 'CASTRO' MPONDELA

Watoto wa Marehemu wakiweka shada la maua

Rais w TFF Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Yusuf Manji CEO wa Quality Group

Yusuf Manji akiweka shada la maua

Rais wa TFF Jamal Malinzi kiweka shada la maua



Thursday, 19 June 2014

ATHLETICS: JUSTIN GATLIN ANAONGOZA KWA MBIO 2014


Justin Gatlin, bingwa wa kukimbia na mshindi wa medani ya dhahabu katika Olympics za 2004, alikimbia mbio za mita 100 kwa kutumia sekunde 9.86 jana.... Mpaka sasa anaongoza mwaka huu kwa kuwa mtu mwenye spidi kuliko wote...Gatling alikimbia  kwenye mashindano ya Golden Spike huko Czech Republic...

WORLD CUP 2014: SPAIN YAVUNJA REKODI


Vargas akipachika bao

Spain jana ilivunja rekodi kuwa timu ya kwanza ambayo ni mabingwa watetezi kufungwa mechi mbili za mwanzo na kutolewa...Hii ilitokea katika uwanja wa Maracana baada ya kuchapwa 2-0 na Chile...Spain sasa umahiri wao kwa miaka 6 ndio umeisha... Chile walicheza vizuri sana na pia goli lao la kwanza lilikuwa la kiufundi sana na aliye funga alikuwa Eduardo Vargas kwenye dakika ya 20...
 
Casillas akifungwa baada ya kutokuwa makini

Chales Aranguiz alipachika bao la 2 mnamo dakika ya 43 baada ya Ike Casillas kutokuwa makini...Chile na Netherlands watasonga mbele kwenye mtoano...Bofya hapa usome zaidi....

WORLD CUP 2014: NETHERLANDS WATOLEWA JASHO NA AUSTRALIA



Netherlands jana walikimbizwa na Australia ambayo ni timu yenye rank ya chini kuliko zote kwenye World Cup ya mwaka huu...Katika uwanja wa Beira Rio Australia walicheza mpira mzuri sana bila kuogopa mtu na Netherlands walikuwa wanasali mpira uishe maana kuna kipindi walikuwa nyuma 2-1 na Van Persie alirudisha bao wakawa sawa... Tim Cahill ambaye sasa anacheza soka huko Marekani alipachika bao zuri sana...Netherlands inabidi wajipange maana hii World Cup sio ya mzaha kabisa...Bofya hapa usome zaidi....

Wednesday, 18 June 2014

SQUASH: HUDHAIFA ASHRAF ASHINDA JUNE DAR GHYMKHANA CLUB JUNIOR BELL

Ashraf akipokea zawadi kutoka kwa Mr. Marwa Busigara

anayejitahidi sana Hudhaifa Ashraf ameshinda michuani ya mwezi wa June...Ashraf pia alikuwa mshindi ya muchuano ya mwezi May...Nafasi ya 2 ilichukuliwa na dogo mwingine mkali Fadhili Ally...
 
Fadhili Ally akipokea zawadi


Junior Bell ya mwezi huu imekuwa kivutio kikubwa sana na hasa pia support ya familia ya walioshiriki imesaidia sana...Hongera kwa washindi na walioshiriki...

WORLD CUP 2014: FRANCISCO GUILLERMO OCHOA AWA KINARA WA GAME YA BRAZIL NA MEXICO



Guillermo Ochoa kipa wa Mexico amekuwa kinara wa mechi kali sana ambayo mpaka sasa tulikuwa hatujawahi kuona mechi kali kama hii ya Brazil na Mexico...

Tuesday, 17 June 2014

YANGA: MPONDELA KUZIKWA KESHO KUTWA KINONDONI


Katibu Mkuu wa zamakni wa YANGA marehemu George 'Castro' Mpondela aliyefariki kutokana na kuugua ugonjwa wa Moyo anatarajiwa kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni Alhamisi ijayo...Kwa habari zilizoingia Max Sports hivi punde ni kwamba mwili wa marehemu utalala nyumbani kwake kesho huko Kigamboni na Alhamisi kutakuwa na misa heshima za mwisho Kanisa Katoliki Muhimbili saa 7 na baada ya hapo atapelekwa kupumzika katika makaburi ya Kinondoni...Apumzike kwa Amani...

EPL: CHELSEA WANAMTAKA SANA TONI KROSS


Chelsea FC wamemwekea dau kijana matata mwenye umri wa miaka 24 Toni Kross  kutoka Bayern Munich na wanataka kumlipa 130,000 kwa mwezi pound za Uingereza... Wengine wanaomwania Toni ni Real Madrid na Manchester United....

GOLF: KINARA WA GOLF TANZANIA NURU MOLLEL ASHINDA HUKO ARUSHA


Nuru Mollel kijana mkali sana katika mchezo wa Golf nchini Tanzania ameshinda michuano mikali ya K.N.L. Legal Golf Tournament huko Arusha Gymkhana Club (AGC)...Mollel alipata score ya -4 (four-under) 40 points...Katika mashindano haya makali yaliyotumia mfumo ya stable ford Mollel alimpita Fransis Julius ambaye alikuwa wa 2 na wa 3 alikuwa Peniel Uriwa...Bofya zaidi hapa upate mambo zaidi...

WORLD CUP 2014: DRAW YA KWANZA BILA KUFUNGANA KWENYE WORLD CUP NI KATI YA NIGERIA NA IRAN


Katika game mbovu toka michuano hii ianze ni hii ya Nigeria na Iran...

WORLD CUP 2014: USA YAANZA VIZURI


USA meanza vizuri michuano ya World Cup huko Brazil kwa kuichapa Ghana 2-1...USA wameweka rekodi kwa kufunga goli la 5 la haraka katika historia ya World Cup...Bao hilo lilifungwa dakika 29 tu toka mpira uanze...Bao lilifungwa na Clint Dempsey...Ghana walichangamka baadaye sana na Andrew Ayew alipokea mpira kutoka kiganja cha nyuma cha Asamoah Gyanbao na kupachika bao...Mwishoni wamarekani walianza kuishiwa pumzi lakini John Brooks aliweza kupata bao la ushindi kwa kichwa...Hichi ni kisasi ambacho Marekani wanalipa kutokana na kutolewa katika mechi za World Cup zilizopita na Ghana...Bofya hapa upate habari zaidi...

Monday, 16 June 2014

WORLD CUP 2014: GERMANY YAICHAPA PORTUGAL 4


Germany imetoka kuigaragaza Protugal vibaya sana kwa bao 4-0... Thomas Muller alipata hat-trick leo...Wajerunani walijipanga sana na badae Portugal wakawa wana hasira na hii ilionyesha baada ya Muller kufanyiwa foul na Pepe na alivyukuwa chini Pepe alikuja karibu na kumgonga kichwa mwenzake ndio refa akaona atoe red card...Coentrao pia aliumia na kutolewa nje kwahiyo Portugal na Ronaldo walikuwa hawana tena nguvu....Hii ni hat-trick ya kwanza kwenye World Cup hii ambayo imejaa magoli mengi...Portugal na Ronaldo wao itabidi wakajipange kama kweli wanataka kushinda...Germany waliongoza possession 54%-46%...

Sunday, 15 June 2014

WORLD CUP 2014: IVORY COAST YAANZA VYEMA KWA KUICHAPA JAPAN




Ivory Coast imekuwa nchi ya kwanza ya kutoka Africa kushinda game yake ya kwanza hapo Arena Pernambuco...Ivory Coast iliichapa Japan 2-1...Japan ndio walianza kufunga bao na aliyefunga ni Keisuke honda...kipindi cha kwanza kilikri kwa timu zote mbili kwani Japan walishambulia sana lango la Ivory Coast na badaae kibao kikageuka...


Kipindi cha kwanza Didier drogba alikuwa benchi na alipoingia tu game ikabadilika na Ivory Coast ikapata mwamko mpya...Mbony alipachika bao baada ya cross kutoka kwa Serge Aurier dakika ya 64...Dakika 2 tu baadae Gervinho alipachika la pili...Hii ni mara ya 3 Ivory Coast wanacheza World Cup na hawajawahi kwenda mbele ya group stage...Bofya hapa upate habari zaidi....

Saturday, 14 June 2014

WORLD CUP 2014: COLOMBIA YAICHAPA GREECE


Colombia imepata points 3 za uhakika baada ya kuichapa Greece mabao 3-0...Pablo Armero wa kutoka Napoli ambae yuko West Ham kwa mkopo ndio aliye pachika la kwanza mwanzoni...


Gutierrez ambae ni forward aliyechukua nafasi ya Ramadel Falcao aliweza kupata bao la 2 baada ya kona kutoka kwa James Rodriguez...Huyo Rodriguez aliweza kufunga la 3 dakika za nyingeza...Usikuose mechi ya Italy na England badae usiku huu...

NBA: MICHAEL JORDAN SASA NI BILLIONAIRE


Michael Jordan  sasa ni billionaire...Jordan ambae alikuwa MVP mara 5 na aliwahi kushinda ligi ya NBA mara 6 bila kusahau medali 2 za dhahabu za Olympics sasa amekuwa billionaire...Jordan sasa amekuwa mwanamichezo tajiri kuliko wote duniani na pia amekuwa mwanamichezo wa kwanza katika historia kufikia ubillionaire...Jordan ameweza kuwa billionaire kutokana na kuongeza umiliki wake katika timu ya NBA ya Hornets (zamani ilikuwa Bobcats)...Jordan ameongeza umiliki wake kutoka 80% mpaka 89.5%...


Jordan sasa ni mwanamichezo tajiri kuliko wote na ameweka rekodi ya kuwa mwanamichezo billionaire wa kwanza katika historia ya michezo...Jordan alinunua shares Hornets mwaka 2006 na badae akamnunua mmiliki Robert Johnson kwa dola millioni 175 na kuwa mmiliki wa timu wa ya Hornets...Bofya hapa upate habari zaidi kutoka Forbes.com


WORLD CUP 2014: NETHERLANDS YAIGARAGAZA VIBAYA SPAIN



Netherlands wameshangaza dunia kwa akufanya kitu ambacho hakijafanywa kwa kuchapa mabingwa watetezi kwa mabao 5 - 1...Spain ndio walioanza kuona lango kutokana na penalty aliyefunga Xabi Alonzo dakika ya 27...Robin Van Persie alichangamka na kuchapa kichwa cha kurukia kabla ya half-time...



Muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha 2 Arjen Robben aliwaweka Netherlands mbele...Free-kick kutoka kwa Wesley Sneijder ilimkuta Stefan de Vrij na kuandika bao la 3...Van Persie alimtoka kipa dakika ya 72 na kuandika bao la 4 ubaoni...Robben akapachika bao la mwisho dakika ya 80 kwa juhudi zake mwenyewe...



Spain mara ya mwisho kuchapwa 5 ilikuwa mwaka 1963...Bofya hapa upate habari zaidi....

Friday, 13 June 2014

WORLD CUP 2014: CAMEROON YACHPWA NA MEXICO



Cameroon imeanza vibaya michuano ya Wold Cup baada ya kuchapwa na Mexico bao 1 kwa 0 hapo Estadios des Dunas katika mji wa Natal...Mechi ya leo ilichezwa wakati mvua yingi nikinyesha mwanzo mwisho...



Cameroon ikiongozwa na Samuel Eto ilianza kwa kushambuliwa sana na Mexico na kukoswa mara nyingi kwani mshika kibendera alikuwa anawadaka Mexico kwa kuotea mara nyingi na pia kuna wakati refa aliwaonea Mexico mara 2...Cameroon walijitahi kuamka na kuwapelekea mpira Mexico lakini ilikuwa ngumu...Pia kulikuwa na rafu nyingi lakini refa alikuwa hatoi kadi kabisa mpaka mwishoni mwa kipindi cha pili...



Kipa wa Cameroon alijitahidi sana kupangua na kurukia mipira...Kuna kipindi Eto aligonga mwamba na akabaki anashangaa tu...Orilbe Peralta ndio aliwatoa Mexico kwa bao ambalo lilisababishwa na mabeki wa Cameroon kulala...Benoit Assou-Ekotto ndio mchezaji aliyejituma sana game ya leo...Bofya hapa usome zaidi...

NBA: SPURS YAIGARAGAZA MIAMI HEAT TENA

 
Tony Parker akikimbiza mpira

Maji shingoni kwa Miami Heat baada ya kupata kichapo kikali tena kwao na San Antonio Spurs 107-86...Mabingwa watetezi Miami wanaonekana kushindwa kumudu game ya Spurs na wako karibu kutolewa...Dwane Wade hakuisaidia timu yake kwani alipata point 1 kati ya 10 vipindi vitatu na alimaliza game na points 10 tu...LeBron james alijaribu lakini hakufu dafu kwa Tony Parker na wenzake...James alipata points 29 na rebound 8...Kawhi Leornrd alipata points 20 na rebound 14...Kazi ipo game 5 itakuwa Jumapili usiku...Usikose...Bofya hapa upate habari zaidi....

WORLD CUP 2014: WADAU KUTOKA TANZANIA WATUWAKILISHA VYEMA

 
Anthony Mark (kushoto) akiwa na
mdau mwenzake wakiwakilisha Tanzania

World Cup 2014 watu wengi wamepata nafasi ya kwenda na kuhudhuria michuano hiyo mikubwa sana duniani.

WORLD CUP 2014: BRAZIL YASHINDA 3-1 KWA SHIDA

 
Timu zikiingia uwanjani na watoto

Brazil ilifanikiwa kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Croatia 3-1 katika uwanja wa Arena de Sao Paulo...Croatia ndio walianza kupata goli la bure baada ya kusaidiwa na Marcelo ambae alijifunga dakika ya 11...Dogo Neymar alisawazisha dakika ya 29...Croatia walikuwa wanacheza mpira wa uhakuka na Brazil walipoteza utaalam wao mwanzoni lakini waliupata baadae...Kocha wa Croatia Niko Kovac alichukizwa sana na maamuzi yaliyo kuwa yanatolewa na mwamuzi kutoka Japan Yuishi Nichimura...Mnamo dakika ya 70 Kovac alikasirika tena baada ya huyo refa kutoa penalty ya bure kabisa...
 
Neymar akishangilia goli...

Neymar ndio aliye piga penalty ambayo kipa aliifuata lakini ilikuwa na nguvu ikaingia nyavuni...Dogo Oscar alifunga goli zuri sana pekeyake dakika za mwishoni...Ushindi ni muhimu na sasa Brazil wamepata pointi 3...Usikose kuangalia mechi za leo....Mexico vs. Cameroon, Spain vs. Netherlands na Chile vs. Australia... 

Thursday, 12 June 2014

WORLD CUP 2014: WACHEZAJI WAKIINGIA BRAZIL

Timu ya Costa Rica

Timu ya Honduras

Timu ya Ecuador

Messi na timu yake ya Argentina

Luis Suarez akiongea na Diego Lugano (Timu ya Uruguay) wakiwasili Brazil

Timu ya Ubelgiji ikiwa ndio imetua Brazil

WORLD CUP 2014: RATIBA YA WORLD CUP


Pata ratiba ya World Cup 2014 (Muda wa East Africa)...Mechi zinaanza leo na mechi ya kwanza ni kati ya Brazil na Croatia saa 5 usiku...


12-6-2014
23:00 Croatia v Brazil


13-6-2014
19:00 Cameroon v mexico
22:00 Holand v Spain
01:00 Chile v Australia


14-6-2014
19:00 Colombia v Greece
22:00 C.Rica v Aruguay
01:00 England v Italy
04:00 Japan v Cote d Voire


15-6-2014
19:00 Switzerland v Ecuador
22:00 France v Honduras
01:00 Argentina v Bosnia


16-6-2014
19:00 German v Portugal
22:00 Iran v Nigeria
01:00 Ghana V USA


17-6-2014
19:00 Belgium v Algeria
22:00 Mexico v Brazil
01:00 Rusia v Korea


18-6-2014
19:00 Holand v Australia
22:00 Chile v Spain
01:00 Cameron v Croatia


19-6-2014
19:00 Cote devir v Colombia
22:00 England v Portugal
01:00 Japan v Greece


20-6-2014
19:00 C.Rica v Italy
22:00 Switzerland v France
01:00 Ecuador v Honduras


21-6-2014
19:00 Argentina v Iran
22:00 Ghana v German
01:00 Nigeria v Bosnia


22-6-2014
19:00 Belgium v Russia
22:00 korea v Algeria
01:00 Portugal v USA


23-6-2014
19:00 Chile v Holland
19:00 Australian v Spain
23:00 Cameron v Brazil
23:00 Croatia v Mexico


24-6-2014
19:00 Italy v Greece
19:00 C.rica v England
23:00 Colombia v Japan
23:00 Greece v Cote d' Voire


25-6-2014
19:00 Argentina v Nigeria
19:00 Bosnia v Iran
23:00 Switzerland v Honduras
23:00 Ecuador v France


26-6-2014
19:00 Ghana v Portugal
19:00 USA v German
23:00 Belgium v Korea
23:00 Algeria v Russia

WORLD CUP 2014: LEO NDIO KOMBE LA DUNIA LINAANZA! USIKOSEEEE!!!!!



Leo ndio leo! Kombe la dunia litaanza leo kwa sherehe kubwa ya ufunguzi na badae kutakuwa na mechi ya kwanza kati ya wenyeji Brazil na Croatia...Mechi itaanza saa 5 kamili usiku...Usikose!!!! Timu 32 za nchi mbalimbali zitachuana mpaka apatikane bingwa July 13...Brazil haijawahi kufungwa mechi yao ya kwanza...Kazi ipo...Pamoja na matatizo ya hapa na pale tunatarajia World Cup itakuwa safi tu...Usikose kuangalia!!!