Monday, 23 June 2014

WORLD CUP 2014: MSIMAMO WA GROUP A-C

Group A
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS

1
2
1
1
0
3
1
2
4

2
2
1
1
0
1
0
1
4

3
2
1
0
1
5
3
2
3

4
2
0
0
2
0
5
-5
0
 
Group B
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS

1
2
2
0
0
8
3
5
6

2
2
2
0
0
5
1
4
6

3
2
0
0
2
3
6
-3
0

4
2
0
0
2
1
7
-6
0
 
Group C
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS

1
2
2
0
0
5
1
4
6

2
2
1
0
1
3
3
0
3

3
2
0
1
1
1
2
-1
1

4
2
0
1
1
0
3
-3
1
 

U.S WOMENS OPEN CHAMPIONSHIP: MICHELLE WIE ASHINDA MAJOR YA KWANZA


Michelle Wie amefanikiwa kushinda shindano la kwanza kubwa la Golf la U.S. Open ya wanawake...


Wie ambae wadau wengi wa Golf walithani amepunguza uwezo wake wa kucheza walibaki wakishangaa baada ya Wie kuongoza U.S Open round ya pili mpaka ya mwisho na aliingia round ya mwisho akiwa -3 (3 under par) na akashinda kwa stroke mbili mbele ya mchezaji Stacy Lewis...
 
Hapa akiwa na Caddie (msaidizi) wake



Wie alianza kucheza mashindano makubwa akiwa na miaka 13 mwaka 2003 alisifiwa sana na lakini miaka ilivyosogea hakuwa mkali kama watu walivyotegemea na ndio maana ushindi huu ni muhimu sana kwake na kwa Golf ya wanawake...Bofya hapa upate habari zaidi...

WORLD CUP 2014: USA YASHINDWA KUIFUNGA PORTUGAL


Varela alipokea cross ya Cristiano Ronaldo na kupachika bao dakika ya mwisho ya mechi  na kuharibu kabisa sherehe za USA za kusonga mbele kwenye 16 bora...Nani aliwaweka Portugal mbele mapema kwenye dakina ya 5 tu...



Badae sana Jermain Johns alisawazisha na dakika 9 kabla ya mchezo kuisha Clint Dempsey ambae ni supa staa wa USA alipachika bao...Portugal ilikuwa watolewe lakini walikomaa na lazima walishukuru muda wa nyongeza ulikuwa mwingi...


Sasa Group G iko wazi na wote wana nafasi ya kusonga mbele...Kazi ipo...Bofya hapa upate habari zaidi...

TFF: SIMBA RUKSA KUENDELEA NA UCHAGUZI


TFF wamewaruhusu Simba SC kuendelea na uchaguzi wao...Uchaguzi utafnyika Juni 29...Habari hizi zilitolewa na msemaji wa TFF bwana Boniface Wambura...Uamuzi huu ulikuwa baada ya Aden Rage kuiandikia TFF na kuiomba iwaruhusu waendelee na uchaguzi kama ilivyo pangwa...Rage alimwomba rais wa TFF asisitishe uchaguzi kwani kufanya hivyo utaleta sura mbaya kwenye club na nchini...Malinzi alisimamisha uchaguzi na kuwataka Simba watengeneze kamati ya uadilifu ndani ya club na hii imetokana na malalamiko mengi na pia sheria inasema club lazima ziwe na kamati ya uadilifu...Bofya hapa upate habari zaidi...

F1: LEWIS HAMILTON ASHIKA NAFASI YA 2 BAADA YA KUANZA WA 9


Nico Rosberg kutoka timu ya Mercedes amechukua Austrian Grand Prix...Nico akishindana na na mwenzake Lewis Hamilton aliwez kushinda ingawa Lewis ndio aliyefanya kazi sana kutoka wa 9 mpaka wa 2...Valtteri Bottas alikuwa wa 3 na ni mara yake ya kwanza kufika top 3...Massa alichukua nafasi ya 4...GP imerudi Austria toka 2003 katika uwanja wa Red Bull zamani ulikuwa unaitwa A1-Ring kabla ya kununuliwa na Red Bull...Bofya hapa upate habari zaidi...

Saturday, 21 June 2014

WORLD CUP 2014: SAJO NA WADAU NDANI YA BRAZIL

Mdau Sajo Kibonde na Wasia Mushi wakiwa na bendera ya Tanzania wakituwakilisha vyema huko Brazil...Safi sana wadau...

Sajo Kibonde (kushoto) na Wasia Mushi (wa 4 kutoka kushto) wakiwa na wenyeji wao huko Brazil - Picha kwa hisani ya Materi a.k.a Bucha

WORLD CUP 2014: JOE MARO NA WENZAKE WATUWAKILISHA SAO PAULO

Mdau wa Max Sports Joseph Maro na wenzake wanatuwakilisha vyema huko Sao Paulo kwenye World Cup...Tunashukuru sana kwa kutuwakilisha...Brazuka!

Joe Maro (Kulia) na wadau wenzake

Sehemu zote ukipita utakutna na screen kubwa

MAZOEZI: GYM MPYA NA YA KISASA IMEFUNGULIWA UPANGA

Just Fitness ni Gym mpya na yenye vifaa vya kisasa imefunguliwa Upanga mtaa wa Mindu opposite Richmond Appartments...Karibuni wadau wote...Ukiwa unatoka kazini na hautaki kukaa kwenye foleni zetu za Dar basi unakaribshwa ufanye mazoezi...Walimu waliobobea katika mazoezi na pia waliobobeea katika mafunzo ya kuogelea pia wapo...Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako... Pata picha hapo chini za Just Fitness...










Karibuni wote...

WORLD CUP 2014: BENZEMA AIWASHIA MOTO USWISS

Hebu mcheki Benzima alivyo wawashia moto Switzerland hapo chini...Uswss walichapwa 5-2...



Friday, 20 June 2014

WORLD CUP 2014: ROY HODGSON AGOMA KUJIUZULU


Kocha wa England amegoma kujiuzulu baada ya kuchapwa na Uruguay 2-1...Sasa England ina hali tete sasa kwani nafasi ya kuingia kwenye mtoano imekuwa finyu sana...Hii haijawahi kutokea kwa England kuondoka mapema toka 1954...England sasa wanasubiri game ya Italy na Costa Rica...Italy wakishinda England itasonga mbele...Pata habari zaidi hapa...

YANGA: MAZISHI YA GEORGE 'CASTRO' MPONDELA

Watoto wa Marehemu wakiweka shada la maua

Rais w TFF Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Yusuf Manji CEO wa Quality Group

Yusuf Manji akiweka shada la maua

Rais wa TFF Jamal Malinzi kiweka shada la maua



Thursday, 19 June 2014

ATHLETICS: JUSTIN GATLIN ANAONGOZA KWA MBIO 2014


Justin Gatlin, bingwa wa kukimbia na mshindi wa medani ya dhahabu katika Olympics za 2004, alikimbia mbio za mita 100 kwa kutumia sekunde 9.86 jana.... Mpaka sasa anaongoza mwaka huu kwa kuwa mtu mwenye spidi kuliko wote...Gatling alikimbia  kwenye mashindano ya Golden Spike huko Czech Republic...

WORLD CUP 2014: SPAIN YAVUNJA REKODI


Vargas akipachika bao

Spain jana ilivunja rekodi kuwa timu ya kwanza ambayo ni mabingwa watetezi kufungwa mechi mbili za mwanzo na kutolewa...Hii ilitokea katika uwanja wa Maracana baada ya kuchapwa 2-0 na Chile...Spain sasa umahiri wao kwa miaka 6 ndio umeisha... Chile walicheza vizuri sana na pia goli lao la kwanza lilikuwa la kiufundi sana na aliye funga alikuwa Eduardo Vargas kwenye dakika ya 20...
 
Casillas akifungwa baada ya kutokuwa makini

Chales Aranguiz alipachika bao la 2 mnamo dakika ya 43 baada ya Ike Casillas kutokuwa makini...Chile na Netherlands watasonga mbele kwenye mtoano...Bofya hapa usome zaidi....

WORLD CUP 2014: NETHERLANDS WATOLEWA JASHO NA AUSTRALIA



Netherlands jana walikimbizwa na Australia ambayo ni timu yenye rank ya chini kuliko zote kwenye World Cup ya mwaka huu...Katika uwanja wa Beira Rio Australia walicheza mpira mzuri sana bila kuogopa mtu na Netherlands walikuwa wanasali mpira uishe maana kuna kipindi walikuwa nyuma 2-1 na Van Persie alirudisha bao wakawa sawa... Tim Cahill ambaye sasa anacheza soka huko Marekani alipachika bao zuri sana...Netherlands inabidi wajipange maana hii World Cup sio ya mzaha kabisa...Bofya hapa usome zaidi....

Wednesday, 18 June 2014

SQUASH: HUDHAIFA ASHRAF ASHINDA JUNE DAR GHYMKHANA CLUB JUNIOR BELL

Ashraf akipokea zawadi kutoka kwa Mr. Marwa Busigara

anayejitahidi sana Hudhaifa Ashraf ameshinda michuani ya mwezi wa June...Ashraf pia alikuwa mshindi ya muchuano ya mwezi May...Nafasi ya 2 ilichukuliwa na dogo mwingine mkali Fadhili Ally...
 
Fadhili Ally akipokea zawadi


Junior Bell ya mwezi huu imekuwa kivutio kikubwa sana na hasa pia support ya familia ya walioshiriki imesaidia sana...Hongera kwa washindi na walioshiriki...

WORLD CUP 2014: FRANCISCO GUILLERMO OCHOA AWA KINARA WA GAME YA BRAZIL NA MEXICO



Guillermo Ochoa kipa wa Mexico amekuwa kinara wa mechi kali sana ambayo mpaka sasa tulikuwa hatujawahi kuona mechi kali kama hii ya Brazil na Mexico...

Tuesday, 17 June 2014

YANGA: MPONDELA KUZIKWA KESHO KUTWA KINONDONI


Katibu Mkuu wa zamakni wa YANGA marehemu George 'Castro' Mpondela aliyefariki kutokana na kuugua ugonjwa wa Moyo anatarajiwa kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni Alhamisi ijayo...Kwa habari zilizoingia Max Sports hivi punde ni kwamba mwili wa marehemu utalala nyumbani kwake kesho huko Kigamboni na Alhamisi kutakuwa na misa heshima za mwisho Kanisa Katoliki Muhimbili saa 7 na baada ya hapo atapelekwa kupumzika katika makaburi ya Kinondoni...Apumzike kwa Amani...

EPL: CHELSEA WANAMTAKA SANA TONI KROSS


Chelsea FC wamemwekea dau kijana matata mwenye umri wa miaka 24 Toni Kross  kutoka Bayern Munich na wanataka kumlipa 130,000 kwa mwezi pound za Uingereza... Wengine wanaomwania Toni ni Real Madrid na Manchester United....

GOLF: KINARA WA GOLF TANZANIA NURU MOLLEL ASHINDA HUKO ARUSHA


Nuru Mollel kijana mkali sana katika mchezo wa Golf nchini Tanzania ameshinda michuano mikali ya K.N.L. Legal Golf Tournament huko Arusha Gymkhana Club (AGC)...Mollel alipata score ya -4 (four-under) 40 points...Katika mashindano haya makali yaliyotumia mfumo ya stable ford Mollel alimpita Fransis Julius ambaye alikuwa wa 2 na wa 3 alikuwa Peniel Uriwa...Bofya zaidi hapa upate mambo zaidi...

WORLD CUP 2014: DRAW YA KWANZA BILA KUFUNGANA KWENYE WORLD CUP NI KATI YA NIGERIA NA IRAN


Katika game mbovu toka michuano hii ianze ni hii ya Nigeria na Iran...

WORLD CUP 2014: USA YAANZA VIZURI


USA meanza vizuri michuano ya World Cup huko Brazil kwa kuichapa Ghana 2-1...USA wameweka rekodi kwa kufunga goli la 5 la haraka katika historia ya World Cup...Bao hilo lilifungwa dakika 29 tu toka mpira uanze...Bao lilifungwa na Clint Dempsey...Ghana walichangamka baadaye sana na Andrew Ayew alipokea mpira kutoka kiganja cha nyuma cha Asamoah Gyanbao na kupachika bao...Mwishoni wamarekani walianza kuishiwa pumzi lakini John Brooks aliweza kupata bao la ushindi kwa kichwa...Hichi ni kisasi ambacho Marekani wanalipa kutokana na kutolewa katika mechi za World Cup zilizopita na Ghana...Bofya hapa upate habari zaidi...

Monday, 16 June 2014

WORLD CUP 2014: GERMANY YAICHAPA PORTUGAL 4


Germany imetoka kuigaragaza Protugal vibaya sana kwa bao 4-0... Thomas Muller alipata hat-trick leo...Wajerunani walijipanga sana na badae Portugal wakawa wana hasira na hii ilionyesha baada ya Muller kufanyiwa foul na Pepe na alivyukuwa chini Pepe alikuja karibu na kumgonga kichwa mwenzake ndio refa akaona atoe red card...Coentrao pia aliumia na kutolewa nje kwahiyo Portugal na Ronaldo walikuwa hawana tena nguvu....Hii ni hat-trick ya kwanza kwenye World Cup hii ambayo imejaa magoli mengi...Portugal na Ronaldo wao itabidi wakajipange kama kweli wanataka kushinda...Germany waliongoza possession 54%-46%...

Sunday, 15 June 2014

WORLD CUP 2014: IVORY COAST YAANZA VYEMA KWA KUICHAPA JAPAN




Ivory Coast imekuwa nchi ya kwanza ya kutoka Africa kushinda game yake ya kwanza hapo Arena Pernambuco...Ivory Coast iliichapa Japan 2-1...Japan ndio walianza kufunga bao na aliyefunga ni Keisuke honda...kipindi cha kwanza kilikri kwa timu zote mbili kwani Japan walishambulia sana lango la Ivory Coast na badaae kibao kikageuka...


Kipindi cha kwanza Didier drogba alikuwa benchi na alipoingia tu game ikabadilika na Ivory Coast ikapata mwamko mpya...Mbony alipachika bao baada ya cross kutoka kwa Serge Aurier dakika ya 64...Dakika 2 tu baadae Gervinho alipachika la pili...Hii ni mara ya 3 Ivory Coast wanacheza World Cup na hawajawahi kwenda mbele ya group stage...Bofya hapa upate habari zaidi....

Saturday, 14 June 2014

WORLD CUP 2014: COLOMBIA YAICHAPA GREECE


Colombia imepata points 3 za uhakika baada ya kuichapa Greece mabao 3-0...Pablo Armero wa kutoka Napoli ambae yuko West Ham kwa mkopo ndio aliye pachika la kwanza mwanzoni...


Gutierrez ambae ni forward aliyechukua nafasi ya Ramadel Falcao aliweza kupata bao la 2 baada ya kona kutoka kwa James Rodriguez...Huyo Rodriguez aliweza kufunga la 3 dakika za nyingeza...Usikuose mechi ya Italy na England badae usiku huu...