Saturday, 6 May 2017

HIMIDI MAO MKAMI: 'NINJA' ANAENDELEA VIZURI NA MAJARIBIO YA KUJIUNGA NA RANGERS YA DENMARK


Kiungo mkabaji wa timu ya Taifa Himidi Mao Mkami anaendelea vizuri na tizi la kupimwa kabla hajaingizwa rasmi Rangers ya Denmark...

Tayari Himiri ameshapiga tizi mara 2 na kikosi cha akiba na atapumzika kidogo ndipo atajufua na timu ya kwanza ya Rangers...

Mkami atatumia siku 10 za tizi kabla ya kurudi nyumbani na kuendelea na timu yake ya Azam FC...

Mkami atapata fursa ya kucheza mechi kamili na timu ya akiba dhidi ya AC Horsens...Ni mechi ya timu za akiba ndani ya ligi yao ya Danish Superliga.