Monday, 29 May 2017

MBWANA SAMATTA: NAHODHA WA TAIFA STARS MBWANA SAMATTA ATUPIA BAO LA 20 ULAYA


Mbwaba Samatta ambae ni forward wa K.R.C. Gemk na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, au 'Stars' anaendelea vuwashangaza wazungu huko Ulaya kwa ufungaji wake hodari...
Samatta sasa amefikia mabao 20 toka ajiunge na Genk huku akiwa amecheza mechi 59...

Samatta aliongeza idadi ya mabao kwenye mechi ya Kundi B la kuwania tiketi ya kucheza UEFA Europa Leage dhidi ya Sint-Truiden...

Sint-Truiden walichapwa 3-0 na Genk...


Bao la kwanza lilitoka kwa kiungo mkongwe Thomas Buffel mwenye umri wa miaka 36 mnamo dakika ya 32 na bao la 2 lilitoka kwa Jean-Paul Boetius dakika ya 43...

Bao la Samatta lilipatikana kwenye dakika ya 55 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jakub Brabec anayetokea Jamhuri ya Czech.