Friday 28 October 2016

YOUNG AFRICANS FC: HATIMAYE KOCHA PLUIJM AREJESHWA JANGWANI


Sakata la kocha Hans van der Pluijm lachukua sura nyingine kabisa huku kocha huyo akirejeshwa tena Yanga...
Mwanachama wa siku nyingi sana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba, ameingilia kati issue ya kocha kwa kukaa nae kikao kuhusiana na kujiuzulu kwake hatimaye kufanikiwa kumrejesha kocha huyo...



Kikao hicho kilikuwa pia chini ya usimamizi wa Kaimu Katibu Mkuu Baraka Deusdedit...Ni habari njema kwa wana Yanga kwani ligi ndio imepamba moto na kubadilisha kocha wakati wachezaji wako mbioni kusaka ubingwa sio jambo jema...



Kutokana mazungumzo hayo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga alimwandikia kocha barua safi kabisa ya kumshukuru kwa saidia Yanga na pia kukataa kuziuzulu kwake...Habari hii ni njema kwa mashabiki na pia kwa wachezaji ambao wanapambana na ligi...Sasa ni  business as usual (biashara kama kawa) pale Jangwani.

No comments:

Post a Comment