Thursday 3 November 2016

VODACOM PREMIER LEAGUE: YOUNG AFRICANS YACHAPWA NA MBEYA CITY 1-2


Dar es Salaam Young Africans (Yanga) wamechapwa na wenyeji wao Mbeya City 1-2 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya...
Ni ushindi wa kwanza kwa Mbeya City dhidi ya Young Africans toka wa pande daraja...



Bao la kwanza lilitoka kwa Hassan Mwasapili mapema kabisa mnamo dakika ya 6 tu na kwaacha Yanga wakitafakari...Kenny Ally nae akaongeza bao la 2 na ndipo mambo yalipokuwa magumu kwa Yanga kuondoka na pointi japo 1...



Donald Ngoma alifanikiwa kupata bao la kufutia machozi ingawa alipata shida za Tumba Sued...Sasa Mbeya City wana pointi 19 kati ya mechi 14 walizocheza na Yanga inabaki na pointi 27 kati ya mechi 13...



Mdau maarufu sana wa Max Sports, Kassim Mbarouk Mwandoro, alikuwa akisubiri matokeo ya kipenga cha mwisho kabisa huku akigoma kutoka kwenye redio yake ngumu ya National...Mdau huyu yuko makini kabisa kufuatilia matokeo ya ligi hii kali sana...Mdau mwingine mkuu wa Max Sports, Makulilo Kassera, anaifananisha Mbeya City na Chelsea FC ilivyo kuwa fasta msimu huu...Ingawa Chelsea sio kivile sana lakini ngoja tuangalie msimu unavyosonga mbele.

No comments:

Post a Comment