Tuesday, 28 June 2016

EURO 2016: ITALY YAWAPELEKA SHULE SPAIN


Italy waonyesha Ulimwengu kuwa mpira hauhitaji mbwewe wa chenga nyingi ila ni ufundi wa hali ya juu sana na akili ya ziada tu...Spain ilichapwa na Italy bila ubishi tena Spain wamepata somo zuri sana na inabidi wawashukuru sana Italy...


Italy ilishinda mechi ya jana 2-0 na mabao yalitoka kwa Giorgio Chiellini dakika ya 33 na Graziano Pelle dakika ya 90+1...


Kuna gazeti moja huko Spain liliandina 'The End' au 'Mwisho' kuashiria mwisho wa Spain...Spain wameanza kupoteza dira na inabidi waanze kujipangamaana kuna vitimu vidogo lakini hatari sana siku hizi...


Kocha wa Italy ambae anahamia Chelsea, Antonio Conte, ni kocha mzuri ambae aleweza kuwachapa Belgium na Spain kwenye michuani ya Euro...Ingawa anavituko uwanjani kama Jose Mourinho lakini ni kocha makini sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

EURO 2016: ROY HODGSON AMEACHIA NGAZI BAADA YA KICHAPO CHA ICELAND


Kocha wa timu ya England, Roy Hodgson, ameona isiwe tabu maana timu ya England hasara tupu...Hodgson amesema anaondoka wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchapwa na Iceland...


Kocha huyo amesema makocha wasaidizi Ray Lewington na Gary Neville na wataondoka...


England wako kwenye hali mbaya sana kwenye timu ya taifa na nchi baada ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) hali ambayo imesababisha pesa yao kushuka sana dhidi ya dola...Bofya hapa upate habari zaidi.

EURO 2016: EDEN HAZARD AFUNGA BAO KALI SANA HUKU BELGIUM WAKIIRARUA HUNGARY


Bao la Eden Hazard nyota wa Chelsea FC limezua gumzo kwani ni kati ya magoli bora Euro 2016...Hazard alikatizia kutoka kushoto na kuwapita wachezaji wawili na kupachika bao sa kabisa...Belgium imemewachapa hungary 4-0 na sasa itakutana na Wales robo fainali...

EURO 2016: ENGLAND YACHAPWA NA NCHI NDOGO YA ICELAND


England wameaibishwa na Iceland kwa kutolewa nje ya michuano ya Euro 2016...


Iceland ni ka timu kadogo ambako wachezaji wake hawana hata pesa na wengine wanacheza mpira kwa msimu tu maana wana kazi nyingine zakufanya lakini wamefanikiwa kuwatoa England na kelele zao...


Iceland inawatu takriban 330,000 na timu ni namba 34 duniani...England ni timu ambayo imejengwa kwa makelele na kujisifu bila kuwa na mantiki yoyote...


Iceland ndio waliocheza vizuri kuliko England na kweli walistahili ushindi...

Wameshinda 2-1 na mabao ya Iceland yalitoka kwa nyota Sigurdsson dakika ya 6 na Sigthorson dakika ya 18...


Rooney ndie aliyepata bao pekee la England dakika ya 4 kwa tuta...


Iceland watakutana na France ndani ya Stade de France Jumamosi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 27 June 2016

COPA AMERICA: ALEXIS SANCHEZ ASHINDA GOLDEN BALL


Nyota wa timu yaArsenal, Alexis Sanchez, amekuwa mchezaji bora wa Copa America...Sanchez ameshinda Golden Ball baada ya kuwachapa Argentina 4-2 kwenye matuta na kuchukua ubingwa wa Copa America...Goli kipa Claudio Bravo amechukua Golden Glove...Bofya hapa upate habari zaidi.

EURO 2016: RATIBA YA MECHI ZALEO (GMT)

MONDAY 27TH JUNE 2016

BREAKING NEWS: LIONEL MESSI ANASTAAFU BAADA YA ARGENTINA KUCHAPWA NA CHILE


Habari mpasuko zilizoingia Max Sports hivi punde ni kuwa Lionel Messi ametangaza kutoichezea Argentina tena...Baada ya Argentina kuchapwa na Chile Copa America Messi alionekana kuchukizwa na kichapo hicho na kuwaambia waandishi wa habari anachana na mpira wa kimata...Habari zaidizinakuja....

Sunday, 26 June 2016

BOXING: ANTHONY JOSHUA AMLAZA BREAZEALE ROUND YA 7


Anthony Joshua amebakiza mkanda wake wa IBF baada ya kumtandika Mmarekani Dominic Breazeale ndani ya O2 Arena...Breazeale alidondoshwa round ya 7 na ni mara ya kwanza anachezea kichapo...


Joshua toka mwanzo alikuwa hatari lakini Breazeale alipokea makonde mpaka Joshua round ya 6 akaanza kukasirika...Round ya 7 Joshua alianza kurusha makonde ya kutetea kabisa na ngumi yake ya kushoto ikamshusha Breazeale chini...Sasa Joshua yuko tayari kuzichapa na watu wenye uzoefu zaidi...


Joshua amesema angependa kumuenzi Muhammad Ali kwa kuzichapa barani Africa nchini ya Nigeria au Ghana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 25 June 2016

SOUTHAMPTON: NATHAN REDMOND ASAINI MKATABA NA SOUTHAMPTON


Nathan REDMOND ameshinda mkataba wa miaka 5 akitokea Norwich...England U 21 ni winger mzuri na amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Southampton baada ya ligi kumalizika...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 24 June 2016

LEBRON JAMES: NITABAKIA CLEVELAND CAVALIERS



LeBron James na timu yake ya Cleveland Cavaliers waliochukia ubingwa wa NBA hivi juzi tu wmerudi nyumbani na kupokelewa kama wafalme...



Toka mwaka 1964 mji wa Cleveland haujawahi kushinda kitu chochote...



Katika kusherehekea ushindi LeBron James au King James kwa jina lingine amesema bado ataendelea kuwepo na timu ya Cleveland...Bofya hapa upate habari zaidi.








NEW YORK KNICKS: RAIS WA KNICKS PHIL JACKSON ANAMTAKA KEVIN DURANT


Baada ya kumchukua Derek Rose kutoka Chicago Bulls Rais wa New York Knicks ,Phil Jackson, amesema anamfukuzia Kevin Durant...Jackson anaamini Rose na Durant wataibadilisha kabisa New York Knicks timu ambayo zamani ilikuwa inawika sana...


Uzoefu wa Phil Jackson ni mkubwa sana na  akimpata Durant basi mambo yao yatanyooka...Bofya hapa upate habari zaidi.

VICTOR WANYAMA: TOTTENHAM WAMCHUKUA WANYAMA


Victor Wanyama amesaini mkataba na Tottenham wa miaka 5...Dau la Wanyama ni Pounds Milioni 11...Wanyama mwenye umri wa miaka 24 atakutana tena na kocha wake wa Saints, Mauricio Pochettino, ndani ya White Hart Lane...Wanyama amesema ni vigumu kuaga timu ambayo imempa nafasi mkeya wa kwanza kucheza Premier League...Bofya hapa upate habari zaidi.

TOTTENHAM HOTSPURS: WAZEE WA NORTH LONDON KARIBU KUNYAKUA WANYAMA


Tottenham bado wanaendela na mazungumzo na Southampton kuhusu Victor Wanyama...Du la Wanyama ni Pounds za Englang 11 milioni...Kenya International amebakiza mwaka 1 kwenye mkataba wake...Southampton walitoa Pound 12 milioni kumchukua Wanyama kutoka Celtic...Bofya hapa upate habari zaidi.

LIVERPOOL: LIVERPOOL WANATAKA KUMALIZA BIASHARA MAPEMA YA KUMCHUKUA SEDIO MANE


Liverpool FC karibu wanamalizia deal ya kumchukua winger Sadio Mane kutoka Southampton kwa dau la Pounds milioni 30...

FC BARCELONA: BARCELONA YACHANGIA ALISILIMIA 1.5 YA PATO LA TAIFA


FC Barcelona yachangia asilimia 1.5 katika pato la Jiji la Barcelona...Katika report iliyotolewa na kampuni ya Deloitte inasema timu ya Barcelona inachangia sana hasa katika kuajiri watu, utalii na mapato ya kodi...Mchango wa timu ya Barcelona ni Euro 906 milioni ambayo ni asilimia 1.5 ya biashara yote jijini Barcelona katika mwaka 2014-2015...


Deloitte wamesema kwa upande wa ajira tu Barcelona imetoa ajira kwa watu 16, 620...Kwa upande wa utalii asilimia 6 ya watalii wanaoingia Barcelona wanasema ni kwasababu ya timu ya Barcelona...Bofya hapa upate habari zaidi.

NBA: DEREK ROSE TO BE TRADED AGAINST THREE PLAYERS

Derrick Rose


New York Knicks and Chicago Bulls reach a deal whereby Derrick Rose will move to Knicks.. Three players will move to Bulls.

Thursday, 23 June 2016

CRICKET: CAPTAIN WA ZAMANI ANIL KUMBLE AMEKUWA KOCHA MPYA INDIA


India imemchagua mchezaji na Captain wa zamani wa Cricket, Anil Kumble, kuwa kocha mpya wa timu ya India...Kumble hana uzoefu wa kimataifa lakini anaongoza kwa wickets nyingi....Kumble ana wickets 619 katika mechi 132...India walikuwa hawana kocha toka Duncan Fletcher alivyoondoka World Cup ya mwaka 2015...



Alivyo staafu alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya International Cricket Council (ICC)...Bofya hapa upate habari zaidi.

LEICESTER CITY FC: VARDY AMEAMUA KUBAKIA LEICESTER


Mshambuliaji mashuhuri wa Leiceester na timu ya taifa ya England, Jamie Vardy, amesaini mkataba mpya wa miaka 4 na kuondoa gumzo la wengi baada ya club ya Arsenal kutangaza nia ya kumchukua mchezaji huyo...Msemaji wa club ya Leicester alisema "Leicester City pamoja na mwakiishi wake wamekubali kuongeza mkataba baina ya mshambuliaji huyo na mabingwa wa ligi ya England" Aidha aliongeza na kusema "natumanini mkataba huo utamaliza gumzo lililojengeka la Vardy kuhamia Arsenal baada ya club hiyo kutangaza nia"...


Vardy ambae yuko nchini France na timu ya taifa ya England, hatosema lolotehadi mashindano hayo yatakapoisha...England inajifua kujiweka tayari kupambana na Iceland...

EURO 2016: MPANGILIO WA MECHI ZA 16 BORA


EURO 2016: RATIBA YA 16 BORA (GMT)

SATURDAY 25TH JUNE 2016

ROUND OF 16

  • Switzerland14:00Poland
  • Wales17:00Northern Ireland
  • Croatia20:00Portugal

COPA AMERICA: CHILE NDANI YA FAINALI YA COPA AMERICA


Chile imewalaza Colombia 2-0 ndani ya uwanja uliojaa maji kutokana na mvua kubwa sana iliyosababisha mechi kusimamishwa...Mechi iliahirishwa masaa 2 ndani ya uwanja wa Chicago Bears...Fainali ya mwaka huu inajirudia tena kwani mwaka jana Chile walifanikiwa kushinda kupitia matuta...Colombia sasa watacheza na USA kutafuta mshindi ya 3...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday, 22 June 2016

ARUSHA OPEN GOLF CHAMPIONSHIP: MADINA IDDI AWIKA ARUSHA OPEN




Madina Iddi akicheza na handicap 3 ameshinda michuano mikubwa ya golf jijini Arusha...Michuano hiyo ya Arusha Open Golf Championship iliyofanyika katika viwanja vya Arusha Gymkhana Golf Club ilikuwa na vipaji vingi lakini hatimae Madina aliibuka mshindi...Madina alipiga mikwaju 146 katika mashimo 36...


Amesema ushindi wake ulikuja kwa kufanya mazoezi sana na kujituma...Neema Olomi nae wa Arusha Gymkhana Club alikuwa wa 2 na Leah Nicholas...Bofya hapa upate habari zaidi.

RIHANA: NYOTA WA MCHEZO WA NGUMI ZA UFC CONOR MCGREGORY AMEFURAHI KUKUTANA NA RIHANA NDANI YA DUBLIN


Baada ya concert ya mwanamuziki maarufu sana duniani Rihanna nchini Ireland jiji la Dublin alikutana na nyota wa ngumi za UFC Conor McGregory...McGregor aliacha tizi kali la kujifua ngumi na kukutana na Rihanna...


Pia McGregor alihudhuria concert ya Rihanna ya Album ya ANTI na mpenzi wake Dee Devlin...


Rihanna alifurahi kukutana na McGregor na kumshukuru kwa maneno mazuri...Bofya hapa upate habari zaidi.

TP MAZEMBE: STICKER GIVEN SINGULUMA HATOCHEZA MECHI DHIDI YA YOUNG AFRICANS


mazembe watakuwa bila striker wao Zambian International, Given Singuluma, kutokana na kutenguka kwa mkono...Singuluma alitenguka katika mechi ya TP Mazembe na Madeama SC ya Ghana...Singuluma atauwa nje kwa muda wa wiki 3 mpaka 6...TP Mazembe walianza michano ya makundi vizuri kwa kuwachala Madeama SC 3-1 ndani ya Lubumbashi...Bofya hapa upate habari zaidi.

EURO 2016: TIMU AMBAZO NIMEINGIA 16 BORA MPAKA SASA


Group A: France and Switzerland

Group B: Wales and England

Group C: Germany and Poland

Group D: Croatia and Spain

Group E: Italy

Group F: Hungary

Best third-placed teams: Slovakia and Northern Ireland