Tuesday 9 December 2014

EPL: VAN PERSIE AIOKOA MAN UNITED


Manchester United lazima wakatambike maana hata kocha Van Gaal anasema ulikuwa na bahati balaa...Manchester united imepanda na kukaa number 3 kwenye ligi kali ya premiership baada ya kushinda 1-2 dhidi ya timu kali ya Southampton kwenye uwanja wa St. Mary's...Toka August 23 mwaka jana Manchester United haijawahi kuiona hiyo nafasi ya 3 na sasa wako katika ushindani mzuri wa kubakia top 4 kwenye ligi...Van Persie alipachika bao mapema dakika ya 12 baada ya makosa ya John Fonte katika kutoa pasi...Southampton walisawazisha dakika ya 31 kupitia kwa Graziano Pelle na baada ya hapo Man U walishambuliwa na kukoswa mara kibao...Van Persie aliibuka tena baada ya free-kick ya Rooney kumkuta Van Persie na kupachika bao la ushindi...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment