Saturday 4 February 2017

VODACOM PREMIER LEAGUE: YOUNG AFRICANS YAMCHAPA STAND UNITED 4-0


Dar es Salaam Young Africans (Yanga) jilifanya mauji hatari sana kwa kuitundika Stand United mabao 4-0...
Mbio za ubingwa sasa ni za moto kweli kweli kwani Simba sasa inabidi washinde mechi yao ya leo kama wanataka kupambania ubungwa...Kwa sasa Yanga wana pointi 49 kati ya mechi 21...Simba wana pointi 44 kati ya mechi 20...Donald Dombo Ngoma aliipatia Yanga bao la kwanza kabisa alivyo pokea kross ya Msuva sakika ya 17...Ngoma alikuwa hajacheza kwa takriban wiki 4 hivi...Dakika ya 26 Msuva akatingisha nyavu na kuipatia Yanga bao la 2...


Msuva anaongoza ligi kwa kuwa na mabao mengi kuliko wachezaji wote...Amefunga mabao 10...Obrey Chirwa aliifungia Yanga bao la 3 mnamo dakika ya 46 kwa shuti kali la mbali...Nadir "Cannavaro" Haroub funga bao la mwishi ambalo lilitokana na kross ya Juma Abdul.

No comments:

Post a Comment