West Ham19:00Man Utd
Max Sports brings you the latest sports news, reviews, statistics, videos, documentaries and more from across the 🌎
Sunday, 17 April 2016
Saturday, 16 April 2016
EPL: ASTON VILLA YASHUKA DARAJA
Aston Villa yashuka daraja rasmi...Aston Villa wanakumbukia historia yao ya mwaka 1982 walivyo kuwa mabingwa wa Ulaya lakini kwa huzuni kubwa wanashuka daraja bila kupenda...Villa walishindwa kujipanga msimu huu katika moja ya ligi ngumu duniani...Leo baada ya kuchapwa na Manchester United 1-0 imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja...Newcastle nao hatinani kushuka ingawa leo wamepata mabao muhimu sana....Nyota wa mchezo wa leo ni dogo Marcus Rushford...Rushford ni mdogo kwa umri na umbo lakini hujituma kama veteran...Rushford leo kufunga bao lake la 4 toka aanzishwe na Van Goal mechi chache zilizopita....
Rooney amerejea leo lakini alikuwa mzito nadhani umri umesogea kwani anataka kujituma lakini mwili unakataa...Bofya hapa upate habari zaidi.
Friday, 15 April 2016
MONTE CARLO MASTERS 2016: ANDY MURRAY AMCHAPA KIRAHISI RIONIC NA KUINGIA NUSU FAINALI
Andy Murray amefanikiwa kumchapa Milos Raonic anayetokea Canada kirahisi 6-2 6-0 na kuingia katika nusu fainali ya michuano ya Monte Carlo Masters...Murray atakutana na Rafa Nadal nusu fainali...Bofya hapa upate habari zaidi.
EUROPA LEAGUE 2016: LIVERPOOL KUKUTANA NA VILLARREAL NUSU FAINALI
Ratiba ya nusu fainali imetoka na Liverpool FC wamepangiwa kucheza na Villarreal CF wakati FC Shakhtar watachuana na mabingwa Sevilla FC.
LEICESTER CITY: DAU LA N'GOLO KANTE £20 MILIONI NA PSG WANAONGOZA MBIO ZA KUMYAKUA DOGO
N'golo Kante mwenye umri wa miaka 25 anasakwa sana PSG pamoja na timu zingine kubwa...Kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachosema kama unamtaka Kante weka £20 milioni mezani...Dogo huyu amejitahidi sana na ameonekena kifaa ndani ya Leicester City ambao karibu wananyakua ubingwa premiership...Kante aliingia Leicester City kwa dau la chini kidogo ya £6 milioni akitokea Caen...Bofya hapa upate habari zaidi.
CHINESE GRAND PRIX: ALONSO ARUHUSIWA KUSHIRIKI CHINESE GP
Fernando Alonso amekubaliwa kushiriki Chinese GP na madaktari wake baada ya ajali mbaya sana iliyomtokea katika mashindano yaliyopita...Katika ajali hiyo alikuwa akikimbiza gari yake spidi 180 mph na kugonga ukingo na gari kuzunguka hewani mana kadhaa kabla ya kutua chini...
Pamoja na kukubaliwa ameambiwa akisikia chochote mwilini asimamishe gari mara moja...Bofya hapa upate habari zaidi.
EUROPA LEAGUE 2016: LIVERPOOL YAIDUWAZA DORTMUND NA MASHABIKI WAKE
The Kop jana usiku paliwaka moto kwani Liverpool ilikuwa imeshajulikana inatolewa nje ya michuano ya Europa au 'Uefa ndogo' kwa msemo wa kitaa lakini la hasha...Kama umewahi kusikia timu inaitwa 'The Comeback Kings' basi jana hiko jina lilijulikana kama la Liverpool moja kwa moja...Mechi yao dhidi ya Dortmund haikuwa rahisi kabisa kwani Dortmund wamesimama na ndio walionza kufunga mabao...Liverpool mara 2 kwenye mechi hiyo walihitaji mabao matatu kufuzu...
Hali ilikuwa tete sana tena siku ambayo Liverpool walikuwa wanakumbuka miaka 27 iliyopita mashabiki 96 walipoteza maisha yao katika siku ya 'Hillsborough disaster'...Kabla mpira kuanza walitoa heshima kwa waliopoteza maisha kwa kukaa kimya kwa dakika 1...Dortmund walikuwa mbele mapema dakika ya 5 kupitia bao la Henrikh Mkhitaryan na muda mfupi badae Pierre-Emerick Aubameyang akapachika bao dakika ya 9...Mashabiki wakajua leo ndio bye bye lakini ngoma ikaendelea kuchezwa na Divock Origi aliwapa matumaini alipofunga baodakika ya 48...
Liverpool walianza kwa kushambuliwa sana na Dortmund ila badae waliweza kutulia na kucheza mpira wa maana...Reus wa Dortmund kwenye dakika ya 57 akapachika bao na kurudisha matumaini ya Liverpool nyuma....Dakika ya 60 Philippe Coutinho alifanikiwa kurudisha matumaini japi finyu lakini alibadelisha game...Dakika 10 baadda ya bao hilo Mamadou Sakho akapachika bao na sasa angalau matumaini yakarudi ingawa dakika zilikuwa zinayoyoma...
Dakika za lala salama umati wa the Kop uliruka juu kwa kushangilia sana baada ya bao la Dejan Lovren kutikisa nyavu....Kweli Liverpool imeshangaza hadi mashabiki kwa kuwa timu ambayo hata ikichapwa hurudisha mabao na kushinda...Bofya hapa upate habari zaidi.
Thursday, 14 April 2016
NBA: STEPHEN CURRY AVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE NA KUFIKIA 3 POINTS 400 MSIMU HUU
Stephen Curry anaendelea kuacha midomo ya mashabiki waazi huku akiendelea kuvunja rekodi mbali mbali...Curry amekuwa mtu wa kwanza kabisa toka ligi ianzishwe kufikia 3 points 400 kwa msimu mmoja na pia amefanikiwa kupata 3-points 10 katika game moja akivunja rekodi yake ya awali na pia wakati team yake ya Golden State Warriors wakivunja rekodi ya ushindi wa mechi 73 katima msimu mmoja...Golden State walifikia hiyo rekodi katika ushindi wao dhidi ya Memphis Grizzlies wa points 125-104...Bofya hapa upate habari zaidi.
KOBE BRYANT: KOBE BRYANT AGONGA POINTS 60 SIKU YAKE YA MWISHO
Kobe Bryant anajulikana kwa majina mengine maarufu sana 'The Black Mamba' au 'KB24' au 'Vino' alefanikiwa kuingiza points 60 katika game yake ya mwisho kabisa...
Wednesday, 13 April 2016
NBA: KOBE BRYANT AZUA GUMZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSTAAFU KWAKE LEO
Kobe Brant au kwa jina maarufu 'The Black Mamba' amezua gumzo kubwa sana nchini Marekeni na duniani kwa ujumla kutokana na mechi yake ya mwisho leo...Kobe ni kati ya wachezaji wakali sana waliowahi kucheza NBA na aliingia kwenye ligi akiwa mdogo akitokea high school...
Kobe anaastaafu kucheza basketball leo ikiwa anaingia uwanjani na Utah Jazz na uwanja umesha furika kwani hakuna hata ticket moja imebaki...Ticket zenyewe zilikuwa bei mbaya na kuzipata kwa mbinde sana...Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu sana duniani na mashabiki wa Kobe na basketball kwa ujumla itaweka historia ya aina yake kwani watu wengi sana wataangalia jinsi anavyoagwa...
Watu kati ya 400 na 500 wa habari wamepewa nafasi ya kuingia na kutangaza siku ya leo...Kobe leo anamalizia msimu wa 20 toka aanze kucheza NBA...Usikose game ya mwisho ya mkali wa basketball Kobe Bryant leo usiku...Bofya hapa upate habari zaidi
CHAMPIONS LEAGUE 2016: KEVIN DE BRUYNE AIPELEKA MAN CITY NUSU FAINALI KWA MARA YA KWANZA
Manchester City inaingia nusu fainali ya Champions League kwa mara ya kwanza kabisa kwa kumtoa PSG kwa aggregate ya 3-2...Watu wawili wakushukuru ni Joe Hart na Kevin De Bruyne...Hart alipangua mikwaju hatari mitatu na kuwalinda City mpaka Kevin De Bruyne alipopachika bao mnamo dakika ya 76....Umati wa watu 53,039 walishangilia sana bao lilipoingia na pia mwisho wa mchezo kwani ni historia kubwa katika club hiyo ya Man City...Bofya hapa upate habari zaidi.
CHAMPIONS LEAGUE 2016: RONALDO AIOKOA REAL MADRID
Madrid waliweza ball control vipindi vyote na pasi za uhakika wakati Woolfsbug wakichemsha hasa defense...
Pia hawakuwa na ari ya kusukuma mpira kama mechi ya awamu ya 1...Ronaldo sasa kwa ujumla ana mabao 460 na bado ana nafasi ya kuendelea kupata mabao lukuki...Bofya hapa upate habari zaidi.
Tuesday, 12 April 2016
TANZANIA GOLF UNION: TGU KUFUNDISHA WANAFUNZI GOLF
Tanzania Golf Union imeamua kufundisha Golf kwa wanafunzi ili kukuza vipaji na mchezo wa Golf kwa ujumla...Kufundisha watoto wa shule kutategemea upatikanaji wa vifaa alisema Mwenyeki wa TGU bwana Joseph Tango...Kwa sasa wamepata vifaa vichache vya kuanzia na wataanza na zoezi la chip and putt kabla ya kuendelea na mazoezi mengineBofya hapa upate habari zaidi.
Monday, 11 April 2016
NBA: GOLDEN STATE WARRIORS WAFIKIA REKODI YA CHICAGO BULLS YA 1995-96
Golden State Warriors wakiongozwa na Stephen Curry wameweza kufikia rekodi ya Chicago Bulls ya msimu wa mwaka 1995-96 ya kushinda mechi 72...Pamoja na hayo wanaweza kuvunja hiyo rekodi na kuwa na ushindi wa mechi 73 Jumatano wakiingia uwanjani na Memphis Grizzlies...Sasa Curry na wenzake wako juu kama Michael Jordan na wenzake kwa kuwa wachezaji na timu bora kwenye ligi ya NBA...Bofya hapa upate habari zaidi.
THE MASTERS 2016: DANNY WILLEtT KUTOKA ENGLAND ACHUKUA KOTI LA KIJANI
Danny Willett ameshangaza ulimwengu wa Golf duniani alivyoshinda Masters 2016 huko Agusta Georgia...Aliyekuwa anategemewa, Jodran Spieth, alichemsha kwenye shimo la 3 round ya mwisho na kusababisha Danny Willett ashinde kwa -5 (67)...Hakuna mtu alitegemea Willett kushinda kwani Jordan Spieth ilikuwa ashinde kilaini lakini mambo hayakumwendea vizuri...Willett mwenye umri wa miaka 28 ameshinda Major yake ya kwanza na toka miaka 20 iliyopita hakuna mtu kutoka England aliyeshinda...Lee Westwood alimaliza wa 2 akiwa na -2 (69) akiwa na Jordan Spieth...Paul Casey alimaliza wa 3 akiwa na score ya -1...Bofya hapa upate habari zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)























