Monday, 10 November 2014

EPL: SWANSEA YAIBUKA NA USHINDI


Arsenal imepoteza mechi ambayo walitakiwa kushinda na walikuwa mbele mpaka dakika za katikati kipindi cha 2...Arsenal kupitia kwa Alexis Sanchez walipachika bao dakika ya 63 baada ya Danny Welbeck kuchomoka na mpira fasta na kusukuma pasi safi ambayo ilimkuta Sanchez na akapachika bao la karibu...


Dakika ya 75 Gylfi Sigurdsson alisawazisha na badae kidogo Bafetimbi Gomis dakika ya 78 aliwapa Swansea ushindi...Swansea sasa wamekaa nafasi ya 5 na Arsenal wamedrop kuingia nafasi ya 6...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: YESTERDAY'S RESULTS

Sunday, 9 November 2014

Saturday, 8 November 2014

THE BLACK STARS: AVRAM GRANT KOCHA MTARJIWA GHANA


Aliyekuwa kocha wa Chelsea Avram Grant anatarjiwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ghana the Black Stars...Avram akikubaliana na shirikisho la soka la Ghana (GFA) kwenye masuala ya pesa atasaini mkataba na kuisaidia Ghana...Shirikisho la soka la Ghana limesema kati ya makocha, Juan Ignacio Martinez na Michel Pont aliyekuwa msaidizi wa timu ya Switzerland, wanamtaka Grant anayetokea Israel...Grant aliwapeleka Chelse mpaka fainali ya Euro Champions League 2008 na alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Israel kwa miaka 4...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 7 November 2014

ENGLAND SQUAD: MRUNDI SAIDO BERAHINO NDANI YA TIMU YA TAIFA


Saido Berahino alizaliwa Burundi ni mchezaji wa West Brom ambae amechaguliwa kuichezea timu ya taifa na kocha Roy Hodgson.

BBALL KITAA: CBE & UDSM WAPAMBANA LEO! USIKOSE!


Mechi kali ya basketball hapa mjini inasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya College of Business Education (CBE) na University of Dar es Salaam (UDSM) leo usiku katika vwanja vya Ghymkhana....Timu zote mbili ziko tayari kupambana na UDSM wako tayari kucheza vizuri baada ya kushindwa katika game yao ya 1...Game ya eo ni kati ya game nyingi za kusherekea mwaka 1 wa BBall Kitaa...


Mratibu wa BBall Kitaa, Lawrence Karabani, amesema wanajivunia kwamba BBall Kitaa imefanikiwa sana hasa kuwaunganisha vijana wengi kuwapa shughuli ya kufanya na hasa vyuo vimehusika sana...Pia wadhanini wa BBall Kitaa Coca-Cola kupiti kinywaji cha Sprite wamefurahi sana kupewa nafasi ya kupromote basketball nchini Tanzania na kuchangamsha maisha ya vijana wengi na wataendelea kufanya kazi na wadau wa basketball Tanzania ili kuendeleza mchezo huu na kukuza vipaji...Usikose kuangalia jii game leo usiku katika viwanja vya Gymkhana...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 6 November 2014

SQUASH WARM UP: ANGALIA NINAVYOPASHA MISULI KABLA YA GAME

CHAMPIONS LEAGUE: MATOKEO YA MECHI ZA JANA

CHAMPIONS LEAGUE: MAN CITY HALI TETE


Mambo sio mambo kwa Manchester City baada ya kuchapwa nyumbani na CSKA Moscow 2-1...Man City sasa wameshikilia mkia kwenye Goup E wakibakiwa na mechi 2...Hali ni tete kutokana na Yaya Toure na Fernandinho kutolewa na watakosa mechi inayokuja dhidi ya kisiki Bayern Munich...


Man City hawakucheza vizuri na Seydou Doumbia alianza kupachika bao mapema dakika ya 2 na dakika ya 8 Toure alisawazasha...Kipindi hicho hicho cha 1 Doumbia alipachika bao dakika ya 34 na kuwaacha hoi Man City ambao sasa wako hatrini kutolewa...Bofya hapa upate habari zaidi.


Wednesday, 5 November 2014

QATAR 2022 WORLD CUP: PLATINI ATAKA WORLD CUP IFANYIKE KIPINDI CHA BARIDI


Rais wa Uefa Michel Platini anataka World Cup itakayochezewa huko Qatar mwaka 2022 ifanyike kipindi ambacho hakina joto...Platini amesema joto litawaumiza sana wachezaji World Cup ikifanyika kipindi cha joto ambacho ndio kipindi cha summer kwa maeneo mengi ya kaskazini mwa Equator...Clubs nyingi zimesema ratiba ikibadilika itaharibu utaratibu wa mambo mengi lakini Platini amesena clubs hazichezi ila wachezaji ndio wanaocheza na hawawezi kucheza wakati joto liko centigrade 40...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL WAACHIA MAGOLI NA KUTOA DRAW


Arsenal wako karibu kufuzu kuingia 16 bora ya Champions League lakini walichemsha jana kwani walikuwa mbele magoli 3 na Anderlecht wakarudisha yote 3 ndani ya dakika 29...Bao 1 lilitoka kwa Arteta kwa njia ya penalty, la 2 kutoka kwa Alexis Sanchez kwa mkwaju mkali wa volley kutoka yadi 20 na la 3 kutoka kwa Oxlade-Chamberlain...Sasa Arsenal wanahitaji point 1 tu ili waweze kuingia 16 bora na bado wana game na Dortmund November 26 na Galatasaray December 9...Bofya hapa upate habari zaidi.


CHAMPIONS LEAGUE: YESTERDAY'S RESULTS

Tuesday, 4 November 2014

BALIMI BOAT RACE 2014: TEAM ELIUD PROSPER YANYAKUA UBINGWA


Mashindano ya Mkoa wa Kagera ya makasia au mitumbwi timu ya Eliud Prosper kwa upande wa wanaume na wanawake timu ya Khadija Ramadhan wamenyakua ubingwa...


Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na TBL kupitia brand yake ya Balini Extra Lager yalikuwa yakusisimua na ya ushindani mkubwa sana...


Mabingwa walizawadiwa 900,000/- na kupata nafasi ya kuiwakilisha Kagera kwenye fainali za kanda jijini Mwanza...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: BAADA YA CHRIS SMALLING KUITWA BWEGE NA VAN GAAL SASA ATANIWA NA VIRGIN TRAINS


Baada ya dogo Chris Smalling kuchemsha na kusababisha timu yake ifungwe na Manchester City kwa kufanya foul ya kizembe na kutokewa nje na baadae kocha Van Gaal kumwita Smalling 'Bwege' au kwa jina lingine 'Juha' sasa moja ya kampuni ya usafiri ya Uingereza ya Virgin Trains ambao wana treni nyingi wameamua kumtania Smalling kutokana na uzembe aliofanya uwanjani...Eti wanasema kwenye tweeter page yao kwamba ticket za kwenda London zipo!...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: SUNDERLAND YATOKA SHIMONI


Sunderland imefanikiwa kujitoa kwenye relegation zone baada ya kuichapa Crystal Palace 3-1...Steven Fletcher aliissaidia timu yake ya the Black Cats kwa kuipatia mabao 2...Bao la kwanza alipachika Fletcher dakika ya 31 kwa kichwa...Crystal Palace walizawadiwa bao wakati Wes Brown alipijifunga dakika ya 55...Sunderland walikuwa wamewazidi sana Crytal Palace hasa midfield na hata boss wa Sunderland Gus Poyet alisema walikuja kucheza wakijua wako vizuri kuliko Crystal Palace...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Chelsea101626
No movement2Southampton101622
No movement3Man City101020
No movement4Arsenal10717
No movement5West Ham10517
No movement6Swansea10315
No movement7Liverpool10014
No movement8Tottenham10-114
No movement9Everton10213
No movement10Man Utd10213
No movement11West Brom10013
No movement12Newcastle10-413
No movement13Stoke10-212
No movement14Hull10-111
No movement15Sunderland10-711
No movement16Aston Villa10-1110
No movement17Crystal Palace10-59
No movement18Leicester10-59
No movement19QPR10-117
No movement20Burnley10-144

Monday, 3 November 2014

F1: HAMILTON AMZIDI AKILI ROSBERG NA KUSHINDA USA GRAND PRIX


Lewis Hamilton amevunja rekodi ya Uingereza iliyowekwa na Nigel Mansel ya mtu mwenye kushinda races nyingi...Hamilton amesema alimzidi akili Rosgerg alivyompita na kushinda GP ya USA huko Austin Texas...


Kutokana na ushindi huu Hamilton yuko karibu na kushinda Championship ya GP...Bado kuna GP ya Braziil na Abu Dhabi na Hamilton akitoka wa 2 katika zote 3 atakuwa bingwa wa dunia...Bofya hapa upate habari zaidi.


Sunday, 2 November 2014

BMW MASTERS: ALEXANDER LEVY AONGOZA KWA MIKWAJU 4


Alexander Levy anaongoza BMW Masters akiwa mbele kwa shots 4 (-22) na anayemfuatia ni Jamie Donnaldson ambae ana -18...Levy alimaliza round ya 3 akiwa na 63 akiwa na birdies 9 katika mashimo 15 ya mwanzo...


Justin  Rose ameibuka wa 3 akiwa -15 na alimalizia round na 64...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MOURINHO ALAUMU MASHABIKI


Jose Mourinho amelaumu mashabiki waliokuja kuangalia game ya Chelsea na QPR...Mourinho amesema katika game ya jana utafikiri hakuna watu uwanjani mpaka walivyofunga ndio akashtuka kuwa kuna watu...Kipa wa QPR baada ya dakika 20 aliomba taa za uwnjani zibadilishwe na Jose alisema mtunza taa alikuwa amesinzia kama mashabiki....Jose amesema hajafurahishwa na jinsi timu yake ilivyocheza ingawa sasa wako points 9 mbele ya timu nyingine...Chelsea ilishinda 2-1...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 1 November 2014

BAFANA BAFANA: MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMUAGA KWA UCHUNGU CAPTAIN SENZO MEYIWA

Rais Zuma akiwa na Senzo Meyiwa enzi za uhai wake...
Mashabiki na wapenzi wa mpira wamejitokeza kwa maelfu na maelfu kumuaga Captain wa Bafana Bafana Senzo Meyiwa...Meyiwa alifariki kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa mpenzi wake wakati akijaribu kuzuia majambazi...


Watu wengi walijipanga barabarani na uwanja wa mpira wa Moses Madhiba ambao uko jijini Durban ulijaa sana wakimuaga Senzo Meyiwa kwa uchungu na majonzi makubwa sana...Kati wa waomblezaji walikuwepo rais wa shirikisho la mpira Afrika ya Kusini Danny Jordaan na wachezaji wenzake wa Orlando Pirates...


Audi Q7 nyeupe iliyobeba mwili wa marehemu Senzo Meyiwa iliingia uwanjani huku watu wote wakisimama kwa majonzi likifuatiwa na polisi na bendi ya polisi, kiongozi wa KwaZulu Natal, Edward Senzo Mchunu, rais wa shirikisho la soka, Dani Joordan, wachezaji wa Orlando Pirates na wengine wengi...


Mwili wake ulizungushwa uwanjani mara 1 na jeneza lilikuwa limefunikwa na bendera ya Afrika Kusini...Bofya hapa upate habari zaidi.


PARIS MASTERS: DJOKOVIC AMSIMAMISHA MURRY


Bingwa wa dunia Novac Djokovic amefanikiwa kumsimamisha Andy Murry...Andy ambae kashinda mechi 11 mfululizo alichapwa straight sets 7-5 6-2 na mtetezi wa Paris Masters Djokovic...


Sasa Andy atapumzika kidogo kabla hajamalizia msimu na World Tour Finals mjini London...Milos Raonic nae amefanikiwa kumchapa namba 2 duniani Federer 7-6 (7-4) 7-5 na yeye pia amefuzu kucheza World Tour Finals mjini London...Bofya hapa upate habari zaidi.