Friday 1 September 2017

SIMBA SPORTS CLUB: KESI YA AVEVA NA NYANGE IMESOGEZWA MBELE MPAKA SEPTEMBA 8


Kesi inayowakabili rais wa Simba Sport Club Evans Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange imesogewa bele mpaka Septemba 8 kutokana na kutokamilika kwa upelelezi...
Aveva na nyange wanakabiliwa na mashtaka ya kugushi nyaraka na kutakatisha fedha zinazofikia shilingi milioni 600...

Kwa mujibu wa kesi, inasemekana Aveva alipokea pesa kutoka Simba Sports Club dola za kimarekani laki 3 ambazo inaonekana kama Simba walikuwa wanalipa deni kwa Aveva...

Pia inasemekana alienda CRDB Bank tawi la Azikiwe na kuwaambia hizo pesa ni za deni lake kwa Simba...

Aveva na Nyange wanatuhumiwa kufoji na kutakatisha pesa hizo kupitia benki nyingine ya Barclays tawi la Mikocheni ambapo walifankiwa kuzichukulia hizo pesa hapo.

No comments:

Post a Comment