Tuesday 27 December 2016

BOXING: FRANCIS CHEKA ASKEMA HAKUUZA MECHI


Francis Cheka bondia wa Tanzania (Bingwa wa WBF [Continental Africa] katika uzito wa Super Middleweight) alichapwa na bondia kutoka India Vijender 'Viju' Singh kwa TKO round ya 3 kati ya round 12 za ubingwa wa Mabara wa WBO Super-middleweight...
Pambano hilo lilifanyika jijini New Delhi usiku wa Decemba 18... Cheka amesema ushindi wa Singh una utata kwasababu akipaliwa na mate akatoa mouth guard na kumwomba kocha wake Abdallah Salehe ambadilishie mouth guard na baada ya hapo alishangaa Sing ananyanyuliwa mkono kashinda...


Wadau wanasema Cheka alikuwa yuko fiti sana na labda aliuza pambano...Tusubiri kuona bingwa Cheka akifanya mambo tena hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment