Monday, 11 April 2016

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

1Leicester332672
2Tottenham333565
3Arsenal322259
4Man City322557
5Man Utd32953
6West Ham321252
7Southampton331050
8Liverpool31848
9Stoke33-647
10Chelsea32744
11Bournemouth33-1541
12Swansea33-840
13West Brom32-840
14Everton31939
15Watford32-638
16Crystal Palace32-737
17Norwich33-2231
18Sunderland32-2127
19Newcastle32-2925
20Aston Villa33-4116

EPL: MANCHESTER UNITED HOI KWA TOTTENHAM


Manchester United wamechapwa 3-0 na Tottenham ndani ya White Hart Lane jana jioni...Tottenham bado wanandoto za mbali za kuchukua ubingwa lakini bado kazi ipo kwani Leicester wako points 7 mbele yao na bado mechi kama 5 vile...Dele Alli ndie aliye pachika bao la kwanza kipindi cha 2 akifuatiwa na kichwa cha Toby Alderweireld na bao la mwisho kutoka kwa Erik Lamela...Manchester United walijitahidi kidogo lakini baada ya dogo Timothy Fosu Mensah kujitahidi sana na badae kuumia ndipo mabao yalianza kumiminika...Mensah mwenye miaka 18 ndie aliyekuwa mchezaji bora Manchester akifuatiwa na Anthony Martial...Bofya hapa upate habari zaidi.

LEICESTER CITY FC: CLAUDIO RANIERI KOCHA WA MWEZI BARCLAYS PREMIER LEAGUE


Claudio Ranieri amekuwa kocha bora wa mwezi Barclays Premiership baada ya timu yake kufanya vizuri sana na pia haikufungwa mwezi March...Ni mara ya 2 msimu huu  Ranieri anachukua tuzo hiyo ya kocha wa Mwezi...Mpaka sasa Leicester au kwa jina maarufu 'The Foxes' wamepoteza mechi 3 tu...Leicester sasa wako points 10 mbele ya Tottenham na wakishinda mechi 2 tu wanatangazwa mabingwa...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 10 April 2016

BOXING: ANTHONY JOSHUA AMTANDIKA CHARLES MARTIN ROUND YA 2 NA KUNYAKUA UBINGWA WA IBF


Anthony Joshua kutoka England amekuwa bingwa wa heavyweight wa mkanda wa IBF baada ya kumchapa Marekani Charles Martin...Martin alikula jabs na makonde yakutosha hasa ya kulia na refa kusitiaha pambano round ya 2 baada ya kuona anaumia...


Joshua ni bingwa wa ndondi za Olympics na sasa kwa mara ya kwanza anakuwa bingwa wa heavyweight...


Joshua ni kati ya watu 3 duniani ambao baada ya kuwa bingwa wa Olympics anakuwa bingwa wa heavyweight...Wengine ni Muhammad Ali na Leon Spinks...Mwaka 1960 Ali alikuwa bingwa wa Olympics na mwaka 1964 akamtandika Sonny Liston na kuwa bingwa wa heavyweight...


Mwaka 1976 Leon Spinks Alipata dhahabu ya Olympics na badae mwaka 1978 alimchapa Ali...Huko mbeleni sasa inaonekana kama Joshua atakutana na bingwa mwingine wa Uingereza Tyson Fury...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: ANDY CARROLL AWASHIKA SHATI ARSENAL


Ndoto za Arsenal zimefifia leo baada ya kushikwa shati na hat-trick ya Andy Carroll wa West Ham United...Game ilikuwa balaa kwani iliisha 3-3 ulimi nje...Carroll alitandika mabao 3 ndani ya dakika 10 na bao la 2 lilikuwa hatari...



Matokeo ya leo hayasaidii timu zote mbili wakati game zimebaki chache...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 8 April 2016

LIVERPOOL F.C.: LIVERPOOL NA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND HOI BAADA YA JORDAN HENDERSEN KUUMIA


Jordan Henderson aliumia katika game dhidi ya Dortmund ambayo Origi alisaidia kuwapatia bao Liverpool na mwisho wa game wakatoka 1-1...

EUROPA LEAGUE 2016: KLOPP APOKELEWA VIZURI NA MASHABIKI WA DORTMUND


Liverpool waliingia uwanjani dhidi ya Dortmung kwenye ungwe ya kwanza ya Europa League na kabla ya mechi kuanza Jurgen Klopp alikaribishwa na alishangiliwa sana na mashabiki wa Dortmund...


Klopp alikuwa kocha wa Dortmund toka 2008 mpaka 2015...Klopp aliwasaidia washinde vikombe 2 na kuwapeleka fainali ya Uefa...


Mashabiki walishika mabango na yaliyoandikwa maneno ya kumkaribisha nyumbani...Bofya hapa upate habari zaidi.

U.S. MASTERS 2016: JORDAN SPIETH TAKES THE OK EAD


Previous  Masters winner takes the lead at  Agusta,Georgia. Jordan Spieth is at -6 followed by  S. Lowry na D. Lee at -4 -4...Cluck here for more.

Wednesday, 6 April 2016

PANAMA PAPERS: BOSS WA FIFA GIANNI INFANTINO ATAJWA KWENYE DOCUMENTS ZA KAMPUNI ILIYOSAIDIA WATU MASHUHURI KUFICHA PESA


Gianni Infantino, Boss mpya wa FIFA, ametajwa kwenye documents ambazo zinaonyesha jinsi watu mashuhuri duniani wakiwemo maraisi na mawaziri wanavyoficha pesa kukwepa kodi...Hizo documents zinajulikana kama 'Panama Papers' na zimetoka kwenye kampuni ya binafsi ya sheria nchini Panama...




Kampuni hiyo jina lakie ni Mossack Fonseca na hizo documents ziliibiwa kupitia mitandao na sasa zimeibua mtazamo mpya kuwa kumbe watu wengi wanakwepa kodi duniani...Kwa upande wa Infantino ni kwamba hizo documents zinazungumzia watu ambao aliwahi kufanya nao mkataba zamani na hao watu wameshahusishwa na rushwa....


Hugo Jinkis, anahusishwa na dili la Uefa na rushwa

Watu hao wanaitwa Hugo Jinkis na Mariano Jinkis ambao walinunua TV rights za Uefa Champions League na baada ya muda mfupi tu wakauza hizo TV rights mara 3 na kuondoka na pesa nyingi sana...Kipindi hicho mkataba huo ulipitishwa na Gianni Infantino ambae alikuwa Mkurugenzi wa Uefa...


Mariano Jinkis akiwa amekamatwa na polisi pamoja na
mzee wake Hugo Jinkis

Infantino amesikitika watu kumfikiria vibaya na FIFA imesema hiyo tender alishinda mwenye dau kubwa na ilikuwa halali...Bofya hapa upate habari zaidi.


CHAMPIONS LEAGUE 2016: BARCELONA YATOKA NYUMA NA KUWACHAPA ATLETICO MADRID 2-1


Barcelona wameshinda mechi ambayo ilikuwa na tension toka mwanzo pamoja na vikumbo vingi...Atletico Madrid walianza kutingisha nyavu kupitia Fernando Torres lakini Torres alivyokuwa kichwa hewa akafanya ndivyo sivyo akalamba kadi ya 2 ya njano na kutolewa nje kabisa ya uwanja...Suarez ndie iliyewaokoa Barca kwa bao dakika ya 63 na dakika ya 74...Barca walichachamaa sana na kushambulia lango la Madrid mara kwa mara mithili ya nyuki wadogo...


Mabao yote ya Barca walikuwa yameenda shule kwani gonga hatari zilitembea na kuwaacha Atletico kutoa macho tu...Kinachowapa moyo Atletico Madrid ni bao la ugenini ambalo litawasaidia wakirudiana...Bofya hapa upate habari zaidi.

ATHLETICS: KENYA KARIBU WANAFUNGIWA KWA MAKOSA YANAYOHUSU UTUMIAJI WA DAWA ZA KUIONGEZA NGUVU


Kenya bado hawajipanga vyema kutatua masharti yaliyowekwa na taasisi cha kudhibiti na kuzuia madawa ya kulevya...Walipewa muda kutatua masharti na muda huo karibu unaisha kwa hiyo wanaweza kukosa Rio 2016...Kenya walihusishwa na matumizi hayo kwenye ripoti ambayo ilisema Urusi na Kenya wanatumia sana dawa na pia inahusishwa na rushwa...World Anti-Doping Agency wanakaa kikao kujadili suala la Kenya Jumanne ijayo na wanaweza wakatangaza Kenya haijafuata masharti ya Wada...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 5 April 2016

REAL MADRID: BAADA YA KUWACHAPA MAHASIMU WAO REAL SASA WAKO TAYARI KUIKABILI WOLFSBURG


Real wamesafiri kwenda kucheza na Wolfsburg baada ya ushindi wao dhidi ya Barcelona...Madrid wameonekana wakiwa na furaha tele na uhakika wa ushindi walivyo kuwa wanasafiri kwenda kucheza mechi ya Champions League huko Germany...


Walitumia shuttle kwenda Madrid-Barajas Airport na hapo wakaingia kwenye ndege binafi na kwenda Germany...


Wachezaji wote walipiga suti hatari kabisa mithili ya zile za Azam walivyo enda bondeni...Bofya hapa upate habari zaidi.

NCAA FINALS 2016: VILLANOVA MABINGWA KWA 'BUZZER BEATER' YA KRIS JENKINS


Villanova wamenyakua ubingwa wa vyuo vikuu marekani....Villanova wanatokea nje kidogo ya Philadelphia na ni shule ya kikatoliki na mwaka huu wameshinda ubingwa wao wa 2 kwa kuwachapa North Carolina sekunde chache sana za mwisho...


Kris Jenkins ndie aliyezamisha mpira wa 3 points sekunde chache sana kabla kengele ya mchezo kupiga kuashiria mwisho wa game...Game ilikuwa kali sana na timu zote zilitoka na kucheza kwa moyo sana...



Kwa kweli game ya leo itakumbukwa kama game kali sana kuliko game nyingi au zote kwani game ilikuwa kali na kilichoamua ubingwa ni shot ya Jenkins tu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 4 April 2016

MANCHESTER UNITED: SIR BOBBY CHARTON APEWA HESHIMA KUBWA KWA KUPEWA ENEO LENYE JINA LAKE OLD TRAFFORD


Sir. Bobby Charlton ni living legend wa Manchester United na kutaokana na heshima yake sehemu ya kusini wa Old Trafford umepewa jina lake...


Jana kabla ya kuanza game ya Manchester United dhidi ya Everton eneo hilo lilizinduliwa mbele ya mashabiki wengi na pia mbele ya wasio mashabiki lakini wanamkubali Sir Bobby kutokana na mchango wake Manchester United...


Sir. Bobby ambae sasa ni mmoja wa wakurugenzi wa club aliingia Manchester mwaka 1953 na kucheza mechi 758 na kufunga mabao 249...Alichezea timu ya England iliyoshinda World Cup ya mwaka 1966...


Sir Bobby alikuja uwanjani na mke wake Norma na Makamu Mwenyekiti wa club ya Manchester Ed Woodword...Eneo la kusini la uwanja ni eneo ambalo halijabadilishwa toka uwanja ujengwe mwaka 1910 na ndio sehemu wakurugenzi wanakaa au kwa jina maarufu 'directors box'...


Alinusurika kifo mwaka 1958 baada ya ndege iliyobeba wachezaji wa Manchester United kuanguka huko Munich na kuua watu 8...Bofya hapa upate habari zaidi.

ICC WORLD TWENTY20 FINALS: WEST INDIES WAWACHAPA ENGLAND NA KUBEBA KOMBE KWA MARA YA 2


West Indies wameweka historia baada ya kuchukua ubingwa wa Cricket duniani wa Tewnty20 kwa mara ya 2...West Indies waliwachapa England kwa wickets 4 wakiwa ndani ya jiji la Kolkata...Kwa upande wa wanawake West Indies waliwachapa Australia...


Cricket T20 ilikuwa inaonekana haina issue kabisa lakini mwaka huu imesisimua mashabiki na kupata kuonekana katika sura mpya...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 3 April 2016

EPL: LEICESTER CITY WAKO MBIONI KUNYAKUA KOMBE LA PREMIERSHIP BAADA YA KUSHINDA DHIDI YA SOUTHAMPTON SIKU YA KUZALIWA MWENYEKITI WA CLUB


Leicester City dakika chache zilizopita wamefaniakiwa kushinda bao 1 dhidi ya Southampton...Captain ndio aliyewapatia bao Leicester City....Sasa wako points 7 mbele ya Tottenham na bado mechi 6 tu msimu uishe....Mechi ilikuwa nzuri na kila timu imecheza vizuri....Southampton wamejitahidi sana pamoja na hayo walinyimwa penalty lakini ndio hivyo Leicester wanayoyoma...Leo ni siku ya kuzaliwa Mwenyekiti wa Leicester F.C. na alikuwa anaangalia mpira uwanjani  akapata zawadi wa bao kutoka kwa Captain...Bofya hapa upate habari zaidi.

EL CLASICO: REAL MADRID WAWASIMAMISHA BARCA


Cristiano Ronaldo jana aliweza kupachika bao lake la 42 la msimu huu na kuwasimamisha Barca ambao wameshinda mechi 39 bila kufungwa....Mwanzo mechi ilikuwa kali na ya umakini kwa pande zote mbili na mnamo dakik aya 56 Gerald Pique akipiga kichwa cha chini na kuiweka Barca mbele...



Karim Benzema nae akapiga bao hatari sana la mkasi na kusawazisha...Bale alikataliwa bao na Sergio Ramos alitolewa baada ya kufanya ndivyo sivyo mara 2...Bofya hapa upate habari zaidi.