Monday 1 January 2018

VODACOM PREMIER LEAGUE: YOUNG AFRICANS YACHAPWA NA MBAO FC | 2-0


Habib Hajji Kiyombo wa Mbao FC ameibuka kuwa kinara dhidi ya Young Africans (Yanga) kwa kufunga mabao yote mawili ndani ya CCM Kirumba jijini Mwanza...
Mabao hayo yalipatikana mnamo dakika ya 53 na 68. Mbao FC sasa imefikisha pointi 14 kati ya mechi 12 walizocheza. 

Yanga wao wana pointi 21 kati ya mechi 12 walizocheza. 

Azam FC wana lambalamba wako mbele kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 26 sambamba na Simba Sports Club. 

Yanga sasa iko nje ya tatu bora wakiwa wamezidiwa na Singida United.

No comments:

Post a Comment