Tuesday 6 September 2016

VPL: MBEYA CITY WAKO TAYARI KUWAKABILI AZAM FC


Mbeya City FC iko tayari kuikabili Azam FC ndani ya uwanja wa Sokoine mwisho wa wiki...Baada ya kuwa na ziara kanda ya ziwa kwa muda kipenzi cha wana Mbeya sasa wako fiti kuchuana na Azam FC...Kwa mujibu wa Meneja wa timu Geoffrey Kapeta timu itapumzika siku moja kwa ruhusa ya kocha Kinnah Phiri na kesho itaendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya game ya mwisho wa wiki...Meneja Kapeta amesema wachezaji wote wana afya nzuri kwa mujibu wa taarifa ya daktari wa timu.

No comments:

Post a Comment