Wednesday, 21 May 2014

F1: BINGWA WA F1 WA ZAMANI AFARIKI


Sir Jack Brabham amefariki akiwa na umri wa miaka 88...Sir Brabham alikuwa bingwa wa mashindano ya F1 mara tatu miaka ya 1959, 1960 na 1966...Alikuwa ni mtu pekee aliyewahi kushinda mashindano haya makubwa kwa kutumia gari aliyoitengeneza mwenyewe...


Mpaka leo hakuna mtu ambae amedesign, ametengeneza na kuendesha gari yake na kushinda...Hiyo gari ilikuwa na engine nyuma na iliiywa BT-19...


Sir Brabham anatokea Australia na huko ndio alipoanza kuendesha magari ya mashindano baada ya kuacha kazi jeshi la anga akiwa kama fundi wa ndege...Wadau wa F1 duniani wamesikitika na habari hizi...Max Sports inamtakia apumzike kwa amani...Bofya usome zaidi hapa...

AFRICA YOUTH GAMES: TANZANIA YAPELEKA KIKOSI IMARA CHA VIJANA


Mashindano ya 2 ya vijana Africa yatafanyika Gabarone, Botswana, kuanzia Alhamisi...Tanzania tumepelekeka kikosi imasa sana ambacho kitaingia kwenye mashindano mbali mbali kama soka, riadha na swimming...Afisa wa TFF bwana Boniface Wambura amesema kikosi cha U-15 au wachezaji chini ya umri wa miaka 15 kiko imara sana na kiko tayari kupambana katika haya mashindano...Pia haya mashindano yanachukuliwa kama jaribio la mwisho ambalo litapelewa vijna kwenye Olympics za vijana huko Nanjing China mwaka huu....Bofya hapa upate habari zaidi...

NBA: LeBRON NA HEAT WASHINDA GAME 2 YA FAINALI YA MASHARIKI


LeBron James ameweza kuisaidia timu yake iweze kuichapa Indiana Pacers kwenye game ya 2 ya fainali za conference ya mashriki...Game ilimalizika 87-83...Kuna wakati Heat walikuwa juu 12-2 baada ya James kudumbukiza point 6...James alipata pointi 22 na 12 kati ya hizo zilikuwa robo ya mwisho wa mchezo...Wade alipata pointi 23...Kutoka Pacers Lance Stephenson alipata pointi 25 na Paul George pointi 14...Sasa timu ziko sare na game 3 itkuwa jumamosi huko Mimi...Usikose kuicheki....

Tuesday, 20 May 2014

DAR ES SALAAM GYMKHANA CLUB OPEN BONANZA!


Karibuni wote kwenye Bonanza hii kubwa hapo Gymkhana Club jumamosi hii tarehe 24 May!!!! Kiingilio ni bure kabisa!!! Kutakuwa na mashindano mbali mbali ya michezo mbali mbali!!! Sponsors mnakaribishwa sana mshiriki katika hii Bonanza ya ainayake na yakipekee kutokea Dar es Dalaam!!!


TENNIS: WENGI WAJITOKEZA KWENYE MSIBA WA BALTACHA



Watu zaidi ya 300 wamehudhuria msiba na mazishi ya aliyekuwa bingwa wa tennis Uingereza kipindi cha nyuma Elena Baltacha...Baltacha alifariki akiwa na umri wa miaka 30 kutokana na Cancer ya Ini...

Bingwa wa tennis Uingereza Laura Robson

Msiba huu ulikuwa huko Ipswich huko Uingereza ambako alianzisha Academy ya watoto ya tennis...

Tim Henman bingwa wa zamani wa tennis Uingereza

wengine walikuhudhuria walikuwa Tim Henman bingwa wa tennis wa Uingereza na namba 1 wa tennis wa sasa Uingereza Laura Robson...Pata habari zaidi hapa...

LA LIGA: LUIS ENRIQUE KOCHA MPYA BARCA


Barcelona imepata kocha mpya...Luis Enrique kutoka Celta Vigo ambayo ilimaliza ya 9 kwenye ligi ya Spain....Luis sio mgeni kwa hii club ya Barca kwani toka 2008 mpaka 2011 alikuwa kocha wa timu B ya Barca...Pia aliwahi kuwa mchezaji wa Barca kipindi cha nyuma....Luis anachukua nafasi ya kocha Gerardo Martino baaada ya kukosa ubingwa mechi ya mwisho ambayo walicheza na mabingwa Atletico Madrid...Bofya hapa upate habari zaidi...

Thursday, 15 May 2014

NBA: LeBRON NA WENZAKE WAITOA NETS


LeBron James amesaidia sana timu yake kuitoa Brooklyn Nets kwenye series katika mechi ngumu ya Game 5 ya michuano ya playoffs...Miami Heat walishinda 96-94...LeBron ambae alipata pointi 29 kwenye hii game alicheza sana defense na kumkabili NBA All-star wa Nets Joe Johnson...Johnson alipata wakati mgumu sana na hata kufanya makosa madogo madogo...Wade na Bosh nao walisaidia sana na Wade alipata career high point 28 kwenye playoffs hizi..Bofya hapa upate habari zaidi....

ITALIAN OPEN: ROGER FEDERER ACHAPWA


Bingwa wa zamani wa tennis amechapwa 1-6, 6-3, 7-6 (8-6) na Jeremy Chardy huko Rome Italy....Kichapo hiki kinakuja baada ya kupumzika kidogo kutokana na mke wake kujifungua mapacha...Ilikuwa asicheze lakini mke wake alimlazimisha na akakubali...Kuna wakati seti ya mwisho ilikuwa ashinde tie-break lakini alizidiwa na forehand kali ya Jeremy...Djokovic nae karibu achapwe lakini alijitahidi na kushinda...Wengine walioshinda ni Thomas Berdych, Serena Williams na Maria Sharapova...Bofya hapa upate habari zaidi...

EUROPA LEAGUE: SEVILLA BINGWA


Sevilla ni bingwa Europa League...Sevilla wamefanikiwa kuwatoa Benfica kwenye mechi kali sana iliyufanyika huko Turin...Mpaka half-time ilikuwa na mambo yaliendelea hivyo hivyo mpaka mwisho wa muda wa kawaida...Muda ukaongezwa na hakuna aliyefanikiwa kupachika bao...Benfica ilikuwa wawe mbele mwishoni lakini walichemsha...Bingwa sasa ilikuwa apatikane kwa matuta...Kipa wa Sevilla ndio alikuwa staa baada ya kuwakatalia Oscar Cardozo na Rodrigo...Stephane Mbia kutoka QPR kwa mkopo alikuwa makini na kupachika bao...Kevin Gameiro ndio aliepachika bao la ushindi...Bofya hapa upate habari zaidi...

Wednesday, 14 May 2014

WORLD CUP 2014: BRAZUCA MPIRA MPYA KUTOKA ADIDAS


Brazuca ni mpira mpya ambao utakuwa unatumika huko Brazil kwenye World Cup muda si mrefu....Brazuca ni mpira wa 12 wa World Cup kutengenezwa na Adidas...Adidas walipata wakati mgumu sana World Cup iliyopita huko South Africa baada ya mpira wao ambao ulijulikana kwa jina la Jabulani ulipigwa vita sana kutokana na kubadilisha mwendo ukiwa angani...


Brazuca sasa umeimarisha sana na mkurugenzi wa mpira wa miguu wa Adidas amesema kuwa majaribio yameonyesha mpira uko safi na unafuata unapipigwa...Brazuka umetengenezwa na vinundu vidogo vingi ili kusaidia mwendo wake ukiwa hewani...Bofya hapa upate habari zaidi za mpira mpya kabisa Brazuca.....

WORLD CUP 2014: UFARANSA YATAJA KIKOSI NA NASRI HAYUPO


Didier Deschamps ametaja kikosi chake cha World Cup...Katika hicho kikosi Samir Nasri ametemwa pamoja na Gael Clichy...Kocha huyo anasema Nasri ni mzuri akiwa na Man City lakini sio mzuri akichezea timu ya Ufaransa...Wachezaji 23 wamechaguliwa na kati ya hao 9 wanachezea ligi ya Uingereza...Wachezaji watatu wanatokea Arsenal FC...Hebu soma hiyo squad hapo chini...


Goalkeepers: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Mickael Landreau (Bastia).
Defenders: Mathieu Debuchy (Newcastle), Lucas Digne (Paris St-Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny, Bacary Sagna (both Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid).
Midfielders: Yohan Cabaye, Blaise Matuidi (both Paris St-Germain), Clement Grenier (Lyon), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille).
Forwards: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newastle, on loan from QPR), Franck Ribery (Bayern Munich), Stephane Ruffier (Monaco).
Standby: Loic Perrin (St Etienne), Maxime Gonalons, Alexandre Lacazette (both Lyon), Morgan Schneiderlin (Southampton), Benoit Tremoulinas (Dynamo Kiev), Remy Cabella (Montpellier).

EPL: TIM SHERWOOD SACKED


Tim Sherwood has been sacked by Tottenham after a poor season.

Tuesday, 13 May 2014

CONGO PLAYOFFS: WATU 15 WAMEPOTEZA MAISHA KATIKA MECHI YA ASV NA TP MAZEMBE


Ulimwengu wa soka wa Congo uko katika majonzi baada ya watu 15 kupoteza maisha na watu 21 kujeruhiwa huko Kinshasa, Demokrasia ya Congo....Ugomvi ulianza wakati mechi inaendelea na Tout Puissant Mazembe wakiwa mbele kwa bao moja mashabiki wa pande zote mbili wakaanza fujo na kurusha vitu uwanjani wakitaka refa asimamishe mchezo...Baada ya hapo polisi walirusha mabomu ya machozi na kuwachanganya mashabiki ndipo watu wakaanza kukanyagana wakitafuta pakwenda...Hizi timu 2 ni timu maarufu sana huko Congo...ASV ni timu maarufu sana huko Kinshasa na Tout Puissant Mazembe ni timu kubwa sana na mabingwa kutoka Lubumbashi na mmiliki wake ni tajiri sana na ni gavana wa jimbo la Katanga anaitwa Moise Katumbi...Timu hizi zikikutana lazima kuwe na msuguano na polisi wanaimarishwa kila wakikutana...Wachezaji wawili wa Tanzania nao pia wamenusurika kwenye vurugu hizo...Hao ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu...CAF kupitia mwenyekiti Hayatou amsema wamesikitika sana na hizi habari....Bofya usome zaidi hapa...

EPL: RIO FERDINAND KUONDOKA MANCHESTER UNITED


Rio Ferdinand beki machachari wa Manchester United anafunga virago muda si mrefu baada yakuitumikia timu ya Manchester United miaka 12...Ameamua kuondoka baada ya club kutompa mkataba mwingine...Aliombwa abaki kama balozi wa timu lakini ameamua kuondoka na kutafuta issue nyingine...Ferdinand amekaa Man U miaka 12 na kati ya hiyo amepata magoli 8 na ameingia uwanjani mara 454...Tweet kutoka club ya Man United #mufc inamshukuru kwa utumishi wake na inamtakia heri huko atapoenda...Bofya hapa upate habari zaidi..

Monday, 12 May 2014

WORLD CUP 2014: GHANA YATAJA KIKOSI CHAKE CHA AWALI




Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah, ametaja kikosi chake cha awali cha wachezaji 26 lakini atakipunguza mpaka 23...Watu wengine kama masupa staa John Mensah na Isaac Vorsah wametemwa na kuingizwa madogo wengine wakali...Michael Essien ameingizwa kwenye squad baada ya kukosa World Cup ya 2010 kutokana na kuumia...Dogo mmoja kutoka club moja ya Sweden, Helsingborg, David Accam amechaguliwa kuingia kwenye squad...Dogo mwingine kutola Leister City ambaye alizaliwa Ujerumani, Jeffrey Shlupp, pia ameingizwa kwenye squad...Ghana itaanza tizi kuanzia tarehe 20 na badae watasafiri kwenda Uholanzi kucheza na timu ya taifa ya Uholanzi katika mechi ya kirafiki...Squad ya Ghana hiyo hapo chini...

Goalkeepers: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars).
Defenders: Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege), Harrison Afful (Esperance), Jeffrey Schlupp (Leicester), John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Jerry Akaminko (Kisehirspor), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns).
Midfielders: Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan).
Strikers: Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux), David Accam (Helsingborg).

WORLD CUP 2014: ENGLAND YATAJA SQUAD




Kocha mkuu wa England hivi punde tu katoka kutangaza timu ya taifa ya England itakayo enda Brazil kwenye kombe la dunia...Amesema ametumia maamuzi magumu lakini ametoa kikosi safi cha wachezaji 23 ambao ni vijana zaidi...England wanaanza kampeni yao ya kuwania kombe la dunia na timu ya Italy huko Manaus tarehe 14 Juni pia badae watakutana na Uruguay na Costa Rica...Squad ya England hiyo hapo chini...



Goalkeepers: Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City).
Defenders: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Chris Smalling (Manchester United).
Midfielders: Ross Barkley (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Jack Wilshere (Arsenal).
Attackers: Rickie Lambert (Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).
Standby: John Ruddy (Norwich City), Jon Flanagan (Liverpool), John Stones (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Andy Carroll (West Ham United), Jermain Defoe (Toronto FC).

F1: LEWIS HAMILTON ASHINDA SPANISH GP


Lewis Hamilton alifanikiwa kushinda shindano lake la nne kwa kuchukua Spanish GP...Lewis alichukua nafasi ya kwanza kwenye grid na kona ya kwanza aliweza kuchomoka na kuwaacha mbali wenzake akiwemo dereva Nico Rosberg ambaye wako wote timu moja...


Hamilton aliongoza mwanzo mwisho lakini mwenzake Nico alimkaribia lakini hakuweza kumkamata...Nico likuwa wa 2 akifuatiwa na Ricciardo wa 3 na mwenzake kutoka Red Bull Sebastian Vettel alikuwa wa 4...


Vettel alitoka wa 15 kapambana hadi kamaliza wa 4...Bofya upate habari za f1 hapa...   

EPL: MANCHESTER CITY MABINGWA


Hatimaye kapatikana bingwa kwenye ligi inayofuatiliwa sana duniani ya English Premiership...Bingwa huyo ni Manchester City....Liverpool hawakuwa nyuma sana lakini walizidiwa na hawakuweza kutunza points zao...Manchester City kama mnavyokumbuka ilikuwa timu ambayo ilitumia pesa nyingi kusajili wachezaji miaka michache iliyopita na sasa imezaa matunda...


Mwafrika Yaya Toure ametokea kuwa mchezaji safi na makini na amewasaidia sana City kuutwaa ubingwa mwaka huu...Msimu huu ulikuwa mgumu sana kwa timu zote na ushindani ulikuwa mkubwa sana na sasa itabidi timu zikajipange upya kwa mshimu ujao...Max Sports na wadau tunawapa hongera Manchester City kwa kuwa mabingwa tena kwa mara ya 5...

NBA: CLIPPERS WATOKA NYUMA NA KUWASHANGAZA OKC



LA Clippers timu ambayo imekuwa kwenye vyombo vya habari sana msimu huu kwa uchezaji bora na mmiliki wao kutimuliwa kwenye shughuli zote za NBA wameshangaza mashabiki na wadau kwa kushinda game yao dhidi ya Oklahoma City 101-99...Game ilikuwa kali sana lakini nusu ya kwanza OKC waliweza kuwamudu Clippers hasa Russell Westbrook alikuwa moto akisaidiwa na MVP Kevin Durant ambaye alipata pointi 40 na Ibaka...


Kipindi cha pili kiliona OKC wakiongoza kwa pointi 22 lakini Blake Griffin aliweza kusaidia na kupunguza hiyo gap mpaka ikafikia pointi 10...Griffing alimaliza game akiwa na pointi 25 na rebounds 9...Clippers kupitia Darren Collison waliweza kupunguza gap mpaka pointi 1 dakika za mwisho...Darren alipata point 18 na 8 kati ya hizo zilikuja mwishini...Bofya hapa upate habari zaidi...

Saturday, 10 May 2014

EPL: RATIBA YA MECHI ZA KESHO

  
                          


                  Kick-off
Cardiff V Chelsea                    15:00
Fulham V Crystal Palace                15:00

Hull V Everton                15:00

Liverpool V Newcastle                15:00

Man City V West Ham                15:00

Norwich V Arsenal                15:00

Southampton V Man Utd                15:00

Sunderland V Swansea                15:00

Tottenham V Aston Villa                15:00

West Brom V Stoke                15:00

F1: MERCEDES 1 2 KATIKA PRACTICE YA MWISHO


Hivi punde tu Nico Rosberg na Lewis Hamilton wamemaliza qualifying practice ya mwisho wakiongoza grid ya kesho huko Spain...Lewis alikuwa mbele ya Alonzo wa Ferrari sekunde 0.432 ambaye amekuwa wa 3 akifuatiwa na Massa wa 4 na Grosjean wa 5...Bofya hapa upate habari zaidi....

F1: MSIMAMO WA MADEREVA MPAKA SASA

FIA Formula 1 Drivers' World Championship

Points zinazawadiwa kama ifuatavyo:

1st place - 25 points; 2nd -18; 3rd - 15; 4th -12; 5th - 10; 6th - 8; 7th - 6; 8th - 4; 9th - 2; 10th - 1.
 
DriverCountryTeamPoints
1 Nico Rosberg Ger Mercedes 79
2 Lewis Hamilton GB Mercedes 75
3 Fernando Alonso Spa Ferrari 41
4 Nico Hulkenberg Ger Force India 36
5 Sebastian Vettel Ger Red Bull 33
6 Daniel Ricciardo Aus Red Bull 24
7 Valtteri Bottas Fin Williams 24
8 Jenson Button GB McLaren 23
9 Kevin Magnussen Den McLaren 20
10 Sergio Perez Mex Force India 18
11 Felipe Massa Brz Williams 12
12 Kimi Raikkonen Fin Ferrari 11
13 Jean-Eric Vergne Fra Toro Rosso 4
14 Daniil Kvyat Rus Toro Rosso 4
15 Romain Grosjean Fra Lotus 0

NFL: TOP DRAFT PICK AENDA HOUSTON TEXAS

 

Katika kuchagua wachezaji wapya kutoka vyuo kikuu mbalimbali Houston Texas wamemchagua Jadeveon Clowney kuwa mchezaji wao na pia ni top draft pick...Clowney ni dogo mkali sana na anaumbo bonge ambaye ametokea chuo cha South Carolina...Texas walimruka offensive tackle mmoja anayetokea chuo cha Auburn anayeitwa Greg Robinson ambaye amechaguliwa na St. Luis Rams...Drat pick wa 3 ni Blake Bortles kutoka Central Florida na anachea nfasi ya quarterback...Soma zaidi hapa...

NBA: OKC YAISIMAMISHA CLIPPERS

 

Oklahoma City wameweza kuongoza na kuwa mbele 2-1 game 3 kati ya game 7 zinazotakiwa kuchezwa katika round ya pili ya Playoffs....OKC walishinda 188-112...MVP Kevin Durant alipata points 36 na wenzake wakina Ibaka points 20, Russell Westbrook points 23 na assists 13...Game ilikuwa ngumu sana mpaka robo ya mwisho OKC wakawa moto na Clippers defense ilibaki imechanganyikiwa....Kwa upande wa Clippers Blake Griffin alipata points 34 na Chris Paul alipataa points 21 na assists 16 pia mshindi wa 'sixth man' wa mwaka Jamal Crawford alipata points 20...Bofya hapa upate habari zaidi...

EPL: BRENDAN RODGERS ATABAKIA LIVEROOL


Liverpool wako mbioni kuandaa mkataba mpya wa kocha Brendan Rodgers....Rodgers ataweka saini mwishi wa msimu huu...Amesema hataki kuchanganya mambo na atangoja msimu uishe ndipo atatia saini mkatba mpya endapo utakuwa tayari...Rodgers ameisidia sana Liverpool kwa kuiimarisha na kuifanya iwe na nguvu ya kuwa bingwa....Sasa Liverpool wako chini ya Manchester City kwa pointi 2 wakielekea ukingoni mwa msimu...Bofya hapa upate habari hii zaidi....

Friday, 9 May 2014

WOMEN'S WORLD CUP QUALIFIER: ENGLAND YAICHAPA UKRAINE 4-0


England ilifanikiwa kuichapa Ukraine mabao 4-0...Ukraine nchi ambayo sasa inamatatizo makubwa ya kuigawa nchi haikuweza kufua dafu kwa timu ya wanawake ya England huko Shrewsbury Uingereza...England walipata shida sana dakina 40 za mwanzo lakini goli lilipatinana kutoka kwa mshambuliaji Natasha Dowie kwa kichwa safi kabisa...Baada ya hapo Eniola Aluko aliipatia bao England baada tu ya half-time..Dowie aliweza kupachika la 3 na Aluko alimalizia siku na bao la 4...Bofya hapa ufuatilia mambo ya qualifying  

NBA: MIAMI HEAT SASA WAKO MBELE 2-0


Miami Heat sasa wako mbele game 2 baada yakuizamisha tena Brooklyn Nets 94-82 katika game kali kwenye uwanja wa Heat...Nets walikuwa makini sana kurusha na kupata points mapema na waliongoza kwa muda mpaka LeBron na watu wake wakakaza buti na ilipifika half-time walikuwa wamepishana pointi 1...Kipindi cha 3 na cha 4 Miami walipandisha game yao na kutumia uzoefu zaidi katika kufunga na hivyo mipira ilikuwa inamkuta sana Ray Allen...Mwishoni Miami walikuwa mbele sana na wakawa wanajaribu kufunga lakini wanashindwa na hapo wanapata rebounds zote...LeBron akamalizia kwa kuiwahi clock mwishoni...Timu zote ziko safi lakini Net inabedi wajipange sana iliwaweze kushinda....

EPL: JOSE APIGWA FAINI


Kocha wa Chelsea FC, Jose Mourinho, amepigwa faini ya £10,000...Hii ni kutokana na kauli yake aliyetoa kwa refa wa mchezo kati ya Chelsea na Sunderland ambapo Chelsea ilifungwa 2-1...Mourinho anasema alienda kupongeza refa lakini baada ya hapo hali ya hewa ilichafuka kidogo...Hii ni faini ya pili nyingine ni £8,000 ambayo ameshindwa kuizuia ilikuwa  katika mechi ya Chelsea na Aston Vlla pia Chelsea walifungwa 1-0...Bofya upate habari zaidi...

Thursday, 8 May 2014

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
1Man City376383
2Liverpool375081
3Chelsea374379
4Arsenal372576
5Everton372069
6Tottenham37166
7Man Utd372163
8Southampton37855
9Newcastle37-1549
10Stoke37-847
11Crystal Palace37-1544
12West Ham37-940
13Swansea37-239
14Sunderland37-1738
15Aston Villa37-1938
16Hull37-1337
17West Brom37-1536
18Norwich37-3233
19Fulham37-4531
20Cardiff37-4130