Monday, 19 June 2017

ALVARO MORATA: KIFAA CHA REAL MADRID ALVARO MORATA KIMEPATA JIKO


Alvaro Morata kifaa cha Real Madrid kimepata jiko na kufunga harusi ya kifahari huko Venice Italia...Morata amemuoa mchumba wake Alice Campello katika sherehe ya kuvutia sana huko Venice...

Morata anasakwa sana na timu kubwa duniani ikiwemo Manchester United na AC Milan...


Toka Morata arejee Real Madrid akitokea Juventus amekuwa hapewi nafasi na Zidane na hiyo imemfanya awe na hasira ya kutaka kutoka Real Madrid...

Harusi yake ilifanyika Basilica Del Redentore na baada ya kufunga ndoa walipanda boti ya kifahari na kuzungushwa mji huo wa Venice ambao umezungukwa na maji kila sehemu...


Agent wake Morata alisema mtu wake amepewa ofa nzuri sana na Manchester United ambao wanataka kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic.