Friday 2 December 2016

SIMBA SPORTS CLUB: KIPA MPYA KUTOKA GHANA AMESEMA ATAISAIDIA SIMBA KUPATA USHINDI


Kipa mpya, Daniel Agyei, anayetokea nchi ya Ghana huko magharibi mwa Afrika amesema ataisaidia Simba kupata ushindi msimu huu...
Kipa huyo alikuwa anaishezea timu ya Madeama inayotokea eneo la Tarkwa huko Ghana...Kipa huyo ameingia jijini Dar es Salaam Jumatano kwa mkataba wa miaka 2...Agyei amefurahishwa sana na mapokezi mazuri sana kutoka kwa mashabiki na uongozi wa Simba...Kipa huyo alikuwa pia anaichezea nchi yake ya Ghana kwenye kikosi cha vijana chini ya miaka 20 au maarufu kama Ghana U-20 na pia alishinda 2009 World Youth Championship...Itabidi Agyei ajitahidi sana ili apate namba ya kudumu kwenye timu ya Joseph Omog kwani kuna makipa wengine Peter Manyika na Vincent Angban.

No comments:

Post a Comment