Sunday, 27 September 2015

RUGBY WORLD CUP: CAPTAIN WA SOUTH AFRICA NJE



Captain wa timu ya taifa ya Raga ya South Afrika, Jean De Villiers, hatoweza kucheza tena wenye World Cup kutokana na kuvunjika mfupa unaoshika meno...Captain huyo aliumia kwenye mechi yao dhidi ya Samoa ambayo walishinda 46-6...Ni pigo kubwa sana kwa Springbok lakini wamejipanga kuendelea na mapambano bila De Villiers...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: LEWIS HAMILTON BINGWA JAPAN



Lewis Hamilton kwa mara nyingine awika Suzuka...Hamilton alipambana na mwenzake Nico kwenye kona 2 za mwanzo na kumfanya Nico asogee pembeni ndipo akampita na kuongoza Japanese GP...


Hamilton sasa kashinda mashindano 8 kati ya mashindano 14 na anaongoza kwa pointi 48 na zimebaki pointi 125 za kubeba katika michuano iliyobaki...


Hamilton amefikia rekodi ya mkongwe wa mashindano ya F1 marehemu Aryton Senna ya ushindi wa michuano 41...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 25 September 2015

BUNDESLIGA: PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG AWEKA REKODI MPYA



Forward wa Borrusia Dortmung, Pierre-Emerick Aubameyang, ameweka rekodi mpya kwenye ligi kubwa ya Ujerumani ya Bundesliga...Aubameyang amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika mechi zote 6 za mwanzo...


Kwa sasa ameshafunga mabao katika mechi 8 mfululizo ukichanganya na za mshimu uliopita...Bofya hapa upate habari zaidi.

BASKETBALL: BBALL KITAA YAWAKARIBISHA MALAWI



Bball Kitaa wameandaa mechi 2 kali sana kwa kuwaalika wamalawi kuja kucheza na timu zetu za bongo...Team ya Malawi inaitwa Reject Basketball Club itachuana kesho na Mbezi Beach Club (Western Zone One) kwenye Bball Kitaa park karibu na Gymkhana Club na Jumapili watachuana na Jogoo...Coordinator wa Bball Kitaa, Lawrence Karabani, amesema watu wajitokeze kwa wingi kushuhudia mechi hizo kali kwani Reject ni kati ya timu kali sana huko Malawi...Bofya hapa upate hanari zaidi.

Thursday, 24 September 2015

CHELSEA: EVA ASEPA NA ANATAKA KUFUNGUA MASHTAKA



Dokta wa Chelsea, Eva Carneiro, ambae alishushwa cheo baada ya kuwakiwa na Jose Mourinho kwenye mechi dhidi ya Swansea ameamua kuachia ngazi...Pamoja na kuachia ngazi anafikiria kufungua mashtaka dhidi ya club yake kutokana na issue ya mkataba na kuvunjiwa heshima...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 22 September 2015

TP MAZEMBE: MBWANA SAMATTA WA TANZANIA AWIKA



Mbwana Samatta mtazania ambae anachezea timu kubwa sana ya TP Mazembe anafanya vizuri sana...Alipata hat-trick dhidi ya Moghreb ya Morocco na kuipeleka TP Mazembe nusu fainali ya Africa's Champion League...Samatta anasema anafikiria kucheza soka Ulaya kwani watanzania wachache wameweza kujaribu kucheza Ulaya...Mwaka 2010 Haruna Moshi aliichezea timu ya Gefle IF ambayo iko kwenye premier league ya Sweden na Renatus Njohole alijitahidi sana akiwa na timu ya Uswiss ya premiership ya Yverdon Sport kati ya mwaka 1999 mpaka 2001...Samatta ambae alitokea Simba miaka 4 iliyopita anauwezo mkubwa sana kimpira na tunamuombea aendelee kuibeba bendera ya Tanzania popote atapoenda huko mbeleni...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: COSTA APATIKANA NA HATIA


FA wamemkuta Diego Costa na hatia ya kufanya fujo uwanjani...FA walitumia marefa watatu wazoefu na kuonyeshwa mkanda ambao unaonyesha Costa akimsukuma usoni Laurent na badae kumfanyia fujo Gabriel na baada ya hapo wote walisema Costa apewe red card kwa makosa yake...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 20 September 2015

EPL: MARTIAL APACHIKA ZAKE 2 KATIKA USHINDI DHIDI YA SOUTHAMPTON



Anthony Martial ameanza vizuri baada ya kupata bao 2 katika game dhidi ya Southampton muda mfupi uliopita...Manchester walianza ovyo mwanzoni na walishambuliwa sana na pia walikuwa wakwanza kuchapwa lakini dogo Martial alikuja kusawaazisha...Man U walishinda 3-2 na wamshukuru sana huyo dogo mwenye umri wa miaka 19 tu aliyenunuliwa kwa bei mbaya kutoka Ufaransa...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: FUNGIA DIEGO COSTA MECHI 3 ASEMA ARSENE WENGER



Arsene Wenger kocha wa Arsenal amesema Diego Costa anatakiwa kufungiwa mechi 3 na FA baada ya kufanya uhuni uwanjani kwenye game ya Arsenal na Chelsea...Kutokana na kufanya uhuni huo refa Mike Dean alijifanya hakuona na badae akatoa kadi nyekundu kwa Gabriel wa Arsenal...Wenger amemlalamikia refa huyo kwa kuzembea kuchukua hatua dhidi ya Costa na amesema Dean ni dhaifu sana...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Sat 19 Sep 2015

Friday, 18 September 2015

MANCHESTER UNITED: MASHABIKI WAKASIRIKA FAMILIA YA GLAZER KUPATA £16 MILIONI KAMA GAWIO



Kikundi cha mashabiki wa Manchester United wamekasirika kusikia familia ya Glazer itapata pesa nyingi kama dividend...Ni mara ya kwanza Man U wanatoa gawio la shares toka timu hiyo iuze share zake mwaka 2002 kwenye soko la hisa la New York Stock Exchange...Mashabiki hao wanalalamika kwanini familia ya Glazer ipate pesa wakati imewaingizia hasara timu...Familia ya Glazer inamiliki 83% ya Man U...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND (GMT)

Sat 19 Sep 2015
  • Chelsea v Arsenal 12:45
  • Aston Villa v West Brom 15:00
  • Bournemouth v Sunderland 15:00
  • Newcastle v Watford 15:00
  • Stoke v Leicester 15:00
  • Swansea v Everton 15:00
  • Man City v West Ham 17:30
Sun 20 Sep 2015
  • Tottenham v Crystal Palace 13:30
  • Liverpool v Norwich 16:00
  • Southampton v Man Utd 16:00

Thursday, 17 September 2015

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YAANZA VIBAYA


Arsenal fc imeanza vibaya michuano mikubwa ya UEFA baada ya kufungwa 2-1 na Dinamo Zagreb...Mechi ilikuwa safi sana na Arsenal walikuwa juu kimpira lakini baada ya dakika 40 Olivier Giroud alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kufanya ndivyo sivyo mara ya 2...Katika mechi nyingine timu za Uingereza zilichapwa kasoro Chelsea ambao walishinda 4-0...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 14 September 2015

US OPEN: DJOKOVIC BINGWA


Novak Djokovic amemfunga Roger Federer kwenye fainali ya US Open na kuchukua kombe mbele wa watu wengi waliokuwa wanatazama mechi...Djokovic ambae ni namba 1 duniani ameshindwa kupata Grand Slam lakini amejitahidi sana na kufungwa mara 1 tu msimu huu...Haikuwa rahisi kucheza na Federer ambae ni mchezaji wa kipekee mwenye ujuzi wa hali ya juu wa tennis...Bofya hapa upate habari zaidi.

NBA: MVP MOSES MALONE PASSED AWAY AT 60


Moses Malone has passed away suddenly in Norfolk Virginia aged 60. 

MVP Malone was a very good player in the National Basketball Association (NBA) league. He  retired with the best defensive stats.



Malone will be remembered for being one of the earliest players from high school to the basketball league. 

In 1983 he was named MVP  when playing for his Philadelphia 76ers team. 




He also played for Houston Rockets for a period of 6 years and in Houston he made his mark as the best defensive player.



Getty Images

 

Mwaka 2001 aliingizwa kwenye orodha ya wachezaji bora duniani wa basketball na alisema yeye sio mchezaji mzuri bali mchapakazi...Mungu ailaze mahali pema roho yake...Bofya hapa upate habari zaidi.





Sunday, 13 September 2015

BOXING: MAYWEATHER ASEMA SASA BASI BAADA YA KUFIKIA REKODI YA MARCIANO


Floyd Mayweather amesema atastaafu ndondi kwani hakuna kitu kingine cha kuonyesha umwamba wake...Mayweather alimchapa Andre Berto kwa kushinda score card zote na kufikia rekodi ya Rocky Marciano ya 49-0...



Bado Mayweather anaweza kuongeza pambano moja au mawili lakini kwa sasa amesema anataka atumie muda wake na familia...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 12 September 2015

US OPEN: SERENA NJE


Wadau wa tennis jana walishikwa na butwaa baada ya Serena Williams kufungwa na Roberta Vinci ambae hajawahi kushinda hata seti 1 katika mechi zake na Serena...Serena alitakiwa ashinde mara 2 ili apate Grand Slam na afikie rekodi ya Steffi Graf...Vinci alishinda 2-6 6-4 6-4...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 11 September 2015

MANCHESTER UNITED: DAVID DE GEA ASAINI MKATABA MPYA


David de Gea amewatoa hofu mashabiki wa Man U ambao walijua anahamia Spain...De Gea amesaini mkataba mpya na club hiyo kubwa ya Uingereza ambao utamweka hapo Old Trafford kwa miaka 4...



De Gea mwenye umri wa miaka 24 amechezea Man U mechi 175 toka atoke Atletico Madrid mwaka 2011 kwa dau la pounds milioni 18.9...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 10 September 2015

TOGO: ADEBAYOR THROWN OUT OF NATIONAL SQUAD


Emmanuel Adebayor, Tottenham Hotspurs player, has been booted out of his national team for being too snobbish. 

Wednesday, 9 September 2015

Sunday, 6 September 2015

F1: LEWIS HAMILTON ACHUNGUZWA BAADA YA KUSHINDA ITALIAN GP


Lewis Hamilton ameshinda Italian Grand Prix lakini yuko katika uchunguzi wa presha ya matairi yake...Nafasi ya 2 alichukua Sebastian Vettel na ya 3 Filipe Massa...Lewis mwishoni aliambiwa akimbize sana na timu yake na hakuelewa kwanini na wakamwambia watamueleza kwanini badae...Kumbe tairi lake lilikuwa na upepo kidogo 0.3 psi chini ya sheria za mashindano...Timu ya Hamilton walikuwa wanataka akimbize ili wakipigwa faini awe ndani ya muda mzuri...Bofya hapa update habari zaidi.

AFCON 2015: TANZANIA YASHINDWA KUICHAPA NIGERIA


Taifa Stars imeshindwa kuifunga Super Eagles nyumbani na sasa in a mlima wa kupanda wakienda kwao....Stars walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia...Mzunguko was 2 Eagles watajizatiti sana...Stars walicheza vizuri sana tofauti na matarajio ya wengi...Half time mechi iligeuka kuwa kituko cha siasa baada ya mbunge was Bumbuli Mh. January Makamba kuwalipia watu ambao walikuwa nje ya uwanja waingie kucheki game...Ilivyotangazwa tu umati wa watu walizomea sana na kuonyesha ishara za Ukawa...Kitendo hicho kilishangaza benchi la Nigeria na wakibaki wantoa macho tu...Bofya hapa upate habari zaidi.


BEACH VOLLEYBALL LEAGUE: FURSA YA KUSOMEA UREFA


Referee Training for Beach Volleyball League.
Training Date:12-18 September 2015
Venue: Shule ya Uhuru Kariakoo

iP Sports Club ina nafasi 2 za members wa teams zetu kwenda kusomea Referee wa  Beach Volleyball ,training hii itawezesha muhudhuriaji kusimamia ligi ya mchangani ya Volleyball kwa mkoa wa Dar es salaam itayoanza hivi karibuni,lakini pia itampa mhusika nyenzo muhimu za kumfanya kuwa mwalimu wa mchezo husika.

Ueleze kwa ufupi kwa nini unataka kupewa nafasi ya kusomea u referees na kusoma kwako kutaisaidiaje club yetu katika mchezo wa Volleyball.

Nitumie Cv na maelezo yako kwenda:

iP Sports Club
P.O.Box 92
Dar es salaam. Email:info@matemabeachfestival.com
Tell:+255758484040

Saturday, 5 September 2015

AFCON 2015: STARS UWANJANI LEO NA EAGLES


Taifa Stars leo watachuana na Super Eagles ndani ya uwanja wa taifa....Kwa mara ya kwanza timu hizi zilikutana ilikuwa 1962 na wakatoka sare....Mara ya 2 ilikuwa mwaka 1980 na Eagles walituchapa 3-1...Timu hizi zimekutana mara 4 katika historia na leo ni mara ya 5....Bofya hapa upate habari zaidi.