Sunday 5 February 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: SIMBA SPORTS CLUB YAIRARUA MAJI MAJI 3-0


Simba Sports Club au wana wa Msimbazi wameirarua vibaya Maji Maji huko Songea 3-0...
Simba ambayo inaifukuza Young Africans (Yanga) ilipata ushindi huo muhimu sana kwani wasinge pata pointi 3 mbio za ubingwa zingekuwa ndoto.

Kutokana na huo ushindi Simba sasa wana pointi 48 katika mechi 21 walizocheza.

Wanapishana pointi 1 na mabingwa watetezi Yanga...Ibrahim Salum Hajib Migomba ndio aliyetingisha nyavu mnamo dakika ya 19.

Bao hilo lilifungwa kwa kishwa alivyopata kross ya Shiza Ramadhan Kichuya.

Kwenye dakika ya 63 kifaa hatari cha Simba Saidi Hamisi Ndemla alifanya vitu vyake na kuandika bao la 2 ambalo lilitoke kwenye kona ya James Kotei.

Laudit Mavugo alimvusha beki kanzu na kuandika bao dakika ya 88.

Maji Maji chini ya kocha Kali Ongala ambae amezaliwa hapa Tanzania na anatokea Congo walijitahidi sana.

Walikosa bao dakika ya 45.

Kipindi cha 2 walishambulia hapa na pale lakini hawakuweza kufanya mambo.

No comments:

Post a Comment