Tuesday 22 September 2015

TP MAZEMBE: MBWANA SAMATTA WA TANZANIA AWIKA



Mbwana Samatta mtazania ambae anachezea timu kubwa sana ya TP Mazembe anafanya vizuri sana...Alipata hat-trick dhidi ya Moghreb ya Morocco na kuipeleka TP Mazembe nusu fainali ya Africa's Champion League...Samatta anasema anafikiria kucheza soka Ulaya kwani watanzania wachache wameweza kujaribu kucheza Ulaya...Mwaka 2010 Haruna Moshi aliichezea timu ya Gefle IF ambayo iko kwenye premier league ya Sweden na Renatus Njohole alijitahidi sana akiwa na timu ya Uswiss ya premiership ya Yverdon Sport kati ya mwaka 1999 mpaka 2001...Samatta ambae alitokea Simba miaka 4 iliyopita anauwezo mkubwa sana kimpira na tunamuombea aendelee kuibeba bendera ya Tanzania popote atapoenda huko mbeleni...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment