Tuesday, 6 June 2017

SPORTPESA SUPER CUP: YOUNG AFRICANS (YANGA) YATINGA NUSU-FAINALI


Dar es Salaam Young Africans (Yanga) wamefanikiwa kutinga nusu-fainali ya SportPesa Super Cup baada ya kuilaza Tusker ya Kenya 4-2 kwenye matuta ndani ya Uwanja wa Uhuru...
Timu hizo zilitoka sare ya 0-0 dakika zote 90...Deogratius 'Dida' Munishi kipa namba 1 wa Yanga ndie aliyefanikisha zoezi la matuta na kuwapeleka Yanga nusu-fainali...

Dida alipangua penalty ya Clifford Alwanga na badae kidogo Stephen Owusu aligonga mwamba wa juu...

Waliofunga penaly zao ni Nahodha Nadir 'Cannavaro' Haroub ambae ndio aliyefunga tuta la kwanza...

Wengine ni Obrey Chirwa anayetokea Zambia, Maka Edward Mwakalukwa na Said Mussa...

Tusker wafungaji walikuwa Noah Wafula na Brian Osumba...Yanga itakutana na AFC Leopards ya Kenya tarehe 8 Juni ndani ya Uwanja wa Uhuru.