Monday 19 September 2016

CAF U-17 CUP OF NATIONS: SERENGETI BOYS YAITANDIKA CONGO 3-2


Timu ya taifa ya Vijana ya U-17, Serengeti Boys, imefanikiwa kuwachapa Congo Brazzaville mabao 3-2 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam...Serengeti Boys wako mbio kuwania ticket ya kushiriki Madagascar 2017...Mashindani ya Mataifa ya Afrika yatafanyika nchini Madagascar mwaka ujao...Yohana Mkomola ndie aliyepachika mabao mawili kipindi cha kwanza na kipindi cha pili alifunga Issa Makamba...Serengeti Boys wakifanikiwa kuwatoa Congo mechi ya marudiano watafuzu kuingia Madagascar.

No comments:

Post a Comment