Wednesday, 22 March 2017

TAIFA STARS: HIMIDI MAO MKAMI NA JONAS GERALD MKUDE MANAHODHA WAPYA STARS


Kocha mkuu wa Taifa Stars, Saidi Mayanga, amewachagua Himidi Mao Mkami kutoka Azam FC na Jonas Gerald Mkude wa Simba Sports Club kuwa manahodha wasaidizi wa Taifa Stars...


Uamuzi huo umetokana na nahodha wa zamani John Raphael Bocco kuwa majeruhi toka Januari...Mbwana Ally Samata bado ataendelea kuwa nahodha mkuu wa Taifa Stars...Samatta anaigia nchini leo usiku tayari kujiunga na kikosi cha Stars...


Stars wataingia uwanjani na Botswana Machi 25 na tarehe 28 watacheza na Burundi...

Kikosi kamili cha Stars;

Makipa: Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi (Yanga), Said Mohammed (Mtibwa Sugar)

Walinzi (Pembeni Kulia): Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga)

Walinzi wa (Pembeni Kushoto): Mohammed Hussain (Simba), Gabriel Michael (Azam)

Walinzi wa Kati: Vincent Andrew (Yanga), Samim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba), Erasto Nyoni (Azam)

Viungo wa Kuzuia: Himid Mao (Azam, Jonas Mkude (Simba)

Viungo wa Kushambulia: Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domoyo (Azam), Muzamil Yassin (Simba)

Viungo wa Kulia: Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba)

Viungo wa Kushoto: Farid Musa (Teneriffer, Hispania), Hassan Kabunda (Mwadui)

Washambuliaji: Mbwana Samatta (K.R.C. Genk, Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Simba), Mbaraka Yusuf (Kagera Sugar), Abdul-Rahman Musa (Ruvu Shooting)