Sunday 3 September 2017

TAIFA STARS: STARS WAILAZA BOTSWANA 2-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI JIJI DAR ES SALAAM


Taifa Stars wamefanikiwa kuwachapa wageni wao Botswana 2-0 ndani ya Uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam...
Manao yote hayo mawili yalitoka kwa Tanzanian international Simon Msuva anayeichezea timu ya Premier League ya Didaa Hassan El-Jadida ya nchini Morocco...

Mnamo dakika ya 6 hivi cheche ziliwaka baada ya Hamisi Abdallah anayeichezea Sony Sugar ya Kenya kumtupia pasi ndefu Msuva na baada ha ya hapo Muzamil Hassan kiungo wa Simba alipewa pasi safi na badae kidogo kuirudisha kwa Msuva kwa mbele ambapo Msuva alizama nayo ndani ya box na kuachia shuti hatari kabisa likimwacha kipa wa the Zebra Mwambule Masule akiduwaa kabisa huku nyavu zikitingishika...

The Zebras hawakuwa na kiwango chakutosha lakini walijaribu kuisumbua Stars kwa kutaka kuifunga mara 2 lakini safu ya ulinzi chini ya Kevin Yondan ilikuwa imara sana...

Nahodha wa Stars Mbwana Samatta nae alikuwa hatari kabisa kwenye lango la The Zebras mara kadhaa ingawa walidhibitiwa sana na wageni...

Msuva alikonga mioyo za washabiki kwenye mnamo dakika ya 63 alipopachika bao la 2 baada ya 1-2 safi na kifaa cha Simba Sports Club Ramadhan Kichuya.

No comments:

Post a Comment