Monday 12 December 2016

SIMBA SPORTS CLUB: SIKU YA MAAMUZI KATIKA KIKAO CHA DHARURA CHA UCHAMBUZI WA KATIBA YA SIMBA


Simba Sports Club wanakutana leo Police Officers Mess kujadili maamuzi muhimu sana ya katiba ya timu hiyo...Mkutano huu ni muendelezo ma mkutano uliofanyika July 31 mwaka huu...
Msemaji mkuu wa club ya Simba, Haji Manara, amesema mkutaho huu ni mwendelezo wa majadiliano ya mkutano uliopita ambao unataka kuleta mabadiliko katika timu hiyo...Katika mabadiliko hayo ni pamoja na kuanzisha kampuni na kuuza hisa kwa mwekezaji Mohammed Dewji...Dewji au "MO" kwa jina maarufu ametoa ofa yake ya bilioni 20 yakuchukua asilimia 51 ya hisa za Simba...Mkutano wa leo utaendelea baada ya wanachama wachache kupinga Mahakamani mkutano huu kufanyika...Baraza la wadhamini walipinga mkutano huu na kusema usifanyike mpaka uhakiki wa wanachama wa Simba nchini ukamilike na pia kutoa elimu kuhusu hisa za kampuni kwa wanachama wote nchini...Baraza hili linawajumbe Hamisi Kilomoni, Abdulwahab Abas, Ally Sykes (Marehemu) na Ramesh Patel.

No comments:

Post a Comment