Wednesday, 17 May 2017

VPL: YOUNG AFRICANS (YANGA) UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA UNANUKIA


Young Africans (Yanga) karibu wananyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu sana kama VPL au Vodacom Premier League...Yanga wamefanikiwa kuusogelea ubingwa tena baada ya kuichapa watoto wao, Toto Africans, 1-0 ndani ya Uwanja wa Taifa...Bao hilo pekee lilitoka kwa Burundian international Amissi Tambwe...

Mechi ilikuwa na hekaheka toka mwanzo ambapo Toto walikoswa bao mapema dakika kama ya tatu vile...Walishambuliana kwa zamu lakini Yanga wakafanikiwa kuilaza Toto 1-0 mnamo dakika ya 81 kupitia cross ya Juma Abdul Jaffer Mnyamani...

Yanga sasa ina pointi 68 kati ya mechi 29...

Yanga wanahitaji draw tu iliwawe mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara...

Wana mechi ya mwisho dhidi ya Mbao FC...Hata hivyo kwa hazina ya mabao ubingwa utakuwa wao tu kwani Simba wanatakiwa washinde 13-0 dhidi ya Mwadui FC.