Tuesday 14 March 2017

TAIFA STARS: KOCHA MAYANGA AWAITA WACHEZAJI 26 TAYARI KWA MAANDALIZI YA CHAN NA AFCON


Kocha wa timu ya Taifa, Salum Mayanga, amewaita wachezaji 26 kwasababu ya maadalizi ya michezi ya kufuzu Ubingwa wa Mataifa ya Africa (CHAN) na Komba la Mataifa ya Afrika (AFCON)...Wachezaji hao hajawaita mabeki wa Young Aafricans (Yanga) Kevin Yondan na Juma Abdul pamoja na Mwinyi Hajji Mngwali...Wachezaji wa Azam Aggrey Morris na David Mwantika nao hawajajumuishwa kwenye kikosi hicho...

Kisa cha kutowaita wachezaji wa Zanzibar ni kwamba Mayanga anasubiri maamuzi ya kikao CAF ambacho kitafanyika Machi 16...Maamuzi hayo yanaweza kuipa Zanziba uanachama wa CAF...Mayanga alisema "Kama Zanzibar itapewa uanachama CAF, ina maana hatutaendelea kuchanganyika na Zanzibar, lakini kama ikikwama, basi nitawarudisha wachezaji wa Zanzibar, nimeacha nafasi nne kwaajili hiyo."...

Kikosi cha Mayanga hicho hapo chini: 

Makipa; Aishi Manula (Azam), Said muhammed (Mtwibwa Sugar) na Deogratius 'Dida' Munishi (Young Africans (Yanga)). Mabeki; Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Young Africans (Yanga)), Mohammed 'Tshabalala' Hussein (Simba), Gabriel Michael (Azam), Andrew Vincent (Young Africans (Yanga)), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abidi banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam). 

Viungo; Himidi Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum 'Sure Boy' Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

Washambuliaji: Mbwana Samatta (K.R.C. Genk, Ubelgiji), thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Ajib (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting)



No comments:

Post a Comment