Tuesday 13 September 2016

VPL: SIMBA SC YAISHUSHA YANGA NAFASI YA 2


Simba SC inaendelea vizuri na Vodacom Premier League baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam...Simba ilipata point 3 muhimu kupitia kwa Ibrahimu Ajib na Laudit Mavugo kipindi cha 2...Yanga imeshushwa nafasi na Simba na bado mapambano yanaendelea na ni marefu...Simba inasaka ubingwa toka mwaka 2012...Kwa sasa Azam na Simba wako sawa sema labda wana lambalamba jina lao limeanza na herufi A tu lakini wote wana points 10...Uzuri wa mechi ya Simba ni mashabiki ambao walijaa kushuhudia bao la Ajib...Sehemu nyingine Mbeya Prisons waliibuka kidedea dhidi ya Toto Africans kwa bao 1 kwa mtungi ndani ya Uwanja wa Sokoine. 

No comments:

Post a Comment